Ushauri wa Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula kwa Rais kuhusu wanaharakati kutoka nje

Mimi niliona statement ya Kenya Law Society ikilaani kukamatwa kwa Kizza Besigye Kenya, na pia baadhi ya wanaharakati wa haki za binadamu na wanasheria walihudhuria kesi yake.
Ingependeza kama ungetuwekea hiyo statement mkuu, na pia tuone aina ya maneno waliyokuwa wanaongea kama yanafanana na haya waliyoongea kabla, na baada ya kufika kwetu.
 
Kuna kanuni ya fizikia nilijifunza nikiwa Form I au II inasema: "Action and reaction are equal and opposite."
Kwa kuboresha tu hiyo Law inapatikama Form 1 na inapatikana pia Physics form V, Module ya Mechanics, section ya Motion.

"To every action, there is equal and opposite reaction"

Newton's third law of motion.
 
USHAURI WA ASKOFU KWA RAIS SAMIA JUU YA WANAHARAKATI WATOKAO NCHI ZA NJE!

Tarehe 19 Mei 2025 ni siku iliyokuwa imebana sana kwangu. Sikuweza kufanikiwa kufuatilia hotuba yeyote iliyotolewa na Mheshimiwa Rais Samia Saluhu Hassan. Hata hivyo, usiku niliona habari picha kadhaa zikiwa na maneno ambayo yanaelezwa kuwa yalitolewa na Rais Samia.

Katika habari picha mojawapo, Rais alinukuliwa akisema: "Tusitoe nafasi kwa wanaharakati wa nje kuingilia masuala ya Tanzania"! Kama kauli hiyo ni ya Rais Samia Saluhu Hassan, nchi yetu itakuwa imefikia hatua mbaya sana kwani hata Rais amejua kuwa tumefikia mahali ambapo tunahitaji watu au wanaharakati wa nje kutetea wananchi wa Tanzania.

Huko nyuma kuanzia mwaka 1961 hadi 1990, wanaharakati, wanasiasa na viongozi kutoka Tanganyika na baadaye Tanzania ndio ambao walikuwa wakiingilia masuala ya nchi jirani au nchi za nje. Wanaharakati, wanasiasa, watetezi na viongozi hao waliokuwa wakiingilia mambo ya nchi nyingine waliongozwa na Rais Julius Nyerere mwenyewe.

Wakati Rais wa Malawi, Dkt. Hastings Kamuzu Banda anatesa na hata kuua watu wake, nchi ya Tanzania sio tu kuwa iliingilia masuala ya nchi ya Malawi, bali pia iliwapa hifadhi watu na wakimbizi kutoka Malawi akiwemo mwandishi nguli aliyekuwa akiandikia gazeti la Daily News.

Wakati Idi Amini Dada alipoipindua serikali ya Uganda na kumuondosha madarakani Rais Milton Obote, Rais Nyerere aliingilia masuala ya Uganda, akaenda mbali zaidi akawa hifadhi Milton Obote, Yoweri Kaguta Museveni, nk.

Wakati Afrika Kusini ilipokuwa chini ya mfumo wa utawala wa ubaguzi wa rangi, Tanzania ya Rais Julius Nyerere iliingilia masuala ya Afrika Kusini kwa kuhamasisha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya nchi hiyo ikatoa ardhi kwa wapiganaji wa Afrika Kusini.

Nchi nyingine ambazo ziliingiliwa wanasiasa, wanaharakati na wapiganaji wa Tanganyika na baadaye Tanzania ni pamoja na Rhodesia (sasa Zimbabwe), Msumbiji, Angola, Namibia, Algeria, nk.

