Ushauri: Umri unaenda sina ninachomiliki

Ushauri: Umri unaenda sina ninachomiliki

Omba mkopo kwa mama mtoto uanze kufuga kuku au hata kulima mchicha. Kwa joto la Tz, kuna wanaouza maji baridi, tafuta pa kuanzia.
 
Salaam wanajamvi,

Jamani naomba mnipe ushauri kutoka kwenu hasa kwa wale waliofanikiwa kimaisha.

Kwanza naweza sema hapa Tanzania kusoma sana ndo kuukaribisha umasikini tu.

Kijana mimi wa kitanzania mwenye elimu ya Bachelor degree na Postgraduate Diploma hadi sasa nagonga 30 years sina cha maana ninachomiliki katika maisha yangu.

Sijui kwa sababu nimetumia muda mwingi kusoma, au hii familia niliyozaliwa ya umasikini ndo chanzo hata sijui.

Nilisoma kwa mkopo wa serikali na postgraduate nikafadhiliwa kwa kujua kwamba nikimaliza nitaingia kwenye system kupitia ualimu wa masomo ya arts imekua ndivyo sivyo.

Umri unaenda sina mtaji sina ndugu wa kuniwezesha kwa chochote kazi zimekua ngumu so nategemea kudra za Mwenyezi Mungu labda nitafanikiwa.

Najishughulisha na shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato lakini hakikidhi mahitaji napata hela ya kula, kulipa kodi miezi 2 2 au 1.

Nina mtoto anaishi kwa mama yake, najisikia vibaya kumwona mwanangu anakua lakini hadi sasa baba yake similiki chochote kitakachomsaidia, mama yake ndo anauwezo kwa sasa wa kumjengea mazingira bora coz kipato chake kinatosha kabisa.

Sina ninachomiliki jamani, naombeni ushauri njia bora ya kuishi, namna ya kufanya ili nami niweze kutoka katika dimbwi hili la umaskini, nakiri kwamba nimesoma na kwa sasa sina ndoto tena ya kutaka kuajiriwa nina ndoto ya kujiajiri lakini sijui wapi napata mtaji, labda itokee nipate ajira ya uhakika ya kupata salary bila usumbufu hapo nitajipanga kudunduliza hela nipate japo mtaji.

Umasikini mbaya sana. Na elimu ya Tanzania inachochea umasikini.

Nipeni ushauri jamani ili mwaka 2018 niwe mtu mpya nijue nini nifanye nami nimiliki japo biashara hata ya kuuza juice, banana power hata shujaa vodka.

Ushauri tafadhali, sihitaji maneno ya kejeli nina frustration zangu.

NAWASILISHA
kwa kuwa huu uzi utatolewa na kwa sasa sina muda wa kuchangia kwa kadri ninavyotaka na huwenda ukawa msaada basi naomba ni pm ili hata kama uzi sikuukuta nikupe majibu ninayofikiria.
 
Mda
Usijali.. Zamu yako itafika.. Viongozi wengi na wenye pesa na majumba ya kifahari wengi wamevipata vitu hivyo wakiwa na 50+ years hasa baada ya kupanda vyeo.. Ndio maana wengi ukiwaona ni mabosi ila wana njaa kali 😡... Yani hata wakipelekewa kusaini vocha ya laki moja wanaitolea macho mpaka unawashangaa!
Mdanganye!
 
Mkuu toka jitose ukasake pesa shida kubwa unategemea mno shule/elimu kiuhalisia haina mchango kiivyo kwenye kutafuta na kupata pesa..!

Mimi mbona 30 plus, but sina chochote but soon nitapata tuu, chanji life style unavyoishi na badili mazingira na mbinu unazotumia kusaka pesa.
 
Watoto wa siku hizi bwana yaani miaka 30 ndio unajiona umri umeenda sana.......!!??

Tatizo vijana mnaishi maisha ya kukariri sana na kuigana.........

Ishi maisha yako , panga mipango yako kwa mazingira yako....

Jitihada haishindi kudra.....

Wewe una panga na Mungu na yeye anapanga yake.......

