Ushauri wa Bure: Diamond saidia baba yako

Ushauri wa Bure: Diamond saidia baba yako

Ila diamond naye mbona kama anafuata nyayo za baba ake. Mara ya mwisho kaenda kuona wanae lini. Anayomfanyia baba ake leo akifanyiwa yeye kesho atasemaje.
Kwa hili siwez mtetea unless na yeye angekua baba bora sio bora baba.
 
Umefikiria iwapo Diamond angekuwa maskini, huyo mzee angemjali mwanae?

Hata sasa sijui kama anamjali au hamjali. Ninachoona mimi hakuna faida yeyote kwa Diamond akimwacha mzee aendelee kuhangaika. Ila ipo faida kubwa akimsaidia.
 
Baada ya Paul Ince kupata mafanikio katika soka, siku moja akiwa mazoezini alitokea Mzee Mmoja akidai yeye ndiye Baba halisi wa Paul,

Kilichotokea baada ya hapo,ni habari nyingine.


Sikiliza kibao cha Q chief (Q chilla) "ulinizaa wewe ukanikataa ",ndiyo utajua wanaume wengi tunakosea wapi kwenye mahusiano yetu.
 
Naandika nikiamini kwa namna moja au nyingine ushauri huu utamfikia huyu kijana Diamond. Yeyote asiye na maelewano na wazazi/mzazi wake pia inamuhusu. Na wazazi wanaotelekeza vizazi vyao pia wanaweza kujifunza jambo.

Mimi ni mmoja kati ya watu wanaopenda namna Diamond anavyojituma katika kazi pamoja na ubunifu katika muziki na biashara ya muziki. Pia amekuwa mstari wa mbele kusaidia vijana wenzake, hususan waliotoka katika hali duni kimaisha kama ilivyokuwa kwake, kupata maendeleo kupitia sanaa. Tumeshuhudia hali kadhalika mara kadhaa akirudi maskani Tandale na kuwasaidia wakazi wa huko, kidogo alicho jaaliwa, na mengine mengi mazuri.

Yapo pia mambo kadhaa ambayo sifurahishwi nayo kuhusu yeye, lakini nitalizungumzia hili la kumtelekeza Baba yake. Nimeona mahojiano ambayo baba Diamond amefanya na online TV moja. Ni wazi kwamba huyu mzee alitibuana na demu wake Sandra - mama Diamond, akatimka nyumbani na kutelekeza familia. Anasema wakati huo Diamond alikuwa na akili yake nzuri tu, hivyo huenda Diamond aliathirika sana kisaikolojia kwa Baba yake kutokomea kusikojulikana na kuwaacha yeye na mama yake hawana hata unga robo. Kutokana na maelezo yake aliyotoa na mazingira ya nyumbani kwake, huyu mzee ana hali ngumu. Baba Diamond sasa hivi anafanya biashara ya kukopa viatu vya mtumba Ilala, anarudi kwake magomeni anaviosha na kung'arisha kisha anatembeza mtaani, yaani Mmachinga typical. Anapoumwa kwa mfano, anakuwa hana hata fedha ya matibabu, hivyo kugeuka ombaomba. Kutokana na maelezo ya Mzee mwenyewe, majirani na mdogo wake Diamond anayeishi na baba yake, Diamond kufika kwa mzee wake ni tokea yuko na Wema!

Kilichonifanya kuandika huu uzi ni kwamba Baba Diamond ameomba msamaha kwa makosa aliyoyafanya. Tena amesema kwa uchungu kabisa, kwamba hata Mwenyezi Mungu husamehe. Kwa nini , yeye asisamehewe?. Binafsi naona imefika wakati Diamond akunjue moyo wake na kumsaidia Baba yake. Katika Qur'an, ipo wazi kabisa, kwamba baada ya Mwenyezi Mungu, wanafuata wazazi. "Be grateful to Me and to your parents; to Me is the [final] destination." (Quran 31:14). Mzee Abdul alikosea kumtelekeza mtoto Diamond, haijalishi walitibuana nini na mama Diamond. Diamond hajui nini hasa kilitokea. Mzee ameomba msamaha, anapaswa kusamehewa na maisha yaendelee.

Diamond rudisha maelewano na umsaidie baba yako. Amejutia na ameomba msamaha. Kwa sasa haikupunguzii chochote kumsaidia mzee wako aishi maisha ya kawaida, ya angalau ajue familia yake itakula nini jioni. Utakuwa na amani, Itakuongezea heshima katika jamii, na zaidi utapata credit kwenye daftari lako la Akhera. Maisha yenyewe ndiyo haya. Ukiishi sana 80. Ukiishi zaidi ya 80 ni maumivu tu, uwe na hela au huna. Akifa huyu mzee katika hali hii, Diamond utaaibika Duniani na akhera.
Family squabbles are non of your business

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeona YouTube mzazi ana busara sana kaongea mengi huku akimtakia mafanikio na nyota ing'are. Kasema suala la kumwalika harusini ni lake yeye Diamond cha msingi anapenda aone diamond anaoa na sio kugeuza nyumba daguro!!. Sijawahi kununua kazi ya Diamond na sio shabiki wa miziki yote ya Tz isipokuwa miziki ya OTTU JAZ BAND. Kijana nimemdharau sana kwani sisi wakristu tunafundishwa samehe saba mara sabini

Sent using Jamii Forums mobile app
Dogo mpuuzi sana, yeye anajua ndio ujanja. Muache tu, siku hazigandi namuambia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Diamond ana laaana kubwa, hata yule mama yake nadhani naye ni shithole yaaani rubbish.