Lakini pia hakuna asiyejua ya kuwa wakati wa utawala wa Mobutu Seseko wa Zaire (sasa DR Congo), Tanzania iliingilia masuala ya Zaire kwa kuwahifadhi Desire Kabila (Baba Ntwale) na mwanaye hadi wakafanikisha kumuondoa madarakani Rais Mobutu. Mifano haiishi kwani sio watu wengi wanajua kuwa wanajeshi wetu walikwenda katika Visiwa vya Commoro. Lakini kama walikwenda kutembea au walikwenda kula pikiniki, ajuaye ni Rais Kikwete na Jenerali wake Davis Mwamunyange.

Kama asilimia kubwa ya Watanzania wanajua ya kuwa upinzani unanyanyaswa nchini huku viongozi wao kama Ali Kibao wameuawa na wengine kama Soka, Kipanya, Chaula, Mlay, Mbise na Mdude wametekwa na hawajulikani waliko, hautarajiwi kuwa wanaharakati wa nchi za jirani wasijue kuwa kuna ufinyaji wa haki za msingi nchi ikiwemo haki ya kuishi.

Lissu alipigwa risasi 16 mchana kweupe akiwa katika majengo ya serikali yanayolindwa pia na serikali lakini hadi sasa hakuna mtu ye yote aliyekamatwa na wala hakuna uchunguzi wo wote uliofanywa hadi sasa. Lissu amekamatwa na kupewa makosa mazito kabisa duniani ya uhaini ambayo hatima yake ni kunyongwa hadi kufa. Katika mazingira kama hayo, haitarajii ya kuwa wanaharakati kutoka nje za nje watakaa kimya wasiingilie mambo ya Tanzania. Kama Tanzania ilitia sahihi mikataba ya kimataifa juu ya haki za binadamu, ni lazima itaingiliwa na wanaharakati kutoka nchi za nje.

Kama wao Rais Samia, CCM pamoja na serikali yake wanataka Tanzania isiingiliwe na watu au wanaharakati kutoka nchi za nje, basi wafanye mambo mawili. Mosi, waandike katiba mpya au wabadili katiba iliyopo ili wanyofoe kifungu kile kinacholinda haki za binadamu. Pili, wafanye haraka sana juhudi kuiondosha Tanzania katika mikataba yote ya kimataifa. Baada ya kufanya hivyo, waiondoe Tanzania kutoka katika Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Madola, Jumuiya ya Afrika Mashariki, COMESA, SADC, nk.

Wakimaliza kufanya yote hayo, ndipo Tanzania ivunje uhusiano wa Kibalozi katika nchi zote duniani na iwaite Mabalozi wake wote walioko katika nchi hizo, mwisho iwafukuze Mabalozi wote wa nchi za kigeni walioko Tanzania. Hapo ndipo itoe kauli ya kutokuingiliwa na wanasiasa na wanaharakati kutoka nchi za nje kwani sasa Tanzania itakuwa tayari ni Kisiwa cha Mbudya!
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam, 20 Mei 2025; saa 3:45 asubuhi.
Msamehe Chura Kiziwi - Mpofu huyu Baba Askofu. Huyo Chura vile vile amesahau Nyerere alimuunga Ojukwu wa Biafra kwenye Federation ya Nigeria, mwache kiziwi apumzike
 
Nina mashaka makubwa sana na kauli za Rais Samia, huenda hapitii ripoti anayo pewa kabla ya kutoka hadharani au hulazimishwa kusoma neno kwa neno na ana shindwa kukataa maana anajua yuko madarakani kwa njia gani.
Imefika mahali nashindwa hata kumsikiliza akiongea maana tayari huwa najua hatma ya atakacho ongea ni ujinga. Sitegemei Rais wa nchi awe ana toa speech za aina hizi. Yaani ni aibu.
 
Hiki kijamaa kichokauka mwili nilikidharau sana kipindi kile kinatweet habari za uzushi dhidi ya Mbowe kwenye uchaguzi!! Kishenzi sana hiki kidubwana
huyu mbuzi naye angalia anayojambia humu jukwaani aende zake huko HAKUNA KUWARUHUSU HAO VIBARAKA WAJE KUTUHARIBIA NCHI YETU YANAWAGHUSU NINI HAYA YA KWETU WAMEBANWA KWAO WANAKIMBILIA KWETU HAKUNA KUWAPA NAFASI MAMA SHIKILIA HAPOHAPO
Hamuoni aibu kujiweka hadharani kwamba hamuna hoja yeyite ile ya maana?

