Ushauri Tafadhali

Joined
Mar 24, 2009
Posts
76
Reaction score
14
Waungwana naomba mnisaidie mawazo kwenye hili.

Nina mke na watoto watatu, na tunamshukuru Mungu maisha yanakwenda vizuri.

Kuna binti niliwahi kuwa naye siku za nyuma wakati niko sekondari. Tulikuwa tukionana wakati narudi likizo huko kijijini kwetu. Baadae ule uhusiano haukuendelea baada ya yeye na wazazi wake kuhamia mkoa mwingine ambako nasikia baadae aliolewa. Hii ni kama miaka 17 iliyopita. Pale kijijini walibaki dada zake na ndugu wachache.

Mimi niliendelea na maisha yangu wakati huo sekondari na kisha chuo na sasa nina shughuli zangu binafsi.

Hivi karibuni nimepata simu kutoka kijijini kwetu kwamba kuna binti mdogo mtoto wa wa yule msichana wa zamani amekuja kwa ndugu zake pale kijijini na kudai kwamba ameambiwa na mama yake kwamba mimi ndiyo baba yake mzazi. Huyo binti amemaliza darasa la saba huko kwa mama yake.


Habari hii imenishangaza sana hasa ukizingatia kwamba wakati uhusiano wetu unakwisha miaka hiyo ya 1995 hakuwahi kuniambia kwamba alikuwa mjamzito. Na hata kipindi chote hicho hajawi kuwasiliana na mimi kwa chochote wala ndugu zake waliobaki kijini hawakuwahi kuniambia chochote mimi au ndugu zangu licha ya kuwa huwa narudi kijijini mara nyingi.


Napata wakati mgumu sana juu ya hili hasa ukizingatia kwamba sasa hivi nina familia yangu. Ningependa hili swal liishe kabla halijaleta mchafuko wowote kwenye ndoa yangu.

Naomba ushauri wenu please.
 
Simple.

Compute mara ya mwisho wewe na yeye kujamiiana ilikuwa lini.

Kisha linganisha majibu na miaka ya huyo binti ambaye anadai wewe ni daddy wake.

Kama umri wake unaangukia ndani ya kipindi ambacho wewe na mama yake mlikuwa mna do the dew, basi mkapime DNA.
 
wala lisikupe shida si mkeo anajua kwamba ulikuwa na gf before yeye? ama hukumwambia kabisa? kama ulimwelezaga basi mwambie kuna tatizo imejitokeza kwa upole kisha muulize kwa tatizo kama hili tufanyeje? kisha wewe ndipo utakapo mweleza mawazo yako sasa baada ya kumsikiliza na kujua mtazamo wake.
 
Ungejua umri wa huyo binti(mtoto wako) ingekuwa muhimu sana kabla haujafanya maamuzi mengine.
 

Nashukuru kwa ushauri wako. Lakini vipi kuhusu muda uliopita mpaka sasa. Hata kama DNA ikionesha kweli ni wangu, nahisi itaniwia vigumu sana kuupokea huo ukweli.
 
Nashukuru kwa ushauri wako. Lakini vipi kuhusu muda uliopita mpaka sasa. Hata kama DNA ikionesha kweli ni wangu, nahisi itaniwia vigumu sana kuupokea huo ukweli.

Vipimo vikionyesha kuwa mwana ni wako basi huna jinsi zaidi ya kuwajibika na kujenga mahusiano ya karibu.
 
Nashukuru kwa ushauri wako. Lakini vipi kuhusu muda uliopita mpaka sasa. Hata kama DNA ikionesha kweli ni wangu, nahisi itaniwia vigumu sana kuupokea huo ukweli.

Sasa vipimo vionyeshe kuwa ni wa kwako kisha ukatae majibu ya vipimo ndio vipi?!

Hujui sababu iliyomfanya amlete kwako sasa, labda ana sababu madhubuti.

