Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kwa kuwa huu uzi utatolewa na kwa sasa sina muda wa kuchangia kwa kadri ninavyotaka na huwenda ukawa msaada basi naomba ni pm ili hata kama uzi sikuukuta nikupe majibu ninayofikiria.Salaam wanajamvi,
Jamani naomba mnipe ushauri kutoka kwenu hasa kwa wale waliofanikiwa kimaisha.
Kwanza naweza sema hapa Tanzania kusoma sana ndo kuukaribisha umasikini tu.
Kijana mimi wa kitanzania mwenye elimu ya Bachelor degree na Postgraduate Diploma hadi sasa nagonga 30 years sina cha maana ninachomiliki katika maisha yangu.
Sijui kwa sababu nimetumia muda mwingi kusoma, au hii familia niliyozaliwa ya umasikini ndo chanzo hata sijui.
Nilisoma kwa mkopo wa serikali na postgraduate nikafadhiliwa kwa kujua kwamba nikimaliza nitaingia kwenye system kupitia ualimu wa masomo ya arts imekua ndivyo sivyo.
Umri unaenda sina mtaji sina ndugu wa kuniwezesha kwa chochote kazi zimekua ngumu so nategemea kudra za Mwenyezi Mungu labda nitafanikiwa.
Najishughulisha na shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato lakini hakikidhi mahitaji napata hela ya kula, kulipa kodi miezi 2 2 au 1.
Nina mtoto anaishi kwa mama yake, najisikia vibaya kumwona mwanangu anakua lakini hadi sasa baba yake similiki chochote kitakachomsaidia, mama yake ndo anauwezo kwa sasa wa kumjengea mazingira bora coz kipato chake kinatosha kabisa.
Sina ninachomiliki jamani, naombeni ushauri njia bora ya kuishi, namna ya kufanya ili nami niweze kutoka katika dimbwi hili la umaskini, nakiri kwamba nimesoma na kwa sasa sina ndoto tena ya kutaka kuajiriwa nina ndoto ya kujiajiri lakini sijui wapi napata mtaji, labda itokee nipate ajira ya uhakika ya kupata salary bila usumbufu hapo nitajipanga kudunduliza hela nipate japo mtaji.
Umasikini mbaya sana. Na elimu ya Tanzania inachochea umasikini.
Nipeni ushauri jamani ili mwaka 2018 niwe mtu mpya nijue nini nifanye nami nimiliki japo biashara hata ya kuuza juice, banana power hata shujaa vodka.
Ushauri tafadhali, sihitaji maneno ya kejeli nina frustration zangu.
NAWASILISHA
Story of my life aiseeKati ya watu usiotakiwa tegemea ni
Ndugu (Tumbo Moja au W Mbali)
Familia
Marafiki
Ukiwategemea Hawa utakufa masikini, hata wawe nacho hawawezi kukusaidia zaidi watapenda uwe hivyo ili uwaheshimu
Mdanganye!Usijali.. Zamu yako itafika.. Viongozi wengi na wenye pesa na majumba ya kifahari wengi wamevipata vitu hivyo wakiwa na 50+ years hasa baada ya kupanda vyeo.. Ndio maana wengi ukiwaona ni mabosi ila wana njaa kali 😡... Yani hata wakipelekewa kusaini vocha ya laki moja wanaitolea macho mpaka unawashangaa!
That TrueKati ya watu usiotakiwa tegemea ni
Ndugu (Tumbo Moja au W Mbali)
Familia
Marafiki
Ukiwategemea Hawa utakufa masikini, hata wawe nacho hawawezi kukusaidia zaidi watapenda uwe hivyo ili uwaheshimu
Ushauri na kejeli...hakuna miaka midogo wala mikubwa yote anatupa Mungu , kuna wengi walitaman wafike miaka hio hawakufika ...wewe kama una zaid ya hapo usijione wewe ndo mkubwa hapa duniani, na kudharau miaka ya wengine,Watoto wa siku hizi bwana yaani miaka 30 ndio unajiona umri umeenda sana.......!!??
Tatizo vijana mnaishi maisha ya kukariri sana na kuigana.........
Ishi maisha yako , panga mipango yako kwa mazingira yako....
Jitihada haishindi kudra.....
Wewe una panga na Mungu na yeye anapanga yake.......
Bora uzima na afya njema
I feel you brother. Umejizungumzia wewe kama umenizungumzia mimi na hii BAEd yangu inanifanya najichukia na kujutia muda niliopoteza chuoni. Naelekea kukata tamaa kabisa .Eee mola nisaidie [emoji24] [emoji24]
Kati ya watu usiotakiwa tegemea ni
Ndugu (Tumbo Moja au W Mbali)
Familia
Marafiki
Ukiwategemea Hawa utakufa masikini, hata wawe nacho hawawezi kukusaidia zaidi watapenda uwe hivyo ili uwaheshimu
Ushauri na kejeli...hakuna miaka midogo wala mikubwa yote anatupa Mungu , kuna wengi walitaman wafike miaka hio hawakufika ...wewe kama una zaid ya hapo usijione wewe ndo mkubwa hapa duniani, na kudharau miaka ya wengine,
Haha princess ariana unazingua ujue[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]maisha ya bongo mwisho wa siku unajikuta unamiliki Two pair of balls... pole sana mkuu
Yaan mkuu una akil sna , hakika halio ndo hali halisi haswaKati ya watu usiotakiwa tegemea ni
Ndugu (Tumbo Moja au W Mbali)
Familia
Marafiki
Ukiwategemea Hawa utakufa masikini, hata wawe nacho hawawezi kukusaidia zaidi watapenda uwe hivyo ili uwaheshimu