Ushauri: Umri unaenda sina ninachomiliki

Ushauri: Umri unaenda sina ninachomiliki

hapana mm mwenyewe namiliki one pair of psy.
i feel him ujue ,nayajua maisha ya bongo mkuu acha tu
Duhhh....[emoji15] [emoji15] [emoji15]
Basi umenishinda tabia.....[emoji12] [emoji12] [emoji12]
[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Kati ya watu usiotakiwa tegemea ni
Ndugu (Tumbo Moja au W Mbali)
Familia
Marafiki

Ukiwategemea Hawa utakufa masikini, hata wawe nacho hawawezi kukusaidia zaidi watapenda uwe hivyo ili uwaheshimu
Kwel mkuu na sana sana watakupa pesa ya kula na huku wakiwasaidia marafiki na jamaa kimaisha na kuwaweka kwenye system
 
Umenena vyema.

Anachokipitia jamaa, watu wengi wanapitia ikiwemo mimi.


Alichokisema, nimekipitia.


Nilidharauliwa kwa umasikini wangu japo ni digrii, ila sasa ninaheshimika eti kwa pesa zangu, na sasa wananipiga mizinga, japo sina pesa kihivyo.


Ndugu, marafiki, wengi ni wanafiki tu.
Kwel mkuu,ukitaka kujua tabia za nduhu,jamaa na marafiki uwe hauna kitu
 
Yaan mkuu una akil sna , hakika halio ndo hali halisi haswa

Nina kaka angu yupo uk hapa bongo ana majumba hayana idadi
Ma eka ya mashamba had mengine hayajui

Ila kumseidia mtu shida yaan kukupa kamtaj hawez labda sh 10000 ili sku yapili umuombe tena aone huwezi ishi bila yeye nikaona. Bora nijiongeze saiv sina habar nae kabisa japo km ni kaka baba mmoja ma mmoja ila sina mawasiliano nae tena nafanya yangu

Jaman chonde chonde msitegemee vya ndugu mtakufa masikini
Ndiyo la muhimu na wanaofaidi ni marafiki na jamaa
 
Bro kwanza nikupe pole lakini pia usikufuru Mungu kwa kukata tamaa, elimu uliyonayo inatosha kuifanyia kazi ila jifikirishe haswaaaa.

Pili hujatwambia uko mkoa gani maana kila mkoa na fulsa zake.

Mwisho umesema mzazi mwenzio yupo vizuri kiasi kiuchumi sasa unaonaje ukae nae na akupe mtaji na ufanyie kitu au biashara ambayo kwayo utabadili mawazo yako ya kulaani elimu yako, na unapolaani elimu yako inamaana unawalaani na waliokusomesha kwa kuwa kama wasingekusomesha huenda mda uliotumia darasa ungefanyia kazi za kujiingizia kipato.

Ndugu ngoja nikwambie kitu kimoja Mungu wa ajabu sana tena sana, kwa vile huenda usingeenda shule leo ungekuwa marehemu labda au ungekuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya au ungepata utajiri ambao kwa umri wako huenda ungewadharau hata Mungu wako wa pili ambae ni mzazi.


Ushauri bado mda unao wa kuamua hatima ya maisha yako
 
Salaam wanajamvi,

Jamani naomba mnipe ushauri kutoka kwenu hasa kwa wale waliofanikiwa kimaisha.

Kwanza naweza sema hapa Tanzania kusoma sana ndo kuukaribisha umasikini tu.

Kijana mimi wa kitanzania mwenye elimu ya Bachelor degree na Postgraduate Diploma hadi sasa nagonga 30 years sina cha maana ninachomiliki katika maisha yangu.

Sijui kwa sababu nimetumia muda mwingi kusoma, au hii familia niliyozaliwa ya umasikini ndo chanzo hata sijui.

Nilisoma kwa mkopo wa serikali na postgraduate nikafadhiliwa kwa kujua kwamba nikimaliza nitaingia kwenye system kupitia ualimu wa masomo ya arts imekua ndivyo sivyo.