How comes you are so shameless, are you real human beings or brainless Ni anderthals?!
 
Ingependeza kama ungetuwekea hiyo statement mkuu, na pia tuone aina ya maneno waliyokuwa wanaongea kama yanafanana na haya waliyoongea kabla, na baada ya kufika kwetu.
Oh! Sikufuatilia maneno ya hawa ili kufanya huo ulinganifu. Nimejibu postbysko kwa basis ya statement ya kulaani kama ullivyokuwa umeiweka, maana hukuonyesha content yoyote ya ulinganifu mkuu. Just that.
 
Lakini pia hakuna asiyejua ya kuwa wakati wa utawala wa Mobutu Seseko wa Zaire (sasa DR Congo), Tanzania iliingilia masuala ya Zaire kwa kuwahifadhi Desire Kabila (Baba Ntwale) na mwanaye hadi wakafanikisha kumuondoa madarakani Rais Mobutu. Mifano haiishi kwani sio watu wengi wanajua kuwa wanajeshi wetu walikwenda katika Visiwa vya Commoro. Lakini kama walikwenda kutembea au walikwenda kula pikiniki, ajuaye ni Rais Kikwete na Jenerali wake Davis Mwamunyange.
Aisee
 
Nafikiri Rais hana uelewa wa historia za upigania uhuru na diplomasia. Hajui hata ushiriki wa Tanganyika kusaidia wapigania uhuru wa nchi nyingi kusini mwa Africa.
 
UPUUZI MTUPU!

Mwanasiasa wa Uganda Kizza Basigye alitekwa nchini Kenya akiwa ameomba hifadhi nchini humo, na kupelekwa Uganda kushtakiwa katika mahakama za jeshi.

Je wanaharakati wa Kenya hawakuliona hilo la mtu kutekewa nchini kwao, na kupelekwa Uganda?

Mbona hawakutoa matamko yoyote ya kuilaani serikali yao ya Kenya kwa kuruhusu utekaji huo nchini kwao?

Halikadhalika mbona hawakupaza sauti wala kwenda nchini Uganda kushurutisha serikali ya Uganda imuachie huru mpinzani huyo.

Kwanini harakati zao wazifanye kwa Tanzania tu na sio Uganda, Rwanda au Burundi?

Pia juzikati kuna mbunge wao alipigwa risasi huko huko kwao, lkn hatukuona matamko yao ya kukemea jambo hilo. Ila kwa Tanzania ndio walifikiri ni kichaka cha kuja kujifunzia kupayuka payuka, na kuokoteza umaarufu uchwara.
Una uhakika hawakuingilia? Haya umeyajua kwa kuwa yanakuhusu.
Hivyo unaona kinachofanyika ni sawa? Kuwashitaki wapinzani kwa mashtaka ya uongo? Ama nchi Kuteka na kuua raia zake? Kuzuia haki za washtakiwa.
Inawekana huoni kwa sababu halijakupata. Subiri wewe au ndugu Yako yamkute!
Hawa watu walikuja kusikiliza ili haki itendeke. Hofu ni nini?
 
USHAURI WA ASKOFU KWA RAIS SAMIA JUU YA WANAHARAKATI WATOKAO NCHI ZA NJE!

Tarehe 19 Mei 2025 ni siku iliyokuwa imebana sana kwangu. Sikuweza kufanikiwa kufuatilia hotuba yeyote iliyotolewa na Mheshimiwa Rais Samia Saluhu Hassan. Hata hivyo, usiku niliona habari picha kadhaa zikiwa na maneno ambayo yanaelezwa kuwa yalitolewa na Rais Samia.

