dndagula,
Naunga mkono hoja, ila hili pia tulitungie sheria kama ilivyo picha ya rais kwenye fedha, iliishia kwa rais Nyerere na Mwinyi.
Siku za viongozi wa kitaifa zimeishia kwa Nyerere na Karume kama Waasisi. Tusisibiri hadi viongozi hawa watangulie mbele ya haki ndipo tutambue mchango wao na kuwaenzi, kama wafanyavyo Wakatoliki kwenye canonisation process, bali tuwaenzi wangali hai kwa kutenga siku maalum ya kuwa reflects not necessarily lazima iwe ni public holiday.
Mkapa ni baba wa Demokrasia, tutenge siku, tumreflect Mkapa, kwa kuita "Benjamin Mkapa Democracy Day" to reflect demokrasia aliyoiamini Mkapa, tuwaalike viongozi waliopo na 'watu wa maswali magumu', wawasute viongozi wanaolia 'machozi ya mamba' tuwaulize au tuwasute kwanini wanamlilia Mkapa kwa uchungu na kumsifu sana sasa baada ya kutangulia mbele ya haki lakini wakati yuko hai, hawakumuishi?
Demokrasia ya kweli inajengwa kwa kutoa haki kwa wote, Mkapa na Kikwete kwa kuzingatia uchanga wa demokrasia ya vyama vingi, kwenye nafasi zao za uteuzi wa wabunge 10 wa kuteuliwa na rais, waliteua wabunge wawili kutoka upinzani, sasa subirieni muone ni wapinzani wangapi watapenya uchaguzi wa 2020 na kuingia Bungeni halafu shuhudieni jinsi watu wanavyo muishi Mkapa kwenye demokrasia!
Watu wamemlilia Mkapa kwa machozi ya uchungu, naomba uchungu ule sasa uelekezwe kwenye kumuishi na kuyatenda yale Mkapa aliyo yaamini, vinginevyo baadhi ya machozi ya waliomlilia Mkapa, ni machozi ya mamba!
P