Ungekua na suzuki carry almaarufu kama kirikuu ungeweza kupiga hela kwa kukaa vijiweni jirani na maduka ya hardware. Ungeweza pia kutumia social networks zako kujitangaza kuwa unatoa huduma za usafiri mfano kwa watu wanaohama nyumba. Ungeweza pia kuwa supplier wa vitu madukani hata majumbani. Ungeweza pia kuweka matunda na kuifanya iwe movable genge unaangalia sehemu yenye mkusanyiko wa watu unapaki unauza matunda. Unaenda zako mnadani unapaki unauza matunda. Jumapili unapaki kwenye lango la kutokea kanisani unapiga hela.
ILA SASA WEWE UNA MARK 2 HUNA KIRIKUU ndo maana hapo umepishana na gari la mshahara.
Ila sio mbaya unaweza kuifanya kama TAXI inaweza kukulipa.
Pia unaweza kuanzisha fastfood yako unapikia home au getoni kwako unatengeneza na juice na matunda fresh unakua unafanya delivery maofisini benki n.k. vaa vizuri kama bosi wa maofisi utakayotembelea afu waambie unauza msosi. Tafuta na msaidizi mmoja wa kike mzuri mzuri uwe unaambatana naye.
All the best. Kapambane