Usikimbie majukumu
 
Nyani Ngabu amemaliza.....
pia kama ni kweli huyo mtoto ni wako, huna haja ya kuhofia jinsi ya kumweleza mkeo, ni kitu ambacho hukuwa unakijua na hukutarajia....pia ni zao la uhusiano wa kale kabla yake, unless kama mke si mwelewa.......

ila bado najiuliza kama huyo binti kweli alikuwa mjamzito inakuwaje familia yake isikwambie hadi sasa?
mama wa mtoto yupo?
kama yupo akueleze kwa nini hakusema?




 
Last edited by a moderator:
kweli kiburudisho chako cha zamani cha kijijini kweli yaani sasa ni miaka unaletewa mtoto kama vipi chukua mwanao huyo anawezakuja kukutoa baadae..
 
Watoto wengi wanateseka kwa sababu makosa ya wazazi.
 
Pole sana kwa tatizo lako, labda niseme hivi unapopata habari za tatizo kamahilo kwanza usipaniki, kaachini tulia then tafuta pesa kidogo mchukue mtoto mkapime DNA. Japo inagarimu kiasifulani chamsingi upate uhakika.
 
Everyone will not get everything,
This is the RULE of LIFE,
Dont try to get which is not yours.
But dont dare to loose which is yours..!
Understand

nakushauri uchunguze kwanza ukweli wa hlo jambo kwa kwenda mwenyewe kijijini na kuongea na huyo x wako kuhusu huyo mtoto

Ongea na mkeo kuhusu hlo coz mie sion shida coz huyo mtoto kama kweli wako alipatikana kabla hujakuwa na yy so naamin ataelewa kama ni muelewa.........

fanya DNA kuhakikisha kama kweli ni mwanao au siyo.......

kama ni mwanao be a man, anza matunzo ya mwanao si kifedha tu hata mahusiano yake na ndugu zako wewe, mkeo na wanao wa ndani ya ndoa..............

Good luck
 
ningekuwa na uwezo ningkuwa King Mswati kwa watoto.

Yaani vipimo vioneshe wako afu ishindwe kukubali ukweli??? How??

Mi nadhani mtoto ni faida siku zote??
 
Mkuu ni vyema uende kijijini ukamtafute huyo x-gf wako ili akwambie nini kilisababisha asikwambie kipindi chote hicho..
Then ukiridhika mkapime DNA..

Duuh..mwanamke asingiziwi mimba...Ila wanaume kaaazi kweli kweli.
Pengine utakuta kuna kidume kilishikishwa kuwa ni mtoto wake later on akajakushtuka,ndo maana ameamua aseme ukweli..Huenda ikawa ni damu yako kweli..Usipuuzie mkuu.
 
Kazi kubwa kama ingekuwa bidada uliyemuacha miaka hiyo kitambo anataka au analazimsha uhusiano ,

lakini kama anasema ana mtoto wako tena mtoto mkubwaa amekulelea na inaonekana bi mkubwa hana hiyana anaweza kukupa umlee,

kwahiyo hapo cha kufanya ni kupima dna tu ujihakikishie mtoto ni wa kwako, kisha unamueleza mkeo, atakuelewa tu.
 
hapa naona watu wengi wana recommend kupima DNA ivi mnajua bei ya kupima DNA? mwananchi wa kawaida tu anaweza kuafford kipimo hicho au tunasema tu kwa sababu uwa tunasikia kuna kipimo cha DNA?
 
hapa naona watu wengi wana recommend kupima DNA ivi mnajua bei ya kupima DNA? mwananchi wa kawaida tu anaweza kuafford kipimo hicho au tunasema tu kwa sababu uwa tunasikia kuna kipimo cha DNA?

What is the other option? Unataka akubali bila kujua kwa hakika kama ni wake au sio. Binti kamaliza darasa la 7, akimchukua na kuanza kumtunza atatumia gharama kiasi gani mpaka aanze kujitegemea au kuolewa?

Halafu hakutakuwa na mahusiano mazuri kama mzee ana shaka na uzazi wa huyo mtoto. Ana sababu za kuwa na mashaka, DNA is the best option. Hata kama ni 5mil, jipige uende.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…