Katika habari picha mojawapo, Rais alinukuliwa akisema: "Tusitoe nafasi kwa wanaharakati wa nje kuingilia masuala ya Tanzania"! Kama kauli hiyo ni ya Rais Samia Saluhu Hassan, nchi yetu itakuwa imefikia hatua mbaya sana kwani hata Rais amejua kuwa tumefikia mahali ambapo tunahitaji watu au wanaharakati wa nje kutetea wananchi wa Tanzania.

Huko nyuma kuanzia mwaka 1961 hadi 1990, wanaharakati, wanasiasa na viongozi kutoka Tanganyika na baadaye Tanzania ndio ambao walikuwa wakiingilia masuala ya nchi jirani au nchi za nje. Wanaharakati, wanasiasa, watetezi na viongozi hao waliokuwa wakiingilia mambo ya nchi nyingine waliongozwa na Rais Julius Nyerere mwenyewe.

Wakati Rais wa Malawi, Dkt. Hastings Kamuzu Banda anatesa na hata kuua watu wake, nchi ya Tanzania sio tu kuwa iliingilia masuala ya nchi ya Malawi, bali pia iliwapa hifadhi watu na wakimbizi kutoka Malawi akiwemo mwandishi nguli aliyekuwa akiandikia gazeti la Daily News.

Wakati Idi Amini Dada alipoipindua serikali ya Uganda na kumuondosha madarakani Rais Milton Obote, Rais Nyerere aliingilia masuala ya Uganda, akaenda mbali zaidi akawa hifadhi Milton Obote, Yoweri Kaguta Museveni, nk.

Wakati Afrika Kusini ilipokuwa chini ya mfumo wa utawala wa ubaguzi wa rangi, Tanzania ya Rais Julius Nyerere iliingilia masuala ya Afrika Kusini kwa kuhamasisha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya nchi hiyo ikatoa ardhi kwa wapiganaji wa Afrika Kusini.

Nchi nyingine ambazo ziliingiliwa wanasiasa, wanaharakati na wapiganaji wa Tanganyika na baadaye Tanzania ni pamoja na Rhodesia (sasa Zimbabwe), Msumbiji, Angola, Namibia, Algeria, nk.

Lakini pia hakuna asiyejua ya kuwa wakati wa utawala wa Mobutu Seseko wa Zaire (sasa DR Congo), Tanzania iliingilia masuala ya Zaire kwa kuwahifadhi Desire Kabila (Baba Ntwale) na mwanaye hadi wakafanikisha kumuondoa madarakani Rais Mobutu. Mifano haiishi kwani sio watu wengi wanajua kuwa wanajeshi wetu walikwenda katika Visiwa vya Commoro. Lakini kama walikwenda kutembea au walikwenda kula pikiniki, ajuaye ni Rais Kikwete na Jenerali wake Davis Mwamunyange.

Kama asilimia kubwa ya Watanzania wanajua ya kuwa upinzani unanyanyaswa nchini huku viongozi wao kama Ali Kibao wameuawa na wengine kama Soka, Kipanya, Chaula, Mlay, Mbise na Mdude wametekwa na hawajulikani waliko, hautarajiwi kuwa wanaharakati wa nchi za jirani wasijue kuwa kuna ufinyaji wa haki za msingi nchi ikiwemo haki ya kuishi.

Lissu alipigwa risasi 16 mchana kweupe akiwa katika majengo ya serikali yanayolindwa pia na serikali lakini hadi sasa hakuna mtu ye yote aliyekamatwa na wala hakuna uchunguzi wo wote uliofanywa hadi sasa. Lissu amekamatwa na kupewa makosa mazito kabisa duniani ya uhaini ambayo hatima yake ni kunyongwa hadi kufa. Katika mazingira kama hayo, haitarajii ya kuwa wanaharakati kutoka nje za nje watakaa kimya wasiingilie mambo ya Tanzania. Kama Tanzania ilitia sahihi mikataba ya kimataifa juu ya haki za binadamu, ni lazima itaingiliwa na wanaharakati kutoka nchi za nje.

