Ushauri: Tanzania iwafukuze mabalozi wa Marekani na Uingereza kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi yetu

Una elimu gani aisee!
 
Haina haja ya kuwafukuza, waacheni tu! Walitabiri tutaokotwa mizoga barabarani na haijatokea. Sasa hivi wenyewe wanashangaa kwanini Afrika corona haijaenea sana. Kwa hiyo hata hawa mabalozi watakuja kukanusha vipeperushi vyao wenyewe
 
Tunategemea hao wakubwa kwa mambo mengi yakiwemo ulinzi na usalama,WB,IMF,Science na Techinogia,Utalii,Tafiti,biashara,Elimu ya vyuo vikuu,ustaarabu n.k
UK na USA ni wanachama wa kudumu UN wana kura ya veto umesahau yaliompata Salim alipokataliwa na USA wakati akigombea ukatibu mkuu wa UN?
Je wewe umeishapata sifa hizo au unajiandaa kuishi sayari nyingine?
 


huwezi kukata tawi ulilo likalia..
 
Unafikiri mambo ni rahisi kama unavyofikiria hivi unajua mfadhili mkubwa wa hizo ARV unazokunywa hapo ni nani?
 
Solution ni kufukuza tu,
Sijui hata kama huko mtaani kwenu mnasalimiana na majirani.

Kila mtu kwenu mbaya, ok sawa, tukutane October.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo ni sawa na mwanamke kumfukuza mmewe ndani ya nyumba wakati ndiye anayemlisha! Tunawafukuzaje wakati wao ndiyo wanatupa misaada?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…