Ushauri wa biashara

Ushauri wa biashara

Swelana

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2016
Posts
418
Reaction score
1,259
Wandugu,
Naombeni ushauri,nimehangaika sana mtaani na ajira mpaka imekuwa kero.
Sasa nimebahatika kupata ka usafiri yaani gari ndogo nimesohezewa na ndugu yangu ili nitafutie biashara ya kufanyia.
Sasa naumiza kichwa ni biashara gani naweza kusambaza kwa kutumia hiyo gari ndogo aina ya mark 2 na angalau nikaokoteza?
Nina ka mtaji ka laki mbili tu,ndugu zangu tusaidiane hata ushauri mambo yamekuwa magumu sana.

Nitashukuru sana.
 
Ungesema upo Mkoa gani mkuu ili atakaetoa ushauri atoe ushauri unaolingana na eneo ulilopo.
 
Ungekua na suzuki carry almaarufu kama kirikuu ungeweza kupiga hela kwa kukaa vijiweni jirani na maduka ya hardware. Ungeweza pia kutumia social networks zako kujitangaza kuwa unatoa huduma za usafiri mfano kwa watu wanaohama nyumba. Ungeweza pia kuwa supplier wa vitu madukani hata majumbani. Ungeweza pia kuweka matunda na kuifanya iwe movable genge unaangalia sehemu yenye mkusanyiko wa watu unapaki unauza matunda. Unaenda zako mnadani unapaki unauza matunda. Jumapili unapaki kwenye lango la kutokea kanisani unapiga hela.

ILA SASA WEWE UNA MARK 2 HUNA KIRIKUU ndo maana hapo umepishana na gari la mshahara.

Ila sio mbaya unaweza kuifanya kama TAXI inaweza kukulipa.

Pia unaweza kuanzisha fastfood yako unapikia home au getoni kwako unatengeneza na juice na matunda fresh unakua unafanya delivery maofisini benki n.k. vaa vizuri kama bosi wa maofisi utakayotembelea afu waambie unauza msosi. Tafuta na msaidizi mmoja wa kike mzuri mzuri uwe unaambatana naye.

All the best. Kapambane
 
mark 2 hapo ni mwendo wa lift, breki kiuno, laki 2 ikiisha badilishana na mtu ama uza nunua scarry. 1G FE kavu ama VVTI sio rafiki kwa biashara
 
Wazo zuri
Ungekua na suzuki carry almaarufu kama kirikuu ungeweza kupiga hela kwa kukaa vijiweni jirani na maduka ya hardware. Ungeweza pia kutumia social networks zako kujitangaza kuwa unatoa huduma za usafiri mfano kwa watu wanaohama nyumba. Ungeweza pia kuwa supplier wa vitu madukani hata majumbani. Ungeweza pia kuweka matunda na kuifanya iwe movable genge unaangalia sehemu yenye mkusanyiko wa watu unapaki unauza matunda. Unaenda zako mnadani unapaki unauza matunda. Jumapili unapaki kwenye lango la kutokea kanisani unapiga hela.
ILA SASA WEWE UNA MARK 2 HUNA KIRIKUU ndo maana hapo umepishana na gari la mshahara.
Ila sio mbaya unaweza kuifanya kama TAXI inaweza kukulipa.
Pia unaweza kuanzisha fastfood yako unapikia home au getoni kwako unatengeneza na juice na matunda fresh unakua unafanya delivery maofisini benki n.k. vaa vizuri kama bosi wa maofisi utakayotembelea afu waambie unauza msosi. Tafuta na msaidizi mmoja wa kike mzuri mzuri uwe unaambatana naye.
All the best. Kapambane
 
uza hyo gar upate hela cash ambayo utaitumia km mtaji
 
Back
Top Bottom