Ushauri unahitajika kwa dada yetu

Ushauri unahitajika kwa dada yetu

Sijui kama utanielewa, ila nihivi... ni rahisi mwanaume kumuoa Mwanamke aliyemkuta SINGO yaan singo mazaa , KULIKO kuoa Mwanamke aliyemkuta ndoani,Kisha huyo mwanamke akavunja Ndoa yake ,ili aolewe na Mwanaume Mpya .


Vunja, baada ya miezi mitatu ,utaleta Mrejesho
Thread closed
 
Ukiachika utapata stress mara mbili ya sasa 😂 maana hio furaha unayohisi utaipata kwa mchaga hutakaa uione zaidi ya majuto. Anasubiria uachike ili akuburuze vizuri na hatakuoa hataa...

Ataenda oa mtu wake mpya ili unyooke.
 
Mi sijaolewa ila ushauri wachagga, wapare Hawa watu ni wachukua nyota za watu.
Ulipoolewa uliepushiwa kutolewa sadaka.

Wale wanapenda kuuana .
Yaani maisha Yao Huwa ni ya misimh .
Kuhusu mumeo ni mchaga kamloga ili uachane naye hawawatu walichonifanyia ndio usingle huu ninao hadi sasa kwanza ukienda unazimwa na kitu unakuwa zuzu najiona uko powa ila nyota imeshaenda kwake.
Wewe hujitambui.
 
Nyatyo unaonekana una nyota kali ya usaliti na kutokuwa mvumilivu.
 
Kwa sasa nipo njia panda sielewi. Nawaza je, anania kweli ya kunioa au anataka alipize kisasi? Kwasabu ni haraka sana anataka hili jambo. Na je, ananipenda kweli au anatumia ushirikina maana anasema mimi ndiyo nguvu yake ya mafanikio. Naogopa na sielewi nifanye maamuzi gani, nipo njia panda, au nibaki tu kwenye ndoa nivumilie labda atakuja kubadilika?

Nimelileta kwenu naomba ushauri, nipo njia panda nashindwa kufanya maamuzi, ninachotaka niwe na furaha.
  • Je hii simulizi mzazi wako (mama yako, baba yako au wote mama na baba ) wanafahmu?
  • Iwapo kama hawafahamu basi ni wakati sahihi sasa kuwaeleza/ kuwasimulia kwa kina.
  • Na upokee kama ulivyo huo ushauri utakao pewa na wazazi.
  • Hakuna ushauri bora zaidi utakao weza kuupata, kushinda ule ushauri utokao kwa wazazi wako wapedwa.
Kila lakheri
 
Mi sijaolewa ila ushauri wachagga, wapare Hawa watu ni wachukua nyota za watu.
Ulipoolewa uliepushiwa kutolewa sadaka.

Wale wanapenda kuuana .
Yaani maisha Yao Huwa ni ya misimh .
Kuhusu mumeo ni mchaga kamloga ili uachane naye hawawatu walichonifanyia ndio usingle huu ninao hadi sasa kwanza ukienda unazimwa na kitu unakuwa zuzu najiona uko powa ila nyota imeshaenda kwake.
Tumia akili basi. Wewe ulichukuliwa nyota au uliuliwa ukafufuka .?
 
Mi sijaolewa ila ushauri wachagga, wapare Hawa watu ni wachukua nyota za watu.
Ulipoolewa uliepushiwa kutolewa sadaka.

Wale wanapenda kuuana .
Yaani maisha Yao Huwa ni ya misimh .
Kuhusu mumeo ni mchaga kamloga ili uachane naye hawawatu walichonifanyia ndio usingle huu ninao hadi sasa kwanza ukienda unazimwa na kitu unakuwa zuzu najiona uko powa ila nyota imeshaenda kwake.
Pole sana dadangu,Ila najuwa Huwa nakupenda kimya kimya.
 
Admin mimi nimeolewa na nina mtoto mmoja wa kiume. Kabla sijaolewa nilikua na mahusiano na kijana wa Kichaga, kiukwel tulipendana na yule kijana alinijali, aliniheshimu, kiufupi tuliishi vizuri mikwaruzano ilikuwa michache sana.

Kipindi hicho nilikuwa sina ajira, bali nilikua nafanya kazi ya kujitolea kwenye taasisi fulani, ila huyo kijana yeye ni mwajiriwa wa serikalini. Tulifanikiwa kufungua duka, kiukweli duka lilikua linaenda vizuri.niliwaza huyu ndie atakuja kua mume wangu lkn haikua hivyo.

Tulikuwa na ukaribu hatua hadi nyumbani kwao nilifahamika, na yeye alifamika kwa baadhi ya ndugu zangu ila siyo wazazi na tangu nimekua naye mambo yalikua vizuri, kiufupi nilienjoy mapenzi yake kwa kipindi chote hadi pale nilipoanza kuwasiliana na rafiki yangu mwingine ambaye kwa sasa ni mume wangu.

