Mkuu Buchanan,
Nakubaliana na wewe kuhusu swala la kauli za damu itamwagika. Tatizo la siasa za Tanzania ni kwamba chama kikishaonekana kuwa threat kwa CCM, whether utumie lugha laini au nyepesi au kauli nzuri, bado tu utavikwa ubaya hata kama ni wa kuokoteza. So, hai-make any difference.
Swala la mafisadi/Mkumbwa Alli, nadhani hapo wanaweza kutamka tu kwamba serikali mpya itafuata utawala wa sheria. Including kuwashughulikia hao mafisadi. Hata asipotaja kwamba atawafikisha mafisadi mahakamani, bado mtu yeyote ambaye anajijua ana matatizo ya kifisadi, hawezi kukipigia kura chama ambacho anajua kitakuja kufuata utawala wa sheria. Hivi unategemea mtu ambaye amezowea kuishi kwa misheni town anaweza kuipigia kura CHADEMA hata wasiposema kwamba watawashughulikia mafisadi? Bado proportion ya mafisadi ni ndogo sana hata ukijumlisha na extended family zao. Mafisadi kwanza huwa hawana undugu wala ujamaa, unaweza kushangaa mtu fisadi lakini some of his/her extennded family wako choka mbaya na wakisikia kwamba jamaa kapatwa na kasheshe wanashangilia kabisa. Mzee mzima alipoachia Uwaziri Mkuu kuna some of his extended family members walishangilia sana.