Mkoa Dar es salaam, na gari ni coaster
Sijui vitu vingi ila naweza kusaidia kwa uchache maana jamaa yangu yuko anafanya vitu hivi.. daladala inayoonekana kudumu ni hizi Nissan civilian kwa Dar es Salaam naona matajiri wengi wanazikimbilia (unaweza agiza au ukanunua kwa mtu )
Unapokuwa na daladala, mambo muhimu hakikisha una sehemu ya uhakika ya kulaza gari yako, kwa nini nasema hivi “hii itakusaidia pale utakapokuwa na daladala then unaweka limitation ya kupark gari kama ni saa au saa 3 gari iwe parking, itasaidia kuitunza gari maana deiwaka zipo sana”
Hakikisha una fundi wako wa daladala unayemuamini au gereji in case ya tatizo la daladala fundi ndio ana verify tatizo then spear inatafutwa... Kwa nini nasema hivi “unaweza pigiwa simu ukaambiwa tumenunua kifaa fulani tukafunga kumbe uongo”
Jitahidi ujue sehemu utakapopata vifaa kwa bei rahisi hii itapunguza cost kwako maana sometimes fundi naye anaweza weka cha juu.
Ni mengi ila hayo kwa uchache.. hesabu ya siku inategemeana na route kuna hesabu 90,000, laki kwa hizi daladala za kawaida.. tena gari ikiwa mpya kazia hesabu
Mpe dereva uhuru wa kufanya kazi.. sikiliza pale kunapotokea matatizo ya kihesabu.. sometimes kuwa mkali usiwe normal yaani
Usitegemee sana daladala kama sehemu ya kipato cha kuendeshea maisha iwe ni ziada katika uwekezaji wako
..zaidi utauliza na wadau watachangia #asante