Huyu kijana (name hide) alikua rafiki tu, tuliambiana mambo mengi na kushauriana, sikuwahi kukutana naye kimwili, alikua rafiki tu. Ghafla huyu kijana akaniambia kuwa anataka kunioa, kiukwel nilidhani masihara lakini kadri siku zilivyozid niliona inakua 'serious'. Niliongea na mpenzi wangu Mchaga nikamwambia habari za kuoana akaniambia nisubiri nimalize shule sababu nilikuwa nasoma chuo halafu ndiyo tutanza hizo taratibu.

Lakini pia alikua ananisisitiza nimzalie mtoto kwanza, kiukweli tulipishana maana anataka nimzalie mtoto kabla ya ndoa, nikimwambia swala la ndoa anasema mpaka nimalize chuo upande wangu niliona haijakaa poa.

Sasa wazo la rafiki yangu la kutaka kunioa likaanza kuniingia kichwani. Sijui ni nini kilipata nikaanza kutamani ndoa hadi inafikia hatua tunagombana na Mchaga wangu swala la ndoa.

Hiyo siku niliongea na rafiki aliyetaka kunioa akaniambia amenipenda na ananijua muda mrefu hivyo anaona ninamfaa kuwa mke wake. Akaniambia tupime afya kiukwel nilifanya hivyo bahati nzuri afya zetu zilikua vizuri, na hakuchelewa ikabidi apeleke posa nyumbani, wazazi walipokea na kufanya mandalizi ya kujibu posa.

Kiukwel nilikua na wakati mgumu maana nilimpenda sana Mchaga. Siku moja ilibidi nimwambie Mchaga kuwa nyumbani kuna mtu ameleta posa na bado haijajibiwa, yule Mchaga alikasirika akaniambia kuwa nilikua na mahusiano mengne wakati nipo na yeye jambo ambalo siyo kweli.

Kwahiyo alijibu kwa hasira akaniambia kama unataka kuolewa olewa na kama utanisubiri sawa. Binafsi lile jibu sikulipenda na hapo ndiyo nilipowaza kua Mchaga alikuwa ananichezea tu, hana haja na mimi. Ilibidi niwaambie wazazi wajibu kuwa nipo tayari kuolewa, wazazi walifanya hivyo na ikawa inasubiriwa tarehe ya mahari.

Kipindi yote yanafanyika bado nipo na Mchaga hatujaachana na tangu anijibu vile hatukuwai tena kuzungumzia hilo swala, hivyo nilikuwa nafanya mambo yangu kimya kimya bila yeye kujua. Tarehe ya mahari ilipangwa tukaenda, ni nje ya mji hivyo nilimdanganya Mchaga kuwa naenda kusalimia nyumbani kumbe naenda kutolewa mahari.

Niliporudi tu nilionana na Mchaga, kiukwel nilimuona hayupo sawa kabisa. Kwanza alikuwa kapungua, nikamuliza shida nini akasema hakuna shida ila anahisi homa. Pia nilikua natafuta namna ili tuachane niendelee na mambo ya ndoa.

Siku iliyofuata alikuwa kazini akanipigia simu sikupokea siku nzima, iliniuma lakini nilikua natafuta namna achukie tuachane. Kweli siku iliyofuata tena akapiga sikupokea, akatuma ujumbe kuwa nipokee ana jambo la muhimu hapo nikapokea simu yake.

Kiukwel aliongea maneno makali sana, akasema anajua kila kinachoendelea na ana namba hadi ya huyo bw. harusi mtarajiwa na akanitumia baadhi ya sms tulizokuwa tukichat na bw. harusi mtarajiwa na akaniambia niendelee na mambo yangu kamwe sitokuja kufurahia ndoa. Kiufupi aliongea maneno mabaya na vitisho juu, alipaniki sana na ndiyo siku tuliyovunja uhusiano wetu.

Niliolewa na Mungu akatubariki mtoto. Mwanzoni nilifurahia sana ndoa lakini hivi sasa naona majuto. Mwanaume amebadilika sana, kwanza anataka aoe mke wa pili, cha pili nimefatilia nyendo zake ni mtu mwenye mambo mengi hasa ya wanawake, ni muongo na tangu tumefunga ndoa hakuna mafanikio yoyote tuliyopata zaidi ni kupoteza na kwa upande wangu mambo yamekua hovyo sana.

Kuna muda najitahidi kuvumilia lakini roho inaniuma sana na inanipelekea namkumbuka Mchaga. Siku moja nilijaribu kutuma ujumbe namba ya Mchaga, kiukwel ilikua hewani na alijibu na kunipigia. Tuliongea sana na nilimuomba msamaha nikamwambia nikwel nilimkosea lakini asiwe na kinyongo na mimi.

