Smartgeneration
New Member
- Jul 18, 2022
- 2
- 5
Utumishi wa uwe mwisho miaka 10
Habari za majukumu wana jamii forum, andiko langu la leo ni juu ya ukomo wa utumishi wa umma, kwa mtazamo wangu ni bora zaidi ukomo wa kutumikia serikali upunguzwe hadi kifikia miaka 10, kwa maana ya kwamba serikali itengeneze utaratibu wa wahitimu wa vyuo kuajiliwa mapema pale tu wanapo hitimu masomo yao ya ngazi za juu, hivyo basi mifumo rafiki ya utambuzi wa hitimu iwe ni ya kusajiliwa kwenye mfumo mmoja pale tu wanapohitimu hii ni kwa kuzingatia mwaka wa kuhitimi, hii itasaidia watu kuingia mapema katika ajira za serikali wakiwa na umri mdogo matharani nikiajiliwa na miaka 21 nitastaafu nikiwa na miaka 31, hapa nitakua na nguvu za kutosha za kuweza kumudu mambo mengine kama kuweza kusoma fani zingine, kujiajili kwa kupitia marupurupu yangu ya serikalini.
Lengo kuu la kuweza kufanya hivi ni kiruhusu nafasi ya watu wengi kupata nafasi ya kuajiliwa serikalini ivyo kupunguza hadha ya ukosefu wa ajira kwa muda mrefu, pia kuweza kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi, vile vile itakuza uchumi wa mtu mmoja mmoja katika jamii.
Vile vile hii italeta mtazamo chanya kwa wastaafu kwa kuwa hivi ilivyo sasa watu wamekua wakistaafu wwkiwa na umri mkubwa na kupata kiasi kikubwa cha fedha na kuwa mzigo kwa familia na mstaafu, kwasababu mstaafu anakua amechoka kiakili hivyo anakuwa na mzigo mkubwa wa kumiliki fedha nyingi bila ya kujua namna ya kuzizalisha katika shughuli mbalimbali, hii ni tofauti na mtu akistaafu na umri mdogo, ukistaafu na umri mdogo unakua chachu ya maendereo katika jamii kwasababu unakua umevuna mari kwa muda mfupi na akili ya kuweza kuziongoza fedha za kustaafu inakua kubwa.
Vile vile mtu akistaafu akiwa na umri mdogo anaweza kujiendereza kimasomo katika nyanja nyingine kama ufundi, siasa, biashara na kadharika, na hapa pia ndipo CV ya mtu itakua na mashiko mapana, kwamba CV itaonesha nilishaajiliwa Serikalini katika nyanja fulani na hivyo itaongeza thamani katika sekta binafsi za nje na ndani pia.
Asanteni
Nawasilisha