Umri unaenda sina mtaji sina ndugu wa kuniwezesha kwa chochote kazi zimekua ngumu so nategemea kudra za Mwenyezi Mungu labda nitafanikiwa.

Najishughulisha na shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato lakini hakikidhi mahitaji napata hela ya kula, kulipa kodi miezi 2 2 au 1.

Nina mtoto anaishi kwa mama yake, najisikia vibaya kumwona mwanangu anakua lakini hadi sasa baba yake similiki chochote kitakachomsaidia, mama yake ndo anauwezo kwa sasa wa kumjengea mazingira bora coz kipato chake kinatosha kabisa.

Sina ninachomiliki jamani, naombeni ushauri njia bora ya kuishi, namna ya kufanya ili nami niweze kutoka katika dimbwi hili la umaskini, nakiri kwamba nimesoma na kwa sasa sina ndoto tena ya kutaka kuajiriwa nina ndoto ya kujiajiri lakini sijui wapi napata mtaji, labda itokee nipate ajira ya uhakika ya kupata salary bila usumbufu hapo nitajipanga kudunduliza hela nipate japo mtaji.

Umasikini mbaya sana. Na elimu ya Tanzania inachochea umasikini.

Nipeni ushauri jamani ili mwaka 2018 niwe mtu mpya nijue nini nifanye nami nimiliki japo biashara hata ya kuuza juice, banana power hata shujaa vodka.

Ushauri tafadhali, sihitaji maneno ya kejeli nina frustration zangu.

NAWASILISHA

Acha kukata tamaa, 30 bado mdogo kwa mtu aliyesoma mfumo wa Elimu ya Tanzania na kutokea familia yenye kipato cha kawaida. Kikubwa fanya juhudi upate kazi au kama utapata mtaji ufanye biashara. baada ya hapo ndio uanze kujiongeza..
Usiibe tafuta kipato halali hujachelewa, usije kuharibu maisha yako kwa tamaa au kuiga wengine.
 
Ngoja nikupe siri nyingine ibebe kama ilivyo .katika struggle ya binadamu tuanzia 0 yani bila urithi lazima kutakuwa na kipindi utateseka sanaa lazima ujue hilo utake ustake ,dawa yake ni moja tu nikujiwekea mwenyewe malengo ya kujiyesa kwa miaka kadhaa kwa kuanzia na zero kabisa .mimi kwa sasa hivi nikienda Dar watu huwa wananishangaa sanaa na nikiwaambia sijaajiliwa ndo huwa wananishangaa zaidi sijafanikiwa sana ila alhamudullilah nipo malinyi najishughulisha na kilimo cha mpunga na biashara ya mchele.ila jua lazima one day katika life lako utapitia kwenye tanuli LA moto utake usitake.
Mwakashina mtua.
 
Tafta pikipiki used boxer Dar, utapata kwa bei poa then weka balabalani

Mkuu pikipiki used???? Seriously!!

Hakuna ishu ngumu kama hiyo, usizione humo barabarani ukahisi ni kitonga.. changamoto zake ni kubwa mno. Ningekuona wamaana ungemshauri achukue mpya.

Kuendesha biashara ya bodaboda inatakiwa uwe Na backup savings la sivyo kwa wiki kadhaa ipo juu ya stand ndani
 
We siyo graduated ni graditude huwezi kuwa zoba kwa kiasi hicho nikimuona MTU ana degree halafu analalamika ajira natamani nimtemee mate huna Tina kwa taiga hili kabisa .si ajabu umeacha mashamba kijijini nawe IPO mjini unabanana na washua wakati umeacha Mali ,Mimi na degree ya HRM nibahatika kufanya field wilaya flani hadi Leo nafanya shughuri zangu kwenye wilaya hiyo na sina mpango wa kuajiliwa kabisa .

Shauri sasa acha maneno ya majisifu na dharau, sio kila mtu ana uwezo wakuchangamkia fursa, wengine hadi uwabusti
 
Back
Top Bottom