Ushauri: Umri unaenda sina ninachomiliki

We siyo graduated ni graditude huwezi kuwa zoba kwa kiasi hicho nikimuona MTU ana degree halafu analalamika ajira natamani nimtemee mate huna Tina kwa taiga hili kabisa .si ajabu umeacha mashamba kijijini nawe IPO mjini unabanana na washua wakati umeacha Mali ,Mimi na degree ya HRM nibahatika kufanya field wilaya flani hadi Leo nafanya shughuri zangu kwenye wilaya hiyo na sina mpango wa kuajiliwa kabisa .

We ni faller sana, hivi kila mtu anaweza kua kama wewe? Unajua exposure yake? Umri keshasema ni kitu kinamuumiza na mtoto juu bila asset.
 
Salaam wanajamvi,

Jamani naomba mnipe ushauri kutoka kwenu hasa kwa wale waliofanikiwa kimaisha.

Kwanza naweza sema hapa Tanzania kusoma sana ndo kuukaribisha umasikini tu.

Kijana mimi wa kitanzania mwenye elimu ya Bachelor degree na Postgraduate Diploma hadi sasa nagonga 30 years sina cha maana ninachomiliki katika maisha yangu.

Sijui kwa sababu nimetumia muda mwingi kusoma, au hii familia niliyozaliwa ya umasikini ndo chanzo hata sijui.

Nilisoma kwa mkopo wa serikali na postgraduate nikafadhiliwa kwa kujua kwamba nikimaliza nitaingia kwenye system kupitia ualimu wa masomo ya arts imekua ndivyo sivyo.

Umri unaenda sina mtaji sina ndugu wa kuniwezesha kwa chochote kazi zimekua ngumu so nategemea kudra za Mwenyezi Mungu labda nitafanikiwa.

Najishughulisha na shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato lakini hakikidhi mahitaji napata hela ya kula, kulipa kodi miezi 2 2 au 1.

Nina mtoto anaishi kwa mama yake, najisikia vibaya kumwona mwanangu anakua lakini hadi sasa baba yake similiki chochote kitakachomsaidia, mama yake ndo anauwezo kwa sasa wa kumjengea mazingira bora coz kipato chake kinatosha kabisa.

Sina ninachomiliki jamani, naombeni ushauri njia bora ya kuishi, namna ya kufanya ili nami niweze kutoka katika dimbwi hili la umaskini, nakiri kwamba nimesoma na kwa sasa sina ndoto tena ya kutaka kuajiriwa nina ndoto ya kujiajiri lakini sijui wapi napata mtaji, labda itokee nipate ajira ya uhakika ya kupata salary bila usumbufu hapo nitajipanga kudunduliza hela nipate japo mtaji.

Umasikini mbaya sana. Na elimu ya Tanzania inachochea umasikini.

Nipeni ushauri jamani ili mwaka 2018 niwe mtu mpya nijue nini nifanye nami nimiliki japo biashara hata ya kuuza juice, banana power hata shujaa vodka.

Ushauri tafadhali, sihitaji maneno ya kejeli nina frustration zangu.

NAWASILISHA
Elimu yetu hapa bongo tunaendaga kusomea ujinga, mtu una BSc eti unaweza huna kazi, na unawaza kuajiriwa??? Huu ndiyo things mnaendaga kuusomea huko vyuoni, mama yangu maisha la nne alikuwa anakaa vitumbua na uji wa Mchele na alitusomesha watoto wake wote mpaka vyuoni na sasa tunajitegemea wenyewe, shida mnawaza mambo mkubwa mno, na mnakuwa na high expectations ya kupata ajira mnapokuwa vyuoni.
Think small with big ideas.
Pambana na hali yako tu. Na unapopambana nayo chukua usiharibu hali za wengine[emoji1] [emoji1]
 
We ni faller sana, hivi kila mtu anaweza kua kama wewe? Unajua exposure yake? Umri keshasema ni kitu kinamuumiza na mtoto juu bila asset.
Hivi MTU kama huyo tangu apate hiyo degree yake ya education ameshindwa hata kuoganize vijana wa tuition sekondari kwa masomo ya ziada kwa ujira wa kawaida huku akikuwa taratibu.na kuwa na centre yake.?
 
