wewe bwana timua zako huko nenda kawashauri hao hao CCM wenzako. huna mema yoyote na CHADEMA wewe! muone kwanza, umekaa kiudini udini!!
CHADEMA ni chama cha matumaini. Matumaini kwamba Tanzania bila ya ufisadi inawezekana. Matumaini kwamba Tanzania inaweza kunufaika
kutokana na maliasili zake. Dr Slaa ameshasema kuwa atapunguza baraza la mawaziri, na hivi kupunguza matumizi ya serikali, na hivi kuongeza matumizi katika elimu ya watanzania. Elimu bure kwa Watanzania inawezekana, kama tutaipa kipaumbele. Na Tanzania inayojitegemea inawezekana, siyo hii ya omba omba mpaka tunaambiwa tungekufa njaa kama Kikwete asingeenda safari za nje.
1. Ccm hadi hivi sasa imefanya juhudi kubwa za kuifanya chadema ionekane kama chama chenye fujo na kinaharibu "utulivu na amani" wa watanzania!
Chadema bila kujua hila za ccm kimeingia mkenge hasa viongozi wake wanapodai kwamba kura zikiibiwa "damu itamwagika!" kauli hii iliwagharimu cuf na kilionekana ni chama kinachokusudia kuleta fujo, sasa hisia hizo zimehamia chadema!
2. Kauli zinazoashiria kupunguza idadi ya wapiga kura:
- nikiingia madarakani nitamtimua mhariri wa daily news: Mpiga kura huyo baada ya kuisikia kauli hiyo ataipigia kura chadema?
- nikiingia madarakani nitafuta vyeo vya u-dc: Hapa ina maana ma-dc wote hawatampigia kura dkt slaa kwa kuwa automatically vibarua vyao vitaota nyasi.
- nikiingia madarakani nitawaburuza mahakamani mafisadi wote: Hapa ina maana kuwa wale wanaojihisi kuwa ni mafisadi (kwa bahati mbaya hawa wako wengi)hawataipigia kura chadema!
Nk.
Kauli hizi zirekebishwe ili zilenge electorate wote kwa ujumla na si kubagua kwa namna yoyote, hata kama nia ipo ya kufanya hayo! Lugha nzuri itumike ili kuwaelimisha watz maana kila jambo jipya huwa haliaminiki mwanzoni!
3. Ahadi za huduma za jamii (km elimu) kuwa bure: Ahadi hii imekuwa questioned hata na watu wasioenda shule (watu wa kawaida). Hapa yanahitajika maelezo ya ziada na si kudai kuwa tutachukua fedha za epa ambapo hizo fedha zikiisha ndio inakuwaje! Majibu yangekaa kitakwimu zaidi, km kuna idadi kadhaa za wanafunzi, then kila mwanafunzi anagharimiwa kiasi fulani, then bajeti yetu ni kiasi fulani, etc.
haya ndio yangu kwa leo wanajf hasa wanaoitakia mema chadema!
Tujadili!
Hivi kazi ya JWTZ ni nini? Kwani kuna watu wanataka kupindua nchi? Ninaona JWTZ wanaingilia kazi za Polisi, kitu ambacho siyo jukumu lao. Kungekuwa na tetesi za machafuko ya kupindua nchi, hapo ningeweza kusema wana haki, lakini kama swala ni wananchi kutaka kulinda kura zao sioni nafasi ya JWTZ kwenye huu uchaguzi.
Sana sana Mnadhimu Mkuu wa JWTZ anazidi kuthibitisha kwamba hali ya CCM ni mbaya na sasa wameamua kutumia hata wanajeshi ili kutisha wapiga kura na wananchi.
Kwa nini wanaotaka kumwaga damu wasiende Muhimbili ambapo zinahitajika?
Mkuu Buchanan,
Nakubaliana na wewe kuhusu swala la kauli za damu itamwagika. Tatizo la siasa za Tanzania ni kwamba chama kikishaonekana kuwa threat kwa CCM, whether utumie lugha laini au nyepesi au kauli nzuri, bado tu utavikwa ubaya hata kama ni wa kuokoteza. So, hai-make any difference.
Swala la mafisadi/Mkumbwa Alli, nadhani hapo wanaweza kutamka tu kwamba serikali mpya itafuata utawala wa sheria. Including kuwashughulikia hao mafisadi. Hata asipotaja kwamba atawafikisha mafisadi mahakamani, bado mtu yeyote ambaye anajijua ana matatizo ya kifisadi, hawezi kukipigia kura chama ambacho anajua kitakuja kufuata utawala wa sheria. Hivi unategemea mtu ambaye amezowea kuishi kwa misheni town anaweza kuipigia kura CHADEMA hata wasiposema kwamba watawashughulikia mafisadi? Bado proportion ya mafisadi ni ndogo sana hata ukijumlisha na extended family zao. Mafisadi kwanza huwa hawana undugu wala ujamaa, unaweza kushangaa mtu fisadi lakini some of his/her extennded family wako choka mbaya na wakisikia kwamba jamaa kapatwa na kasheshe wanashangilia kabisa. Mzee mzima alipoachia Uwaziri Mkuu kuna some of his extended family members walishangilia sana.
ni kweli , kabisa wapenda mabadiliko wengi ni watu ambao sio criminal, kwahiyo mafisadi wananafasi ndogo sana ktk ushindi wa CHADEMAHatutaki kura za criminals. Hivyo sikubaliani nawe. Maana si watanzania wote ambao ni criminals. wengi wa watanzania ni watu wema sana na wamechoka na umaskini wa kufanyiziwa.
Tunahitaji hatua kali zichukuliwe kwa criminals full stop.
kabisa mkuluWapiga kura ni lazima wajue wanachochagua. Hakuna kuwalaghai. Ni lazima nchi igawanyike kati ya wanaounga mkono CCM na wanaounga mkono Chadema. Wananchi wajue Dr. Slaa akiingia atafanya nini. There is no middle ground.