mtuporimtupori
Member
- Mar 24, 2009
- 76
- 14
Waungwana naomba mnisaidie mawazo kwenye hili.
Nina mke na watoto watatu, na tunamshukuru Mungu maisha yanakwenda vizuri.
Kuna binti niliwahi kuwa naye siku za nyuma wakati niko sekondari. Tulikuwa tukionana wakati narudi likizo huko kijijini kwetu. Baadae ule uhusiano haukuendelea baada ya yeye na wazazi wake kuhamia mkoa mwingine ambako nasikia baadae aliolewa. Hii ni kama miaka 17 iliyopita. Pale kijijini walibaki dada zake na ndugu wachache.
Mimi niliendelea na maisha yangu wakati huo sekondari na kisha chuo na sasa nina shughuli zangu binafsi.
Hivi karibuni nimepata simu kutoka kijijini kwetu kwamba kuna binti mdogo mtoto wa wa yule msichana wa zamani amekuja kwa ndugu zake pale kijijini na kudai kwamba ameambiwa na mama yake kwamba mimi ndiyo baba yake mzazi. Huyo binti amemaliza darasa la saba huko kwa mama yake.
Habari hii imenishangaza sana hasa ukizingatia kwamba wakati uhusiano wetu unakwisha miaka hiyo ya 1995 hakuwahi kuniambia kwamba alikuwa mjamzito. Na hata kipindi chote hicho hajawi kuwasiliana na mimi kwa chochote wala ndugu zake waliobaki kijini hawakuwahi kuniambia chochote mimi au ndugu zangu licha ya kuwa huwa narudi kijijini mara nyingi.
Napata wakati mgumu sana juu ya hili hasa ukizingatia kwamba sasa hivi nina familia yangu. Ningependa hili swal liishe kabla halijaleta mchafuko wowote kwenye ndoa yangu.
Naomba ushauri wenu please.