Ushauri: Usipende kuweka namba yako ya simu mitandaoni bila sababu. Ni rahisi kumdukua mtu ukiijua namba yake ya simu

Samia atosha tukutane2030

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
17,728
Reaction score
49,762
Napenda kuwapa ushauri wana JF wenzangu.

Mjitahidi kulinda privacy zenu huko Facebook, Instagram, Twitter n.k. Kuna watu wakiipata tu namba yako wanakudukua kiulaini.

Nimewahi kufanya research na kugundua ni rahisi sana kumdukua mtu kwenye mtandao wa kijamii ikiwa tu utaijua namba ya simu aliyoitumia au aliyoiweka wakati anafungua.
 
Watu wepesi sana kutoa namba za simu hadi nashangaa, huko facebook ndo usiseme ukianza tu 'nina mafunzo ya kuku wa kienyeji mwenye kuhitaji aweke namba yake' watu huuuuu, namba kibao!
 
Kudukua kivipi mkuu unamaanisha, Sehemu unayoishi au vipivipi..?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…