Ushauri, Tofali za block vs Tofali za kuchoma

Ushauri, Tofali za block vs Tofali za kuchoma

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
1,047
Reaction score
1,832
Habari ndugu Wana ujenzi, mwaka huu niliweka malengo ya kuweka akiba benki kidogo kidogo kwa ajili ya ujenzi, nilianza kuweka hela ya bati za kawaida, nikafikisha hela ya bati 70 nikaweka hela ya Mbao za kupaulia na ya fundi paa.

Kuanzia mwezi huu nimeanza kuweka hela ya Tofali ila mazingira niliyopo naweza kupata Tofali za kuchoma kwa urahisi, kwani karibu na kiwanja Kuna kichuguu kizuri naweza kukinunua na shambani Kuna mti wa muembe mkubwa naweza kuutumia kwa ajili ya kuchoma Tofali, yaani nikiwa na milioni 1 naweza kufyatua Tofali zaidi ya Elf 15 na kuzichoma.

Sasa niko njia panda kujua Tofauti ya ubora kati ya Tofali za block (za saruji) na Tofali za kuchoma, naombeni ushauri kwa anaefahamu
 
Ubora kwa maana katika Long life na hata kwa gharama tofali za kuchoma ni chaguo sahihi, sema zina usumbufu sana hasa ikiwa unanunua kutoka sites wanapozichoma ila kama mzigo utaandaa mwenyewe hapo safi.

Kingine ujenzi wake huwa unaenda taratibu sana na changamoto yake nyingine ili kuanza kuishi ndani atleast hata kwa ndani upige plasta kuhepusha wadudu kujificha tofaut na block na pia si kila fundi anaziwezea kuzijenga wengi wao huishia kupindisha kuta.
 
Na je? tofali za kuchoma zinafaa kujengwa Kwa tope au cement.
 
Naombeni ushauri, je kipi bora; tofari choma ya 11inch, kina 5inchs, upana 6inchs Au Block ya inch 5?
 
Unataka kujegea mkoa/wilaya gani??
Maana nivyema ukaweka location unapo panga kujega ili wajuzi waweze kukushauri vyema kutokana na aina ya udongo/ardhi ya eneo husika.
 
Ubora kwa maana katika Long life na hata kwa gharama tofali za kuchoma ni chaguo sahihi, sema zina usumbufu sana hasa ikiwa unanunua kutoka sites wanapozichoma ila kama mzigo utaandaa mwenyewe hapo safi.

Kingine ujenzi wake huwa unaenda taratibu sana na changamoto yake nyingine ili kuanza kuishi ndani atleast hata kwa ndani upige plasta kuhepusha wadudu kujificha tofaut na block na pia si kila fundi anaziwezea kuzijenga wengi wao huishia kupindisha kuta.
Thanks
 
Back
Top Bottom