Lad Jay Dee, The Pumpkin of the Old Homestead MUST NOT BE UPROOTED! maana halisi ya hiyo proverb ni USINYEE KAMBI. waswahili wanasema usisahau ulikotoka na aliyekutoa..
wanadamu tuna tabia ya kujisahau sana, haswa tupatapo mafanikio katika nyanja fulani zinazotuhusu. Kujisahau ni ugonjwa mkubwa tupatao sisi wanadamu. Lakini lazima tukubali kujisahau sio kuzuri, ebu jaribu kuvuta picha, hata tu ya kufikirika, vipi asingejitokeza yule mtu katika njia ya maisha yako, je leo ungekuwa hapo? ungekuwa ulivyo?
kamwe usijisahau kiasi cha kumtusi aliyekusimamisha, aliyekutoa katika aibu, aliyekufanya leo utembee na uonekane ulivyo...
Jide, redio ya watu ndio iliyokutoa, ndio waliokutambulisha katika anga ya muziki. maisha yako wewe ni matokeo ya moja kwa moja ya redio ya watu, leo ukitusi na kukebehi kiasi hicho ni kwamba hutafuti kingine zaidi ya laana.. wewe umeonekana kwa sababu ya redio ya watu, wale ndio waliokusimamisha, usisahau ulikotoka. Mumeo, kafundishwa ujanja na redio ya watu, kipaji chake kilionyeshwa na redio ya watu, ni redio ya watu ndio ilimlea na kumkuza. Biashara yenu, yaani Nyumbani Lounge, ni redio ya watu iliyotambulisha biashara yako, kumbuka, kumbuka fresh..... Leo mbona mnajisahau sana..
ushauri wangu: The Pumpkin of the Old Homestead MUST NOT BE UPROOTED!