mkuu hujui hata kubadili tairi ??..
Weka gari pembeni ya barabara penye usalama then weka jiwe kwenye tairi (kama pancha tairi ya mbele kulia basi jiwe weka tairi ya nyuma kushoto ) then chukua wheel spanner na jeki kwenye buti. Hiyo jeki iweke upande wa tairi ya pancha kumbuka kuiweka kwenye ule mzingo wa chasis pembeni kidogo ya tairi sio katikati ya gari.
Legeza kwanza nut za tairi zikilegea piga jeki gari iinuke mpaka tairi iweze zunguka then fungua nut toa tairi. Kama kuna maji karibu lowanisha kitambaa then futa kwanza bolt ukimaliza chukua spare tire iweke halafu funga ila usikaze kwanza.
Shusha jeki then kaza sasa nut za tairi mpaka unapoona yatosha, usikaze saana inaweza pelekea kuua tread zake!. Baada ya hapo upo huru kurudi barabarani.
NB: Kama ni hizi highway au sehemu zenye pilika inakubidi kabla hujaanza hizi mambo toa hazard light zako piga hatua moja toka kwenye gari then moja weka mbele nyingine nyuma, huna weka hata majani. Tairi za kulia zikipata pancha kumbuka kutoka sana nje ya barabara kuepuka gongwa ukiwa unabadili.