Kijana mdogo kama Diamond unashindwaje kumsaidia baba yako ingali unajitapa unasaidia watu??. Yaani hata kama baba alikuumiza kwa kusikiliza masimulizi ya mama yako..bado baba atabaki kuwa baba yako hadi kifo. Dogo tahira sana yule, uhonge mademu umsahau baba yako eti alifanya nini sijui utotoni......... Diamond amepata pesa akiwa tahira sana na anaendelea kuwa tahira......hayo mashetani yake yatakapo mtoka tu atamtafuta baba yake. Pesa maua, anashindwa nini kumsaidia baba yake hata kinafki tu........, mzee hatakufa njaa yule ila laana kijana anayo mgongoni anatembea nayo
 
I ain't seen/heard no squabble. I have only seen a desperate father asking for forgiveness from his son.
All the same.....in simple words.....private family matters are to be kept private and let the family sort out their affairs in private. Mzee kulalamika kwenye media nadhani hatumii the right forum. Sense kwa wana ukoo etc....! I once read somewhere " life is about choices, and every choice has consequences. Make your choices and accept the consequences "

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnamuonea tu Huyo diamond ..... (mimi huwa sivutiwi na Tabia zake chafu chafu) ambazo zimenifanya nisimpende kabisaa"

Lakini kama ni kweli baba yake Alimtelekeza alipo kuwa mdogo kwaajili ya mgogoro na mzazi mwenzie

Basi ana stahiki kupatwa na hicho kinacho mfika " kwa sababu mtoto hakuwa na makosa

Huwa tuna vuna tunacho kipanda' so suala la kumuona diamond kuwa hamtendei haki baba yake " wakati baba yake mwenyewe mbegu aliyoipanda ndio hiyo" ni wazi mtakuwa mnanuonea tu diamond"....., mlitaka mzee avune karanga baada ya kupanda kokoto .. !?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo sasa!!!asingekua staa angemtafuta???

Au ndo mtoto mjinga wa mama...mtoto mwerevu wa baba!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasema tu hawa angekua teja angemtafuta?!!!huyo mzee aache unaafiki
Hakuna kitu kama hicho ... niupuuzi mkubwa huu ..mzazi unapaswa kumlea mwanao nakumpatia mahitaji yake ya msingi yatakayo muweza kumpatia msukumo wakuweza kuzifikia ndoto zake ",

Hata kama ni mzazi masikini komaa na family yako ipatie matunzo hata kama ni haba na uionyeshe upendo" watoto wakija kukua wataelewa tu kwamba mzazi wetu ni masikini lakini hakuwahi kutu telekeza alikuwa pamoja nasi katika kila hali "

Sasa kama wewe ni mzazi halafu uliikimbia family yako" na kumuacha mtoto wako akipitia tabu za maisha ", hakika haustahiki kuonewa huruma na dunia .... acha yakukute mazito

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnamuonea tu Huyo diamond ..... (mimi huwa sivutiwi na Tabia zake chafu chafu) ambazo zimenifanya nisimpende kabisaa"

Lakini kama ni kweli baba yake Alimtelekeza alipo kuwa mdogo kwaajili ya mgogoro na mzazi mwenzie

Basi ana stahiki kupatwa na hicho kinacho mfika " kwa sababu mtoto hakuwa na makosa

Huwa tuna vuna tunacho kipanda' so suala la kumuona diamond kuwa hamtendei haki baba yake " wakati baba yake mwenyewe mbegu aliyoipanda ndio hiyo" ni wazi mtakuwa mnanuonea tu diamond"....., mlitaka mzee avune karanga baada ya kupanda kokoto .. !?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo mzee angetokoroka na mtoto??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sentensi ni moja tu, dingi ni dingi tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Tena ni raha namna gani unaliona dingi lako limevaa kinyamwezi limependeza linakula matunda ya kiuno chake.

Nadhani ushirikina unamsumbua Diamond ndiyo maana aliweza kumnunulia gari Muidini Ngurumo na kumuacha baba yake anadhalilika kuomba chai kwa majirani.

Navyofahamu laana itatembea na baadhi ya watoto wa kiume kwenye uzao wa diamond

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora mzazi akukimbie au awatelekez mkiwa hamna akili timamu... Baba anawatelekeza mkiwa mnaona kabisa na mnajua hapa tumetelekzwa.. Huwa inakuwa ngumu sana kumuelewa mzazi wa aina hyo... Diamond ni kijana wa kiume baba alipowatelekeza yy atakua alichukua nafsi kubwa sana kuhakikisha mamb yanaend sawa nyimbn mpka kauza mitumba na mkumbke inasemkanaga diamond form four alifaulu lakin hakufanikiwa kuendelea kwa kukosa ada.. Kisaikolojia inaathir sana... haijalishi aliyewatelekeza anaish vzr au la.. Kama hamna taarifa nae yyte.. Nyie mtakuw mnafikiria tu mzee yupo huko anakula bata....! MIMI NI MUHANGA NINAJUA DIAMOND ANAVYO FEEL KWA MZEE WAKE....! Honestly nimekuja kumsamehe mzee dakika za mwisho kabla hajafariki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom