Wakati mwingine tuiangalie shillingi kwa pande zake zote mbili. Labda huyu ndugu aliyeanzisha mada hii ama anasoma UDOM lakini ndio wale wale waliozoea ubwete huko walikotoka. Ni kweli ayasemayo lakini alipaswa kutoa whys za kwa nini vijana waombe au wasiombe.
ROMA haijajengwa kwa siku moja, Na zipo sababu za kwa nini hiyo Roma haijajengwa kwa siku moja. Na UDOM pia yawezekana ni vivyo hivyo. Yapo mapungufu kadhaa kwa chuo hiki, lakini pia zipo faida zake.
Huyu mtoa mada alipaswa kueleza pande zote mbili ili sasa muombaji apime.
1. inategemea mwombaji anataka asome nini, kwani unapozungumzia UDOM unazungumzia kapu kubwa ambalo ndani yake kuna vitu vingi, ndani ya UDOM zipo college sita ambazo zinajitegemea kabisa, zipo mbalimbali sana na hazitegemeani kabisa. Mazingira ya college moja sio sawa na ya college nyingine, hata mapungufu na mazuri ya college yanatofautiana kabisa.
Kwa kifupi, mtoa mada alitakiwa kutaja ni college gani ina mapungufu fulani, na mazuri yake fulani. Kusema tu kuwa UDOM haifasi sio jambo la busara sana kwani hata hivyo mambo ya uongozi hayadumu milele, mifumo inabadilika na labda ni suala la wakati tu litabadilisha fikra zake.
Tusubiri tuone........