Kama wao Rais Samia, CCM pamoja na serikali yake wanataka Tanzania isiingiliwe na watu au wanaharakati kutoka nchi za nje, basi wafanye mambo mawili. Mosi, waandike katiba mpya au wabadili katiba iliyopo ili wanyofoe kifungu kile kinacholinda haki za binadamu. Pili, wafanye haraka sana juhudi kuiondosha Tanzania katika mikataba yote ya kimataifa. Baada ya kufanya hivyo, waiondoe Tanzania kutoka katika Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Madola, Jumuiya ya Afrika Mashariki, COMESA, SADC, nk.

Wakimaliza kufanya yote hayo, ndipo Tanzania ivunje uhusiano wa Kibalozi katika nchi zote duniani na iwaite Mabalozi wake wote walioko katika nchi hizo, mwisho iwafukuze Mabalozi wote wa nchi za kigeni walioko Tanzania. Hapo ndipo itoe kauli ya kutokuingiliwa na wanasiasa na wanaharakati kutoka nchi za nje kwani sasa Tanzania itakuwa tayari ni Kisiwa cha Mbudya!
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam, 20 Mei 2025; saa 3:45 asubuhi.
Askofu amenena, chawa watapoteana!
 
Asante sana askofu Mwamakula kwa ujumbe wako mzuri. Naamini, kwa nguvu ya Mungu wetu, walengwa watakuelewa na kuyafanyia kazi. Ubarikiwe sana.
 
Kwa kuboresha tu hiyo Law inapatikama Form 1 na inapatikana pia Physics form V, Module ya Mechanics, section ya Motion.

"To every action, there is equal and opposite reaction"

Newton's third law of motion.
Hongera mkuu! Nilipenda fizikia, lakini nilisoma tu hadi Form II, maana hatukuwa na walimu wa kufundisha madarasa yanayofuata.
 
Huyu Askofu huwa amekonda, sijui tayari ana JULIANA
 
Oh! Sikufuatilia maneno ya hawa ili kufanya huo ulinganifu. Nimejibu postbysko kwa basis ya statement ya kulaani kama ullivyokuwa umeiweka, maana hukuonyesha content yoyote ya ulinganifu mkuu. Just that.
Ok mkuu! Nimeuliza hivyo kwa sababu nika uhakika kuwa hawa watu wengi wao hawaipendi Tanzania. So hili swala la kesi ya Lisu limefanywa kama daraja la kufikia malengo yao ya kuichafua Tanzania, kitu ambacho mimi binafsi sikubaliani nacho.

Kama ni swala la haki kuminywa basi halikuanzia Tanzania. Hata huko kwao kuna watu wengi wananyimwa haki, na wengine mpaka kunyang'anywa ushindj wao katika uchaguzi mkuu (Odinga) na kupelekea fujo iliyogharimu maisha ya ndugu zao wakenya.

Rwanda na Burundi kuna wapinzani likuki wamewekwa ndani kwa sababu za kisiasa, lkn huko hawaendi kwa sababu hawana masilahi napo wala chuki napo.

Sipati picha kama lile tukio lililofanywa na Uganda nchini Kenya, lingefanywa na Tanzania hali ingekuaje!!
 
Mhuyu mbuzi naye angalia anayojambia humu jukwaani aende zake huko HAKUNA KUWARUHUSU HAO VIBARAKA WAJE KUTUHARIBIA NCHI YETU YANAWAGHUSU NINI HAYA YA KWETU WAMEBANWA KWAO WANAKIMBILIA KWETU HAKUNA KUWAPA NAFASI MAMA SHIKILIA HAPOHAPO
Haya ndiyo Matunda ya sekondari, Veta na vyuo vikuu vya kata. Haya ni matumizi mabaya ya Ubongo na akili aliyokupa mwenyezi Mungu.
 
Back
Top Bottom