Mkulima na Mfugaji
JF-Expert Member
- Jul 26, 2013
- 1,047
- 1,832
Habari ndugu Wana ujenzi, mwaka huu niliweka malengo ya kuweka akiba benki kidogo kidogo kwa ajili ya ujenzi, nilianza kuweka hela ya bati za kawaida, nikafikisha hela ya bati 70 nikaweka hela ya Mbao za kupaulia na ya fundi paa.
Kuanzia mwezi huu nimeanza kuweka hela ya Tofali ila mazingira niliyopo naweza kupata Tofali za kuchoma kwa urahisi, kwani karibu na kiwanja Kuna kichuguu kizuri naweza kukinunua na shambani Kuna mti wa muembe mkubwa naweza kuutumia kwa ajili ya kuchoma Tofali, yaani nikiwa na milioni 1 naweza kufyatua Tofali zaidi ya Elf 15 na kuzichoma.
Sasa niko njia panda kujua Tofauti ya ubora kati ya Tofali za block (za saruji) na Tofali za kuchoma, naombeni ushauri kwa anaefahamu