Wanabodi
Ibara ya 49 (5) ya Sheria Mpya ya Uchaguzi inasema (5) Endapo uchaguzi mdogo unatakiwakufanyika na tarehe ya kuvunjwa kwa Bungeimetangazwa au imejulikana kwa mujibu wa matukioyaliyoainishwa katika Ibara ya 90(3) ya Katiba,uchaguzi mdogo hautafanyika katika muda wowotewakati wa kipindi cha miezi kumi na mbili mara tubaada ya tarehe ya kuvunjwa kwa Bunge.
Hivyo nashauri Chadema iachane na hili jambo, kwa muda huu uliobakia kabla ya kuvunjwa kwa bunge, hakuna tena uchaguzi mdogo wowote, hivyo jambo hili halina maslahi yoyote kwa Chadema, kama nilivyoshauri toka mwanzo,
CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao
Baada ya Chadema kuutambua uchaguzi wa 2020 na kumtambua mbunge wake mmoja Mhe. Aida Khenan, Chadema ilikuwa inapigania hao wabunge 19, watenguliwe, ili iteau wabunge 19 wengine, lakini sasa kwa muda uliobakia kabla ya kuvunjwa kwa Bunge, hakuna uchaguzi mdogo wowote mpaka uchaguzi ujao!, hivyo hata kama watashindwa mahakamani na kuvuliwa ubunge, hakutakuwa na maslahi yoyote kwa Chadema!.
Hivyo ni bora Chadema iwasamehe, ujikusanyie maokoto yao kwa ule utaratibu wao, Bunge likishavunjwa, ndipo imalizane nao ndani kwa ndani. Kitendo cha kuwasamehe, watu kama Halima Mdee, Esta Matiko na Esta Bulaya ni watu wenye uwezo mkubwa kurejea Bungeni.
Huu ni ushauri tu
Paskali
Mabandiko mengine ya mwandishi kuhusu issue hii ya wabunge 19 wa Chadema
- CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao
- Wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii. CHADEMA wana macho? Je, wawasamehe Wabunge 19 wabarikiwe, au wakomae nao walaaniwe?
- Je, wabunge 19 wa CHADEMA walijiteua? Je, CC ya CHADEMA ni Kangaroo Court? Je, Baraza Kuu litabariki ukangaroo ule?
- Spika Dkt. Tulia yuko sahihi sana, CHADEMA wajifunze kufanya vitu kwa usahihi na wafanye kiusahihi
- J Mnyika, Aunguruma Channel TEN, Athibitisha maridhiano yameisaidia Sana CHADEMA, Sasa Inayatambua Matokeo, Inalitambua Bunge na Kumtambua Mbunge Wake
- mkeka unaendelea...