Ushauri wa biashara kwa mtaji wa million moja na nusu

Mende mdudu

Senior Member
Joined
Feb 13, 2023
Posts
111
Reaction score
223
Kuna mtu anaomba ushauri nikaona niwashirikishe wanafamilia wa jf,

Ana million moja na nusu anataka kununua bodaboda used namba d ampe mtu ampe elfu nane kwa siku au afungue saluni za mtaani kinyozi ampe elfu saba kwa siku

Wazoefu wa biashara izo toeni ushauri
 
Unapoazisha biashara yoyote ile kitu Cha kwanza ni kulinda na kukuza mtaji halafu mambo ya faida yanafuata. Biashara yoyote ambayo atazisha kwa mtaji million 1 na nusu inatakiwa aifanye yeye maana huo mtaji ni mdogo sana na inahitaji usimamizi makini .
Binafsi namshauri atafute mtaa ambao umechangamka afungue genge, ila kwenye genge awe makin na wake za watu na wadada wa kazi.
 
Saluni Kwa 1.5M? Toa mchangsnuao haitoshi iyo ela
Kiti Cha kutengeneza Kwa ma welders haizidi 70k, viio 2 laki na 40, mashine mbili 50k, Kodi miezi 3, mengineyo ambayo nimesahau ongezea laki 2.5 . Aaah mkuu inatosha anaweka kinyozi na yy anabaki na mtaji wa kufanya ishu zingine. Au wewe unataka barbershop?
 
Kwa huo mtaji ingekua vzr angeanzisha kitu ambacho yeye angeweza kukisimamia Kwa ufanisi bila kumpa mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…