Ushauri wa bure: CHADEMA iachane na issue ya Wabunge wake 19, iwasamehe waendelee na Ubunge wao. Kwa muda uliobakia kuwatengua hakuna maslahi yoyote!

Ushauri wa bure: CHADEMA iachane na issue ya Wabunge wake 19, iwasamehe waendelee na Ubunge wao. Kwa muda uliobakia kuwatengua hakuna maslahi yoyote!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi

Ibara ya 49 (5) ya Sheria Mpya ya Uchaguzi inasema (5) Endapo uchaguzi mdogo unatakiwakufanyika na tarehe ya kuvunjwa kwa Bunge imetangazwa au imejulikana kwa mujibu wa matukio yaliyo ainishwa katika Ibara ya 90(3) ya Katiba, uchaguzi mdogo hautafanyika katika muda wowote wakati wa kipindi cha miezi kumi na mbili mara tu baada ya tarehe ya kuvunjwa kwa Bunge.

Hivyo nashauri Chadema iachane na hili jambo, kwa muda huu uliobakia kabla ya kuvunjwa kwa bunge, hakuna tena uchaguzi mdogo wowote, hivyo jambo hili halina maslahi yoyote kwa Chadema, kama nilivyoshauri toka mwanzo, CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao

Baada ya Chadema kuutambua uchaguzi wa 2020 na kumtambua mbunge wake mmoja Mhe. Aida Khenan, Chadema ilikuwa inapigania hao wabunge 19, watenguliwe, ili iteau wabunge 19 wengine, lakini sasa kwa muda uliobakia kabla ya kuvunjwa kwa Bunge, hakuna uchaguzi mdogo wowote mpaka uchaguzi ujao!, hivyo hata kama watashindwa mahakamani na kuvuliwa ubunge, hakutakuwa na maslahi yoyote kwa Chadema!.

Hivyo ni bora Chadema iwasamehe, ujikusanyie maokoto yao kwa ule utaratibu wao, Bunge likishavunjwa, ndipo imalizane nao ndani kwa ndani. Kitendo cha kuwasamehe, watu kama Halima Mdee, Esta Matiko na Esta Bulaya ni watu wenye uwezo mkubwa kurejea Bungeni.

Huu ni ushauri tu

Paskali
Mabandiko mengine ya mwandishi kuhusu issue hii ya wabunge 19 wa Chadema
  1. CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao
  2. Wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii. CHADEMA wana macho? Je, wawasamehe Wabunge 19 wabarikiwe, au wakomae nao walaaniwe?
  3. "Mzoea vya kunyonga vya kuchinja Haviwezi". Hongera Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji
  4. Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa. CHADEMA inakaribia kufa, hii ndio njia yenu pekee ya kujinasua
  5. Je, wabunge 19 wa CHADEMA walijiteua? Je, CC ya CHADEMA ni Kangaroo Court? Je, Baraza Kuu litabariki ukangaroo ule?
  6. A Kangaroo Court Moja, Kutoa Hukumu Kikangaroo, Kisha Kikao cha Rufaa, Kikiyabariki Maamuzi yale ya Kikangaroo. Je, nacho ni A Kangaroo?
  7. Spika Dkt. Tulia yuko sahihi sana, CHADEMA wajifunze kufanya vitu kwa usahihi na wafanye kiusahihi
  8. J Mnyika, Aunguruma Channel TEN, Athibitisha maridhiano yameisaidia Sana CHADEMA, Sasa Inayatambua Matokeo, Inalitambua Bunge na Kumtambua Mbunge Wake
  9. Makamanda walioigharimia CHADEMA kwa machozi, jasho na damu, leo ni wakuitwa wasaliti? Karma Haitawaacha salama, itawatandika tu
  10. "Mzoea vya kunyonga vya kuchinja Haviwezi". Hongera Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji
  11. The Voices From Within: "Mahakamani Watashindwa Tena!" Sababu ni Mawakili! Jee Tanzania Tuna Mawakili wa Calibre ya Murtaza Lakha?Jitokezeni Kusaidia!
  12. Ushauri wa Bure: Ukijikwaa ukaanguka, usiangalie tu pale ulipoangukia, bali angalia pale ulipojikwaa
  13. Voices From Within: Unaweza usiamini! Aliyetoa A Go ahead kwa Mdee na Wenzake ni Kigogo wa Chadema!. Alikuwepo Ukumbini na Vikaoni! Je, ni nani?
  14. Ni Ubatili Mtupu Mpaka Basi!. CC ya CHADEMA ilipata wapi mamlaka?. Baraza Kuu halina mamlaka hiyo!. Je, inawezekana CHADEMA ni chama majanga ila?
  15. Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.
    Kufanya Kosa Si Kosa, Kosa Kurudia Kosa,
  16. CHADEMA is Almost Dead, Due to deadly mistakes!, This Your Only Survival, Do or Die!, Msirudie Kosa!.
  17. Je, wajua Vyama vya Siasa TZ ni Public Parties? Maamuzi yake lazima yazingatie Public Interest na siyo kufuata ujinga na ubinafsi wa viongozi insane!.
  18. Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni?.
  19. JPM, CCM wakishinda, Freeman Aikaeli Mbowe ni lazima ajiuzulu, amwachie Tundu Lissu. Lissu aache Uanaharakati, aonyeshe Statesmanship.
  20. For the sake of National Unity, Je tumshauri Dkt. Magufuli aahidi kumteua Tundu Lissu kuwa Mbunge?
 
