Ushauri : Ufugaji wa punda

Wang Shu

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2014
Posts
2,562
Reaction score
3,715
Wakuu salaam

Nafikilia kuanza kufuga punda kwa ajili ya kilimo kubebea mizigo miepesi niendapo shamba na kurudisha baadhi ya mazao nyumbani.
Kuna mtu aliniambia kuwa ni maliasili kwaiyo mamlaka husika lazima ikupe kibali cha ufugaji ni kweli? Maana Wamasai wengi wanamiliki kiholela tu hawasumbuliwi.

Pia nataka nikiwanunua niwasafilishe umbali kama mikoa 3,
Kwa anaefahamu utaratibu wakumiliki punda anifahamishe tafadhali...
 


Punda wa kawaida siyo nyara wala maliasili. Au una maanosha Pundamilia? Utaratibu wake ni kama unavyofuga ng’ombe tuuu


—————
Bavuvi
 
Mbona huko singida punda ni kitoweo kuzidi hata ng'ombe.
 
Punda wa kawaida siyo nyara wala maliasili. Au una maanosha Pundamilia? Utaratibu wake ni kama unavyofuga ng’ombe tuuu


—————
Bavuvi
Hapana sio pundamilia namaanisha punda wakawaida tunaoishi nao kuna mtu nilimuulizia akanipa vitisho kuwa na maliasili
 
Umezaliwa Marekani? Texas? Make kwa hata mtoto ambaye hajaanza shule anajua punda ni mifugo kama.walivyo mifugo mingine sasa kama wewe kwa umuro huo naambiwa Punda ni Mnyama wa Polini basi kazi ipo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wazo lako ni zuri sana,
Tatizo wabongo wengi akili zetu ni kama vile zimefungwa kamba, halafu mbaya zaidi ni kupenda kuigana igana na kukatishana tamaa.
Wengi wetu wanafuga punda kwa ajili ya matumizi yao tu ya nyumbani hua hawafikirii kuwafuga na kuwazalisha kibiashara.
Kuna kipindi soko la punda lilikua ni kubwa sana hapa nchini mpaka ikafikia kua ni tishio la kuweza kupotea kabisa punda katika nchi yetu, hii ni baada ya wachina kuwanunua na kusafirisha nyama ya punda nchini kwao.
Serikali kwa kipindi hicho ilipiga marufuku biashara ya kuuza nyama ya punda ila kwa sasa sina uhakika kama marufuku hio bado inaendelea.
Kuhusu kuwasafirisha pia sina uhakika kama ni kosa au la.
Jitahidi kuulizia kwenye ngazi tofauti za serikali ili kujiridhisha kabla ya kufanya maamuzi.
 
Sio kosa kusafirisha,ila kuna taratibu za kusafirisha wanayama kutok eneo moja kwenda lingine.
Aongee na afisa/bwana mifugo wa eneo lake ampe utaratibu wa usharishaji.
 
Sio kosa kusafirisha,ila kuna taratibu za kusafirisha wanayama kutok eneo moja kwenda lingine.
Aongee na afisa/bwana mifugo wa eneo lake ampe utaratibu wa usharishaji.
Bei ya kununua punda 1 ikoje?
 
Aliekwambia ni nyara Alikutapeli

Usichukulie kila cha kuambiwa ni kweli
 
Ni wazo zuri ila uzazi wao unachukua muda mrefu. sidhani kama itakuwa ni biashara ya kukupa mrejesho mapema. Lakini pia punda siyo nyala ya serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…