Ushauri wa Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula kwa Rais kuhusu wanaharakati kutoka nje

Aliyemoiga risasi mbunge ameshakamatwa, he aliyempiga risasi Lisu ameshakamatwa? Waliomua Kibao wako mahabusu?
Nadhani huji ulichojibu.
Juzi tu mmeingilia mambo ya congo kwa mgongo wa Sadeki,kwa ujinga wa watu kama wewe tukapoteza askari wetu.
Inawezekana huna historia nzuri ya harakati.
Mwl Nyerere alikuwa mwana harakati,
Kisha mwana siasa, hata hivyo alifanya harakati katika nchi huru akaunga mkono wapiganaji katika nchi hizo, ni kwa kuwa aliona kuna watu wanakandamuzwa, wanateswa, hawana haki hata ya kusema katika nchi yao. Mifano ni mingi sana.
Sina hakika kama alichokisema Rais ni chake ,nahisi ameandaliwa na kulishwa chakula asichokijua.
Museveni, John Galang, Kabila mkubwa na mtoto wote wamehifadhiwa na serikali ya Tanzania, wengine wakisoma hapa hapa katika vyuo vyetu na kisha kwenda kupigania haki katika nchi zao.
Viongozi wa Anc,swapo, Frelimo na vikundi vingine vingi waliiishi hapa hadi leo wanabaki ya makazi yao hapa.
Tusijisahu leo unawafukuza kesho ni viongozi wa mataifa yao, utaweka wapi uso wako? Au ndo ile samahani,unajua wakati uleee. Hovyo kabisa
 
hivi huyo ndie Askofu Mkuu wa Chadema Church of Tanazania (CCT), right?
 
Una uhakika hawakuingilia?
Wewe mwenye ushahidi wa wanasheria wa kenya wakienda Uganda kuingilia mamlaka, na kumtetea Basigye aachiwe kama walivyotaka kufanya kwa Tanzania uuweke hapa.
Haya umeyajua kwa kuwa yanakuhusu.
Hivyo unaona kinachofanyika ni sawa? Kuwashitaki wapinzani kwa mashtaka ya uongo?
Hilo la kesi ya kweli au ya uongo litajulikana mahakamani. Hakuna mtu ambae hukubali kosa kirahisi rahisi ndomaana hata majambazi mauaji hupinga mahakamani kua yaliua. Moyo wa mtu msitu, wewe huwezi jua kilichojificha ndani ya akili ya mtu.
Ama nchi Kuteka na kuua raia zake? Kuzuia haki za washtakiwa.
Kama swala ni kuua basi wangebaki kwanza wanapambana na serikali yao iliyoua wakenya waliokuwa wanaandamana kuipinga serikali kwa sababu ya ugumu wa maisha. Kwanini utoe kiboti katika jicho la mwenzio wakati wewe mwenyewe unacho? Pia kumbuka kuna mbunge juzi alipigwa risasi huko huko kwao.
Inawekana huoni kwa sababu halijakupata. Subiri wewe au ndugu Yako yamkute!
Hawa watu walikuja kusikiliza ili haki itendeke. Hofu ni nini?
Mimi haiwezi kunipata kwa sababu nafuata sheria za nchi. Siropoki, sivunji sheria wala kutumiwa na mabeberu kulichafua taifa langu kwa mgongo wa siasa uchwara.
 
Hivi huwa huwa unafuatilia habari za kimataifa kweli?

View: https://youtu.be/fMHMk8__BxY?si=KGu7fuK-qytdl8H1
 

Tunakukumbusha tu Binti wa watu marehemu Aquillina hakuwa mropokaji na hakuwahi kuvunja Sheria za nchi ila alipigwa risasi na kufa pale mwembechai.
 
Nimesoma aliyoyaandika askofu nimeyaona ni sawa kabisa ila ameshindwa ikiwa ni pamoja na wewe kutofautisha kati mwanahakati mmoja mmoja na serikali kwa maana ya maamuzi ya nchi. Kama hao wanatumwa na serikali za nchi zao ni jambo lingine lakini kama wanakuja wao kama wao na sio kwa niaba ya serikali zao basi liko tatizo mahali na hayo sio makubaliano.
 
Wale wananchi wanaokuja kununua mapera mbeya kutoka kenya wanakuwa wametumwa na Serikali ya Kenya?
 
HIZI HEKA HEKA NIMEZIPENDA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…