Bora uzima na afya njema
 
Watoto wa siku hizi bwana yaani miaka 30 ndio unajiona umri umeenda sana.......!!??

Tatizo vijana mnaishi maisha ya kukariri sana na kuigana.........

Ishi maisha yako , panga mipango yako kwa mazingira yako....

Jitihada haishindi kudra.....

Wewe una panga na Mungu na yeye anapanga yake.......

Bora uzima na afya njema
Ushauri na kejeli...hakuna miaka midogo wala mikubwa yote anatupa Mungu , kuna wengi walitaman wafike miaka hio hawakufika ...wewe kama una zaid ya hapo usijione wewe ndo mkubwa hapa duniani, na kudharau miaka ya wengine,
 
" Imenigusa sana nilipojaribu kuvaa viatu vyako katika fikira zangu"

Wengi wetu tulitegemea elimu zetu ndizo zitakazotukwamua lakini kwa baadhi imekuwa kinyume.

Sasa ni wakati wa kujifunza kwa bidii kutoka kwa wasio na elimu kama zetu na wamefanikiwa kwa kujishusha.
Wakati huo huo uendelee kushukuru kwa Baraka na Neema nyingi ambazo Mwenyezi Mungu amekujalia ambapo kubwa zaidi ni PUMZI na UHAI uliojaliwa hadi Leo hii.
Kuna wenzako ambao walifanikiwa kielimu, vyeo na nafasi katika umri mdogo zaidi yako ila Leo hawapo tena duniani na hawakuondoka na chochote walichomiliki, pia wapo waliofanikiwa kupata mafanikio katika umri wa miaka 50 na hadi Leo bado wanaishi.

Endelea kumshukuru Mungu na ukiomba huku ukijishughulisha kwa bidii na IPO siku utafanikiwa ni mambo ya wakati tu utafika wakati wako utatoka
 
I feel you brother. Umejizungumzia wewe kama umenizungumzia mimi na hii BAEd yangu inanifanya najichukia na kujutia muda niliopoteza chuoni. Naelekea kukata tamaa kabisa .Eee mola nisaidie [emoji24] [emoji24]



Jimbombo ngavu malafyalee
 
Kati ya watu usiotakiwa tegemea ni
Ndugu (Tumbo Moja au W Mbali)
Familia
Marafiki

Ukiwategemea Hawa utakufa masikini, hata wawe nacho hawawezi kukusaidia zaidi watapenda uwe hivyo ili uwaheshimu



Umenena vyema.

Anachokipitia jamaa, watu wengi wanapitia ikiwemo mimi.


Alichokisema, nimekipitia.


Nilidharauliwa kwa umasikini wangu japo ni digrii, ila sasa ninaheshimika eti kwa pesa zangu, na sasa wananipiga mizinga, japo sina pesa kihivyo.


Ndugu, marafiki, wengi ni wanafiki tu.
 
Ushauri na kejeli...hakuna miaka midogo wala mikubwa yote anatupa Mungu , kuna wengi walitaman wafike miaka hio hawakufika ...wewe kama una zaid ya hapo usijione wewe ndo mkubwa hapa duniani, na kudharau miaka ya wengine,

Nadhani hukunielewa
 
Kati ya watu usiotakiwa tegemea ni
Ndugu (Tumbo Moja au W Mbali)
Familia
Marafiki

Ukiwategemea Hawa utakufa masikini, hata wawe nacho hawawezi kukusaidia zaidi watapenda uwe hivyo ili uwaheshimu
Yaan mkuu una akil sna , hakika halio ndo hali halisi haswa

Nina kaka angu yupo uk hapa bongo ana majumba hayana idadi
Ma eka ya mashamba had mengine hayajui

Ila kumseidia mtu shida yaan kukupa kamtaj hawez labda sh 10000 ili sku yapili umuombe tena aone huwezi ishi bila yeye nikaona. Bora nijiongeze saiv sina habar nae kabisa japo km ni kaka baba mmoja ma mmoja ila sina mawasiliano nae tena nafanya yangu

Jaman chonde chonde msitegemee vya ndugu mtakufa masikini
 
Back
Top Bottom