Ushauri: Tofali za Kuchoma Vs Tofali za block

Ushauri: Tofali za Kuchoma Vs Tofali za block

Wild fauna

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Posts
461
Reaction score
189
salaam wadau!
ningependa kupata ufafanuzi na ushauri kabla sijafanya maamuzi. Nipo kwenye harakati za kuanza kujenga, ningependa kupata ushauri kuhusu tofali.
Ninaishi moshi mjini na nategemea kuanza ujenzi sooon. je ni tofali zipi imara kati ya tofali za kuchoma na tofali za block?
ushaur wenu wadau tafadhali
 
Za kuchoma ni imara na zinapendezesha nyumba kama ukiamua kufanya urembo.
 
Ninaamini za kuchoma ni imara zaidi kwakuwa hazina mchanganyiko wa kemilkali zozote...
 
Hata za blocks zinakuwa imara. Jibu lako linategemea other factors kufikia maamuzi.
interms of gharama tofali za kuchoma zipo cheap. hofu yangu gharama ndogo isisababishe nyumba isiwe imara
nahitaji uimara wa nyumba
 
Nashangaa sana kusikia tofali za kuchoma ETI ni imara kuliko za block ? ? nasema wazi haiwezekani kabisa, Labda na tena kwa mashaka mseme UKUTA wa matofali ya kuchoma sbb ya either double layer or kulaza tofali ILI uwe mpana kuliko ule UKUTA wa block , kwa maana hiyo yawezekana UKUTA wa T za kuchoma waweza kuwa imara kuliko UKUTA wa block tofali za inch 5 or 4 za kusimamisha.

NB; UIMARA wa tofali pekee waweza kuwa sio uimara wa nyumba na kuta zake,
Kama lengo ni nyumba Imara waone wataalam wakushauri vizuri.
 
salaam wadau!
ningependa kupata ufafanuzi na ushauri kabla sijafanya maamuzi. Nipo kwenye harakati za kuanza kujenga, ningependa kupata ushauri kuhusu tofali.
Ninaishi moshi mjini na nategemea kuanza ujenzi sooon. je ni tofali zipi imara kati ya tofali za kuchoma na tofali za block?
ushaur wenu wadau tafadhali
Za block ukikutana na zile hazijawekewa ratio nzuri ya cement utalia nakuambia,yani huwa zinapukutika nyumba itapata nyufa hapo mbeleni, uwe makini na sehemu unaponunua hizo za block kujua ratio ya cement kwa uimara wa tofali
 
Pia kitu ni kile kile wakati wakipiga plasta idadi ya mifuko kwa vymbani ndani na nje ni hiyo hiyo iwe tofali ya block ama ya kuchoma, cha msingi ni wewe tu chaguo lako sema pia kama ni tofali ya kuchoma kuna wale wanaochomea mapumba hizo sio tofali zikimbie achana nazo
 
Ni ukweli tofali za kuchoma ziko imara kuliko za block?
 
Nashangaa sana kusikia tofali za kuchoma ETI ni imara kuliko za block ? ? nasema wazi haiwezekani kabisa, Labda na tena kwa mashaka mseme UKUTA wa matofali ya kuchoma sbb ya either double layer or kulaza tofali ILI uwe mpana kuliko ule UKUTA wa block , kwa maana hiyo yawezekana UKUTA wa T za kuchoma waweza kuwa imara kuliko UKUTA wa block tofali za inch 5 or 4 za kusimamisha.

NB; UIMARA wa tofali pekee waweza kuwa sio uimara wa nyumba na kuta zake,
Kama lengo ni nyumba Imara waone wataalam wakushauri vizuri.
Tatizo unasahau kuwa tofali za block wengi wanapunja ratio ya cement hawa suppliers, na kama unavyoona cement inapanda bei kila siku unategemea mfanyabiashara wa T blocks hatapunja cement usiwe na dhana ya kukariri uwe unafanya kautafiti kwanza
 
Uchakachuaji unaweza kufanyika kote - kwenye blocks na kwenye za kuchoma, japo yamkini ya blocks kuchakachuliwa ni kubwa zaidi.

Lakini ukilinganisha tofali zilizotengenezwa vizuri kote kote - block ni imara sana kuliko tofali za kuchomwa.
 
unajenga moshi sehemu gani? na ni nyumba ya vyumba vingapi?
wapo jamaa wanajenga na kufytua tofali zinaitwa interlock blocks.
 
Moshi msaranga mkuu. bei ya hiz inter lock blocks ni sh ngap? zinapatikana maeneo gan?

ok msaranga............................ yupo jamaa anaziuza hizo tofali moja sh 500 na anajenga pia yeye yupo dar na moshi huwa anafikaga, simu yake ni 0716023456 mfano nyumba ya vyumba 3 tofali 7000 mcheki insta interlocking blocking
 
mkuu natafuta kiwanja msaranga, bonite au sango mbele ya kiboloroni nitapata kweli na bei zake vipi ni nyumba ya vyumba 3 ya makazi najenga, niko moshi mkuu emu nicheki pm
 
Back
Top Bottom