Ushauri: Umri unaenda sina ninachomiliki

Sigara Kali

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
3,623
Reaction score
8,442
Salaam wanajamvi,

Jamani naomba mnipe ushauri kutoka kwenu hasa kwa wale waliofanikiwa kimaisha.

Kwanza naweza sema hapa Tanzania kusoma sana ndo kuukaribisha umasikini tu.

Kijana mimi wa kitanzania mwenye elimu ya Bachelor degree na Postgraduate Diploma hadi sasa nagonga 30 years sina cha maana ninachomiliki katika maisha yangu.

Sijui kwa sababu nimetumia muda mwingi kusoma, au hii familia niliyozaliwa ya umasikini ndo chanzo hata sijui.

Nilisoma kwa mkopo wa serikali na postgraduate nikafadhiliwa kwa kujua kwamba nikimaliza nitaingia kwenye system kupitia ualimu wa masomo ya arts imekua ndivyo sivyo.

Umri unaenda sina mtaji sina ndugu wa kuniwezesha kwa chochote kazi zimekua ngumu so nategemea kudra za Mwenyezi Mungu labda nitafanikiwa.

Najishughulisha na shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato lakini hakikidhi mahitaji napata hela ya kula, kulipa kodi miezi 2 2 au 1.

Nina mtoto anaishi kwa mama yake, najisikia vibaya kumwona mwanangu anakua lakini hadi sasa baba yake similiki chochote kitakachomsaidia, mama yake ndo anauwezo kwa sasa wa kumjengea mazingira bora coz kipato chake kinatosha kabisa.

Sina ninachomiliki jamani, naombeni ushauri njia bora ya kuishi, namna ya kufanya ili nami niweze kutoka katika dimbwi hili la umaskini, nakiri kwamba nimesoma na kwa sasa sina ndoto tena ya kutaka kuajiriwa nina ndoto ya kujiajiri lakini sijui wapi napata mtaji, labda itokee nipate ajira ya uhakika ya kupata salary bila usumbufu hapo nitajipanga kudunduliza hela nipate japo mtaji.

Umasikini mbaya sana. Na elimu ya Tanzania inachochea umasikini.

Nipeni ushauri jamani ili mwaka 2018 niwe mtu mpya nijue nini nifanye nami nimiliki japo biashara hata ya kuuza juice, banana power hata shujaa vodka.

Ushauri tafadhali, sihitaji maneno ya kejeli nina frustration zangu.

NAWASILISHA
 
Usijali.. Zamu yako itafika.. Viongozi wengi na wenye pesa na majumba ya kifahari wengi wamevipata vitu hivyo wakiwa na 50+ years hasa baada ya kupanda vyeo.. Ndio maana wengi ukiwaona ni mabosi ila wana njaa kali 😡... Yani hata wakipelekewa kusaini vocha ya laki moja wanaitolea macho mpaka unawashangaa!
 
Umesema unafanya shughuli ndogo ndogo zinazokusaidia kulipa kodi, ni shughuli zipi hizo na mtaji wake ni kiasi gani? Tunaweza kushauriana namna ya kupanua hizo hizo shughuli zako ndogo na zikawa kubwa
 
Umeandika kwa uchungu sana, ni kweli wakati mwingine unaweza kuhisi hauna bahati kwenye maisha kwa kukosa hiki na kile, mara nyingi katika nyakati hizo huwa napenda kwenda muhimbili au ocean road hospital kama nipo Tanzania, pale nitaona watu wenye shida za ukweli, kwa kufanya hivyo, nitatazama mbingu na kumshukuru Mungu baba kwa kuniinulia uso wake na kunifadhili, afya njema na uhai ni zawadi kubwa kwangu kutoka kwa Mungu, hayo mengine ni ziada. Usikate tamaa endelea kupambana maisha hayana formula, wala hautaweza kuipata formula hapa JF.
 
Kwaio akae hadi miaka 50...?! Usubiri kupandishwa vyeo?!
 
dah pole sana mkuu... hapo ni kujiongeza tu kukaa karibu na wasiosoma wanaofanya ujasiriamali.. utajofunza mengi sana ya mtaji mdogo na jinsi ya kukuza mtaji.. ukiwa karibu na wamachinga, mama ntilie, na wengineo vijiweni....

kuna vingi tu unaweza fanya kwa mtaji wa laki moja sisi wasomi hatuvijui.. ila wasiosoma wanavijua
 
Umesema unafanya shughuli ndogo ndogo zinazokusaidia kulipa kodi, ni shughuli zipi hizo na mtaji wake ni kiasi gani? Tunaweza kushauriana namna ya kupanua hizo hizo shughuli zako ndogo na zikawa kubwa
Nafundisha chuo masomo ya hotel na tourism ila kulipana ni kwa shida sana tena kidogo kidogo so unajikuta huna cha maana unachokifanya kupitia malipo hayo zaidi ya kula na kulipa kodi tena kwa mbinde kwelikweli,endapo kama ningekua nalipwa kwa wakati tena hela yote nna uhakika ningepata mtaji tu ila ndo hivyo magumashi tupu mkuu
 
kuna concept moja ukiielewa inaweza kuchange your life forever (kama utaifanyia action)

"Money owned= value created/delivered to others"

na "consumption doesn't care about education level"
JE, ushawah kwenda kununua kitu unachoitaji, lkn b4 hujalipa ukaulizia "eti muuzaji,una degree ngapi? ".... NO, kama unacho kitu ninachoitaji...you got my money, haijalishi nimesoma/sijasoma....ndio maana utakuta watu std seven wana hela kibao kuliko graduates.....making money is about solving the needs/wants of people... That's how you'll get their money

AF kwny VALUE ss, the more value u provide via solving needs/wants....The more money you'll make....

Soma these books: UNSCRIPTED na THE MILLIONAIRE FASTLANE
 
pole,, ndio Tanzania yetu hii, kwenye maelezo yako hujaieleza vyema , umesema kuna shughuli ndogo unazozifanya unishia kupanta hela ya kula na pango, ungeweka wazi ni shughuli gani ? mtaji wake upoje ? ulianzia wapi na kwa sasa umefikia wapi ? baada ya hayo sisi tungekuja na possible solution nini kifanyike kukuza kipato chako pengine kuna mahali unakosea
 
MKUU USIJALI, HUMU WAPO WENG KAMA WEWE SEMA WEWE UMEKUWA JASIRI UMEELEZA KINAGAUBAGA.

SASA MKUU KAMA HUYO DEMU WAKO MAMBO YAKE NI MURUA KWANINI USIBUNI MRADI UKAMSHRIKISHA AKAKUWEZESHA MTAJI? KAMA KWELI MNAPENDANA NA MNAELEWANA.

ILA ONYO MKUU, ISIJE AKAKUWEZESHA UKATUSUA UKAMBWAGA, UTAPATA LAANA KUU.

FANYA HVYO MKUU ILA UWE MWAMINIFU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…