Nilimbembeleza sana akaniambia ameshanisamehe lakini bado hajanisahau, tukawa tunawasiliana tu kama marafiki. Lakini kadri vituko vya mume vinavyozidi namtafuta Mchaga, kiukwel ananifariji ikafika mahala nilimweleza kuwa mambo siyo mazuri.

Alihuzunika na akaniambia anaomba turudiane hata kama nimeshazaa. Pia akaniambia mimi nina nguvu ambayo inampa mafanikio kwahiyo akiwa na mimi mambo yake yanaenda vizuri. Siku moja ilibidi nikutane naye na tulikaa sehemu tukaongea kwa kirefu sana na hatukufanya chochote japo alinilazimisha sana.

Kiukweli pamoja na yote yanayoendelea sijawahi kumsaliti mume wangu, Sasa hivi karibuni Mchaga alifiwa na bibi yake ambaye ninamfahamu, ilinibidi niende msibani. Nilifanikiwa kuonana na ndugu zake, kiukweli bado wananipenda.

Pia na lile duka tulilofungua bado lipo, baada ya msiba Mchaga alinipigia simu akaniambia anataka anioe. Hivyo akaniambia kwakua mume wangu anataka kuongeza mke wa pili, nitumie hiyo kama fursa ya kuvunja ndoa ili anioe yeye na akarudia tena kusema akiwa na mimi mambo yake yanaenda vizuri. Japo hapa kati tulivyopotezana alishakuwa na mahusiano lakini hayajadumu.

Kwa sasa nipo njia panda sielewi. Nawaza je, anania kweli ya kunioa au anataka alipize kisasi? Kwasabu ni haraka sana anataka hili jambo. Na je, ananipenda kweli au anatumia ushirikina maana anasema mimi ndiyo nguvu yake ya mafanikio. Naogopa na sielewi nifanye maamuzi gani, nipo njia panda, au nibaki tu kwenye ndoa nivumilie labda atakuja kubadilika?

Nimelileta kwenu naomba ushauri, nipo njia panda nashindwa kufanya maamuzi, ninachotaka niwe na furaha.
Kweli kazi unayo upo kwenye wakati mgumu. Nimekos cha kukushauri...
 
Nashauri mchaga asikuoe kwa sababu watu huwa hamjifunz kutokana na makosa
 
Hii ni situation ya mabinti wengi mna haraka sana kama vile mnakufa kesho

Chukua kikombe kivunje then kiunganishe kama kitakuwa kama mwanzo

Unataka kuolewa na mtu uliyemuumiza moyo wake tena akafikia kukonda kwa ajili yaki

Dare it
🤣🤣🤣Huyu hajielewi,yani alimpenda sana mchaga,alafu akaja jamaa anataka kumuoa haraka haraka akakubali,lakini moyo upo kwa mchaga

Yupo ndoani na ameshazalishwa tayari mume na wake,saiv anajuta anamtaka tena mchaga mpenzi wake wa mwanzo amuoe tena?
Hana akili,kama alimpenda mchaga wake kwa nini alikimbilia kuolewa mwanzo?hawanaga maamuzi hawa mabinti.

Yeye apambane na furushi lake tu😀😀
 
we endelea kukitembeza tafuta na muha mnyaturu na mkinga wote uzae nao
 
Leo soma ushauri fanya unachopenda
Bye
 
Binti yangu unafanya uzinifu kwa kiwashirikisha ndugu zako mpaka wachungaji.

Umezini na kijana wa kichaga (kama ndiye wa Kwanza kwako) basi huyo ndiye mumeo sahihi, huyu mwingine ulienda kutokana na tamaa na uroho wa NDOA!.

Ulimuacha mumeo halali anayetakiwa na Mungu
Proverbs 5:18 ukaenda kwa mume wa karatasi na wachungaji, mume au mke ujanani ni yule ambaye mlianza naye show!.
 
Achana na mchaga wabahili hao njoo hapa kwa msukuma maziwa yapo ya kutosha.
Maziwa tu? je hela? nyie wauaji tu hamna lolote hamjiaminigi? mnamlaa mtu Kwa wasiwasi ni kula Kwa amani chakula ni chako jinafasi kikiliwa ni bahati mbaya sana
 
Ukute mchaga bado ana hasira na wewe anataka kulipiza kisasi!!!
Mara uachane na chapombe wako mchaga nae aingie mitini!!!?

Fanya kile kitacho kupa amani my dear.... Ushauri wa wengi umeuona amua kusuka au kunyoa
 
Huna uvumilivu kabisa linda ndoa yako utaishia pabaya na huyo mchaga wako hapo amerudi kulipiza kama hujuwi
 
Back
Top Bottom