Ushauri: Utengenezaji na soko la chaki

Ushauri: Utengenezaji na soko la chaki

Nyamburi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2011
Posts
306
Reaction score
36
Wadau habari!nakuja tena jukwaani kuomba kupata ushauri juu ya biashara ya chaki(chalk),nilibahatika kupata kimasheni cha kutengenezea chaki kama zawadi toka kwa wadau fulani wa nchi ya magharibi!sasa bado sijajua hasa demand (mahitaji) ya soko la bidhaha hii liko vipi na ni wapi naweza kuanzia kimasoko angalau nami nianzi kujikwamua kiuchumi kutokana na uzalishaji wa chaki!nimeleta suala ili kwenu wadau kwa kua nina amini jamiiforums hakuna jambo ambalo utaliwakilisha na ukashindwa kutoka na mawazo chanya!Asanteni sana!
 
Mkuu nakushauri ungezunguka kwenye mashule na taasisi zenye uhitaji wa chalks ujitangaze na kujaribu kuwa win katika bei,otherwise inaonekana ni biashara ngumu kidogo,bora nguvu yako ungewekeza kwenye kilimo/chakula,maana hiyo ndio bidhaha yenye kuhitajika kila siku katika maisha yetu!
 
Quality ya chaki zako zikoje na production cost ikoje (utaweza kuuza kwa ushindani, kama soko au chini ya soko) ?

Fanya SWOT analysis na kwenye Strength zako angalia kama quality yako na bei yako itakuwa nzuri kuliko kilichopo sasa, ikiwa utafanikiwa hayo sioni kwanini usiuze
 
Ni biashara nzuri kama uko mikoani au unawatu mashuleni, kwa sasa hivi Dar wachina wameharibu soko wanauza bei cheap wkati wewe kwa malighafi za hapa Tanzania ukishindana nao hiyo bei ni hasara. Kwa kuzalishia mikoani unaweza kupata zaidi.
 
Back
Top Bottom