Salaam wanajamvi,

Jamani naomba mnipe ushauri kutoka kwenu hasa kwa wale waliofanikiwa kimaisha.

Kwanza naweza sema hapa Tanzania kusoma sana ndo kuukaribisha umasikini tu.

Kijana mimi wa kitanzania mwenye elimu ya Bachelor degree na Postgraduate Diploma hadi sasa nagonga 30 years sina cha maana ninachomiliki katika maisha yangu.

Sijui kwa sababu nimetumia muda mwingi kusoma, au hii familia niliyozaliwa ya umasikini ndo chanzo hata sijui.

Nilisoma kwa mkopo wa serikali na postgraduate nikafadhiliwa kwa kujua kwamba nikimaliza nitaingia kwenye system kupitia ualimu wa masomo ya arts imekua ndivyo sivyo.

Umri unaenda sina mtaji sina ndugu wa kuniwezesha kwa chochote kazi zimekua ngumu so nategemea kudra za Mwenyezi Mungu labda nitafanikiwa.

Najishughulisha na shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato lakini hakikidhi mahitaji napata hela ya kula, kulipa kodi miezi 2 2 au 1.

Nina mtoto anaishi kwa mama yake, najisikia vibaya kumwona mwanangu anakua lakini hadi sasa baba yake similiki chochote kitakachomsaidia, mama yake ndo anauwezo kwa sasa wa kumjengea mazingira bora coz kipato chake kinatosha kabisa.

Sina ninachomiliki jamani, naombeni ushauri njia bora ya kuishi, namna ya kufanya ili nami niweze kutoka katika dimbwi hili la umaskini, nakiri kwamba nimesoma na kwa sasa sina ndoto tena ya kutaka kuajiriwa nina ndoto ya kujiajiri lakini sijui wapi napata mtaji, labda itokee nipate ajira ya uhakika ya kupata salary bila usumbufu hapo nitajipanga kudunduliza hela nipate japo mtaji.

Umasikini mbaya sana. Na elimu ya Tanzania inachochea umasikini.

Nipeni ushauri jamani ili mwaka 2018 niwe mtu mpya nijue nini nifanye nami nimiliki japo biashara hata ya kuuza juice, banana power hata shujaa vodka.

Ushauri tafadhali, sihitaji maneno ya kejeli nina frustration zangu.

NAWASILISHA
Jifunze ujasiriamali.

1998 nikiwa nimemaliza degree yangu ya kwanza nimewahi fanya kazi za ulinzi na kupiga kiwi viatu pia. Pia niliwahi kuajiriwa kama kibarua kwenye duka moja la hardware kariakoo, kazi yangu ilikuwa kupatia nondo kwenye magari ya wateja.

Acha kubweteka, ingia mtaani ukiwa na wazo la kujuajiri na sio kuajiriwa.
Ondoa iabu, pambana na hali yako.

Acha uvivu, jitume.
Tumia akili zako kutafakari na kutengeneza mustakabari wako.
 
I feel you brother. Umejizungumzia wewe kama umenizungumzia mimi na hii BAEd yangu inanifanya najichukia na kujutia muda niliopoteza chuoni. Naelekea kukata tamaa kabisa .Eee mola nisaidie [emoji24] [emoji24]
Same as me kila nikifuga Kuku Nguruwe si songi sikati tamaa kujiajir kazi sana
 
Around 30s bado ni resonable ege. Ingeleta ukakasi kama ungekuwa umegonga 40s.
Hapo bado unanafasi ya kufanya mambo makubwa sana yatakayo change hali ya maisha yako. Cha msingi acha kupanik jiamini kuwa bado unaweza, then panua wigo wa shughuli hizo ndogo unazozifanya angalia ambayo kidogo ina return nzuri isimamie kikamilifu ili usikose hiyo kodi ya nyumba na pesa ya kula, pia jitahidi usave upate angalau laki 7 uanze kilimo hata kwa ekari moja zitajipanua zenyewe ( japo sijajua uko mji gani) ningekushauri kama utapenda uanze kilimo cha mihogo au ngwara huwa hazina gharama sana kwenye kuhudumia. Kama utakuwa serious ninauhakika apart from natural hazards ndani ya miaka 3 utakua mbali.
 