Sioni kama kuna mtu ana muda na ushauri wako. Na huko cdm hakuna mwenye muda na hao akina Mdee, Wala hawawamisi na hawako kwenye mtarajio Yao. Watarejea bungeni kwa uchaguzi gani, huu huu ambao mwenyekiti wa ccm anapanga nani atangazwe mshindi?
 
Ka' Pasco , nina maswali machache, huenda hii ni post yako ya Mwisho kabla hujateuliwa kuchukua nafasi Bi Zuu aliyeondolewa Pale MAGOGONI.

1. Wasaliti hawa 19 wameomba msamaha?
2. Wasaliti hawa 19 inasemekana wamenunuliwa kwa vipande vya fedha, jinai haifi, rushwa haina ukomo, je Huoni itakuwa ticket ya kuwaengua watapogombea kwakuwa mtoaji ana ushahidi?
3. Damage ya Chama waliyosababisha hawa "virusi 19" inatibika kwa neno la mtu kuwasamhehe?
4. Kama Mwenyekiti Mbowe alikwenda, kwa nia njema kabisa, ikulu kuridhiana na CCM na chama kikaanza kupasuka na UVCCM wenyewe wakapa credit kuwa amelishwa asali, vipi kama akisema wamewasamehe, si ndio watasema kajengewa majumba Dubai na kulamba asali?

My take: Waendelee kula dhulma yao, wao na vizazi vyao mpaka cha nne, [ahadi kwenye Biblia na haitokaa kubadilika]!
 
Kwa upande mmoja wa Shilingi, uko sahihi. Lakini kwa upande mwingine, nadhani hujajielekeza sawa. Hizi Kesi pamoja na kutoa Hukumu Bado Zina umuhimu wa kuweka Precedence kwa Hali na mazingira yanayofanana kwa nyakati zijazo.

Hivyo hata kama CHADEMA (kama ikifanikiwa), haitapata manufaa yoyote kwa matakwa ya Sheria uliyoitaja, Lakini itakuwa imefanikiwa kuishawishi mahakama na mahakama ikaweka misingi itakayosimama kwa matukio ya aina hiyo hapo mbeleni. Lakini pia itaudhihirishia umma kuwa Taratibu ilizofuata kwa mujibu wa Katiba Yao, ulikuwa ni utaratibu sahihi na utaendelea kuwa utaratibu sahihi Hadi hapo Katiba itakapokuja kivingine.
 
Hapo kwa suala hili la wabunge 19 chadema imeonyesha udhaifu mkubwa sanaaaa tena sanaaa miaka mitano huku wakijinasibu wana wanasheria nguli huku wakijinasibu kuwa wana haki ya kila kitu na bado wameshindwa kuwatoa bungeni ukiona hivyo hoja zao zilikuwa dhaifu sana kuwatoa hao kina dada bungeni na bado watawatesa sanaaaa
 
Kwa upande mmoja wa Shilingi, uko sahihi. Lakini kwa upande mwingine, nadhani hujajielekeza sawa. Hizi Kesi pamoja na kutoa Hukumu Bado Zina umuhimu wa kuweka Precedence kwa Hali na mazingira yanayofanana kwa nyakati zijazo.

Hivyo hata kama CHADEMA (kama ikifanikiwa), haitapata manufaa yoyote kwa matakwa ya Sheria uliyoitaja, Lakini itakuwa imefanikiwa kuishawishi mahakama na mahakama ikaweka misingi itakayosimama kwa matukio ya aina hiyo hapo mbeleni. Lakini pia itaudhihirishia umma kuwa Taratibu ilizofuata kwa mujibu wa Katiba Yao, ulikuwa ni utaratibu sahihi na utaendelea kuwa utaratibu sahihi Hadi hapo Katiba itakapokuja kivingine.
Lakini ndiyo wameshindwa kuudhihirishia umma kuwa katiba yao iko sawa inamaana wao ndiyo walikuwa wanavunjaq katiba yao ndiyo maana wameshindwa kuwatoa
 
Back
Top Bottom