Ushauri, uanzishaji wa kiwanda cha kisasa cha fanicha

Ushauri, uanzishaji wa kiwanda cha kisasa cha fanicha

1404639207773.jpg1404639234254.jpg1404639265899.jpg
 
Ni biashara nzuri ingawa manunuzi yake ni taratibu
Lakini jaribu kuwa na wazo tofauti katika fani hii ya furniture pia unaweza ukanunua antiques, nikuwekee picha ambazo huenda ukapendelea kuwa nazo hizo kwenye store kama utapata wabunifu wazuri

Nashukuru sana, na watu kama ninyi nawahitaji sana ktk ushauri. Mnanipa faraja sana.
 
Binafsi naongezea.

Angalia makampuni mengine ya furniture duniani yanafanya nini. Angalia bidhaa zao jinsi zilivyo simple na creative. Na wewe fanya hivyo.

Pia, nakushauri ukiweza uzalishe hata furniture zenye frames za chuma au plastic. Usi-base sana kwenye mbao tu.

Na kuongezea unaweza ukawa na mafundi special kwa ajili ya kudesign furniture finishing za nyumba. mf, kujengea makabati ya jikoni, sebuleni au vyumbani..

Na kwenye kujitangaza unaweza kuwatengenezea masuper star furniture bora kwa bei ya discount ila kwa masharti wafanya advertising kwenye page zao za social network.
 
Ndugu zangu,

Nimefikiria vya kutosha na nimepata wazo la biashara la kutengeneza na kuuza fanicha.

Nimeamua nianze kwa kuajiri mafundi wanaoweza kutengeneza fanicha kama makabati, sofa, vitanda, milango, madirisha, meza, viti nk. Nitaanza na mafundi 10.

Vilevile nimefanya utafiti mashine, kama mashine za kuranda mbao, kukata mbao, kutoboa mbao, kushape mbao nk.

Kwa ushauri mbalimbali juu ya matumizi ya kila mashine, nimeona kwa KAMTAJI kangu naweza kununua mashine 20 za aina tofauti.

Nimepata kaeneo Dodoma, ambako nitajenga karakana ya kutengenezea fenicha then nitatafuta show room kwa ajili ya kuuzia.

Je wadau naweza kupata soko ktk mikoa gani ktk mikoa mingine nje ya Dodoma? ukiondoa gharama za management like kulipa gharama za umeme, mafundi, machanic engineers, sales officers, managers etc. vipi naweza kupata faida kweli?
Angalizo: hakikisha unakuwa na quality finishing. JKT wanatengeneza furnitures lakini finishing bab kubwa.

kuhusu masoko, jitangaze tu. Weka fb, instagram, jf etc. Weka mapicha kibao. Utatoka tu, kila la kheri
Poa mkuu ukihitaji ushauri zaidi ni PM niko mjasiria mali kwa miaka mingi na nna different lines za business with enough experience.
Mkuu hii idea ni babu kubwa sana,nilishawahi kuifikiria hasa baada ya kutembelea kiwanda flani kilikua kinaitwa Kilwa woodforms, kilikuwa Mandela road Dar es Salaam(sasa kimefungwa).
Kikubwa ni angalia wapi utapa mbao za bei nzuri hasa mininga na mikongo. Pia ubunifu wa finishing hasa kwa mbao nyeupe.
Pia tumia catalogue za nje kuweza kutengeneza bidhaa zako.

My take,
Mchina ni fake sana lakini zina vision ya kuvutia sana na bei ni poa, hii ni changamoto kwako.
Wazo zuri sana, ushauri ni kwamba jaribu kuwa creative na kuwa na new ideas katika kuunda furnitures, utapata soko, cha msingi uwe na tools and machine za kileo, jengine mbao hakikisha ziwe kavu. Kwa mfano nimegundua na fanya uchunguzi mwenyewe, unakuta kitanda kizuri or mlango baada ya muda mfupi mlango unawacha gaps na kupinda, or kitanda vile vile.

Jengine jinsi ya kuupinda ubao, aisee nimeona utaalamu wa kupinda ubao katika discovery channel, how it's made program. Wanatumia stim kupinda ubao, maji ya moto makali yenye kutoa stim na ubao kuwekwa juu, baada ya ubao kupata uvuke mkali unakuwa kama plastic unbelievable, na unaupinda inavyo taka, sijawahi kuona utaalamu kama huo Tanzania labda kwa kutumia moto.
 
Back
Top Bottom