USHAURI: TFF ni muda sasa umewadia wa kuanzisha Reserve league (Professional development league)

Tipstipstor

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2021
Posts
1,528
Reaction score
3,352
Ahlan wa Sahlan

Katika kuzunguka kwangu katika mataifa ya ulaya nimekutana na mfumo huu wa ligi za reserve wengine hupenda kuuita professional development leagues.Ni mfumo wa ligi unaohusisha wachezaji vijana kutoka academies za timu zinazoshiriki ligi kuu za nchi husika,hujumuisha vijana wa academies wasiozidi umri wa miaka 21 pamoja na wachezaji wachache ambao hawapati nafasi /muda wa kucheza katika timu A. Yaani katika reserve team wale wachezaji ambao hawapati game time katika team A au wake ambao wamerejea kutoka katika majeraha, au ambao wamepewa adhabu za kinidhamu na timu husika wanapewa nafasi ya kuja kucheza katika reserve league pamoja na vijana wa academies wasiozidi umri wa miaka 21 na wakiwa katika form nzuri basi kocha wa team A anaweza kuwarejesha kuanza katika team A, au vilevile kocha anaweza kuchagua hawa U21 players kuja kujiunga na timu ya wakubwa.

Ni mfumo mzuri sana ambao hutumiwa na mataifa yaliyoendelea kisoka, sasa hv tunaona wachezaji mfano wa chama langu Simba mfano Akpan,Dejan,Okwa na kapama hawapo ktk machaguzi ya mwalimu Matola ( Mgunda ), sasa badala ya kukaa benchi tu mwezi mzima bila ya kupata game time ni bora wangekuwa wanacheza dakika 90 kwenye hizo reserve league ili kujiweka fiti.

Pia dhumuni kubwa wa hizi reserve /development leagues ni kuibua vipaji vya wachezaji u21 .
 
Hizo academy za klabu ziko wapi? Kwanza Klabu nyingi ni masikini na haziwezi kuendesha timu mbili. Timu za wakubwa tu zinaishi Kwa kubangaiza halafu uwaongezee mzigo wa kuendesha timu nyingine.

Kwenye ligi ambayo kuna klabu inakosa nauli ili kushiriki kimataifa halafu unataka hiyo klabu iliyokosa nauli iwe na timu mbili.
Klabu nyingi ni oya oya sababu mashabiki hawaendi viwanjani mpaka iwe ni Simba au yanga inacheza.

Uchumi hakuna wa klabu zetu kuwa na timu mbili na ndio maana ukiachana na Simba queens na yanga princes timu nyingi za wanawake zinazoshiriki ligi kuu hazihusiani na timu za wanaume zinazoshiriki ligi kuu.
 
Soka letu litachukua muda sana kukua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…