Ushauri unahitajika: Kati ya Cyber Security na Laboratory Science in Biotechnology

hermanthegreat

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2021
Posts
1,274
Reaction score
3,282
Habari wanajf.

Kuna rafiki yangu kachaguliwa kozi mbili vyuo vitatu, anaomba ushauri vipi a confirm.

1. Cyber security (Arusha)
2. Laboratory science in biotechnology (SUA na MUST)

Msaada tafadhari , ipi Ina soko Sana ama Ina unafuu kwenye upatikanaji wa ajira
 
Cyber security kama ana akili ya kujiongeza..
 
Inategemea lakini Lab Science ni kitu kizur sana...
Kama ametoka familia duni, aende SUA akitoka hapo kaz anapata kirahisi sana...
1. TBS
2. TMDA
3. HOSPITALS
4.INDUSTRIES
5. PRIVATE LABS.
6. ENTREPRENEURSHIP

Hiyo nyingine sijui, wengi niliosoma nao Advance wanaishi miji mikubwa ndani na nje ya nchi kwa hiyo course..
 
Eti kirahisi ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Asisome cyber. Hiyo kozi ni kama mvua za rasharasha tu, kama anataka ajira asome Biotech ni kozi mpya kwa tz na soko la ajira lipo. Lakini asisome MUST-chuo cha teknolojia asisome SUA, hao sua hata kilimo na ufugaji vilishawashinda
 
Mkuu habari yako! Nimemaliza BSC. Biotechnology and laboratory science sua mwaka huu, unaweza nisaidia wazo au connection yeyote kutoka kwa jamaa zako kama hautojali ๐Ÿ™๐Ÿพ
 
Mkuu habari yako! Nimemaliza BSC. Biotechnology and laboratory science sua mwaka huu, unaweza nisaidia wazo au connection yeyote kutoka kwa jamaa zako kama hautojali ๐Ÿ™๐Ÿพ
Kama Upo Dar,
Na unapenda kaz ya kuuza Dawa, kwa kuanzia
Andika CV yako vizur .. peleka. Sehem hizi..
Salama, Heko, Astra, Bahari, Abacus, Core, wambie untafuta kazi ya Sales.... Upo tayar kwa training na kuanza kazi...

Kama hupendi sales,
Nenda physically TBS, TMDA,Viwanda vyote vya Maji na Chakula (GSM, Hills, Afya, Bakheressa etc) wambie unataka kujitolea...

Ukishindwa kabisa ni PM..

Mungu akutangulie.
 
Nipo dar kwa sasa, nimelipenda hilo wazo lako la sales
Naku PM mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