Anza ufugaji mkuu kuanzia mwakani, tafuta matetea yako matatu na jogoo moja tu mbegu nzuri anza mdogo mdogo tu nadhani unahitaji mtaji wa 50k au pungufu mpk mwezi wa sita hivi utakuwa ushapiga hatua kubwa sana na kuanza kuutimulia mbali vumbi umaskini
 
We siyo graduated ni graditude huwezi kuwa zoba kwa kiasi hicho nikimuona MTU ana degree halafu analalamika ajira natamani nimtemee mate huna Tina kwa taiga hili kabisa .si ajabu umeacha mashamba kijijini nawe IPO mjini unabanana na washua wakati umeacha Mali ,Mimi na degree ya HRM nibahatika kufanya field wilaya flani hadi Leo nafanya shughuri zangu kwenye wilaya hiyo na sina mpango wa kuajiliwa kabisa .
Sio kila mtanzania kazaliwa kijijini na anamiliki mashamba ,but ushauri wako ntaufanyia kazi ntaenda kuomba ukaazi kwenye kijiji chochote cha ujamaa nipewe ardhi nilime
 
Hivi MTU kama huyo tangu apate hiyo degree yake ya education ameshindwa hata kuoganize vijana wa tuition sekondari kwa masomo ya ziada kwa ujira wa kawaida huku akikuwa taratibu.na kuwa na centre yake.?
Mkuu hizi mambo zote unazosema hapa nishafanya but imekua kwa msimu tu si unajua tuition za Tz nyingi za msimu tena ule wa likizo na baada ya kutangaza science ndo inatakiwa basi Sie wa arts ndo tumezidi kutupwa shimoni zaidi
 
Anza ufugaji mkuu kuanzia mwakani, tafuta matetea yako matatu na jogoo moja tu mbegu nzuri anza mdogo mdogo tu nadhani unahitaji mtaji wa 50k au pungufu mpk mwezi wa sita hivi utakuwa ushapiga hatua kubwa sana na kuanza kuutimulia mbali vumbi umaskini
Vijana wengi hawataki ushauri kama huo kwa kulingia mavyeti yao ya vyuoni.
 
Nina mpango mwakani January nitafute kijiji cha kwenda kuanziasha ufugaji
 
Sio kila mtanzania kazaliwa kijijini na anamiliki mashamba ,but ushauri wako ntaufanyia kazi ntaenda kuomba ukaazi kwenye kijiji chochote cha ujamaa nipewe ardhi nilime
Ngoja nikupe siri nyingine ibebe kama ilivyo .katika struggle ya binadamu tuanzia 0 yani bila urithi lazima kutakuwa na kipindi utateseka sanaa lazima ujue hilo utake ustake ,dawa yake ni moja tu nikujiwekea mwenyewe malengo ya kujiyesa kwa miaka kadhaa kwa kuanzia na zero kabisa .mimi kwa sasa hivi nikienda Dar watu huwa wananishangaa sanaa na nikiwaambia sijaajiliwa ndo huwa wananishangaa zaidi sijafanikiwa sana ila alhamudullilah nipo malinyi najishughulisha na kilimo cha mpunga na biashara ya mchele.ila jua lazima one day katika life lako utapitia kwenye tanuli LA moto utake usitake.
 
Vijana wengi hawataki ushauri kama huo kwa kulingia mavyeti yao ya vyuoni.
Ha ha ni kutokujua tu lkn ni namna nzuri ya kuanzia maana haihitaji mtaji mkubwa sana unaweza ukaanza nayo huku unapiga mishe nyingine kuongeza kipato
 
Back
Top Bottom