Ushauri unahitajika kabla jahazi halijazama

spongy

Member
Joined
Feb 25, 2019
Posts
61
Reaction score
59
Habari za jioni wakuu, poleni na majukumu ya kila siku.

Jamani sikia, omba yasikukute. Baada ya kupigika na kupoteza mtaji wangu wote kwenye uchimbaji nilikuwa najishughulisha na uchimbaji madini chunya ambapo nilikuwa na mil. 15, nikanunua karasha nikuze mlima.

Baada ya uchenjuaji nimekosa dhahabu mara tatu na sehemu tatu tofauti wenyewe wanaita kuporora nimeona niliuze tu karasha nipate mtaji angalau niingie kwenye biashara.

Nahitaji msaada, ushauri, biashara ambayo ntakuwa natembea na mtaji mana hela niliyo kuwa nayo ni mil. 3.

Nahitaji niikuze haraka wakuu, nahitaji mawazo yenu sasa nataka nihamishie nguvu kwenye biashara.

Msaada jamani.
 
Kabla ya kurukia biashara nyingine,kwanza angalia ulikosea wapi? Unaweza kwenda kwenye biashara nyingine kisha ukarudia kosa lile lile,

Tatizo nililoliona mimi hapo ni kua,

"Uliweka mayai yako yote kwenye tenga moja"

Usiweke mtaji wako wote kwenye biashara ambayo huna uzoefu nayo,

All the best.
 
Pole sana .
Uko chunya si ndivyo ? Panda gari nenda mpka Mbalizi , ukifika Mbalizi omba watu wakuoneshe ilipo stendi ya Umalila huko panda gari za kwenda Umalila zinazoenda Isuto , ukifika Isuto hapo sasa tafuta fremu haitazidi 20 _ 25 baada ya hapo rudi mjini nenda Mwanjelwa kanunue vyombo maplastic kwa sahani na wenzie kaweke kwenye fremu , kauze mara mbili ya bei uliyonunulia ukifika mwezi wa tisa tayari una hela mara tatu ya uliyowekeza , then hapo msimi wa hela kwa huko unakuwa unaelekea mwisho hivyo badili biashara utakuja tena nikuambie ufanye biashara ipi ili kuendelea kwenye trending huko umalila

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Hivi kumbe huwaga ni rahisi hivyo? Mbona nakufa maskini kizembe sasa?
 
Unataka ukue kwa haraka itaisha kaaa tulia
 
Biashara ya kubeti ina faida sana mkuu tafuta odds 2 kwa siku manake apo kila siku ukibetia mil 3 iyo unakua unapata faida mil 3
 
Biashara ya kubeti ina faida sana mkuu tafuta odds 2 kwa siku manake apo kila siku ukibetia mil 3 iyo unakua unapata faida mil 3

Dah kijana wa hovyo [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…