Kwetunikwetu
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 1,535
- 412
Wakuu naomba mnichangie mawazo ya kumpatia ushauri muafaka rafiki yangu. Ni hivi, kuna jamaa ni rafiki yangu wa karibu sana (almost ndugu). Tumesaidiana kwa mambo mengi na kwa muda mrefu sana. Kwa muda wa miaka kama mitatu amekuwa na urafiki na msichana fulani, hatimaye kufikia uamuzi wa kujiweka tayari ili kufunga ndoa. Baada ya kujitambulisha kwenye pande zote mbili za familia, matatizo ndio yameanza kama ifuatavyo;
1. Rafiki yangu na huyo mchumba wake ni wakristo ila madhehebu tofauti; wao wameamua kila mtu abaki na thehebu lake ila ndoa ifungwe kwenye dhehebu la mwanamume. Lakini baba wa huyo binti amekataa katakata anataka ndoa ifungwe kwenye dhehebu la binti yake.
2. Pili, baba wa huyo binti amemtaka rafiki yangu asaini kiapo kuwa watoto wao watabatizwa na kulelewa kiroho kwenye dhehebu la binti yake (ie dhehebu la huyo baba mkwe).
3. Jamaa yangu alimpomweleza huyo binti kuwa masharti hayo ni magumu sana kwake, na hivyo kumtaka binti atoe msimamo wake, binti alimwambia kama itashindikana basi waachane.
4. Kwa sasa binti huyo ni mjamzito wa kama miezi mitano hivi, habari hiyo bado haijamfikia huyo baba mkwe.
Sasa basi, nilipomuuliza rafiki yangu anieleze msimamo wake....alinijibu kuwa mpaka sasa hajui afanye nini. Nilimuomba anipe wiki moja nijaribu kutafakari kwa vile nisingeweza kukurupuka ukizingatia uzito wa suala lenyewe.
Wadau naomba mistari ili niweze kutoa ushauri muafaka