Singo Batan
JF-Expert Member
- Apr 24, 2020
- 295
- 198
Nimefuatilia Press ya Katibu Mkuu wa CHADEMA Bw. John John Mnyika, akiitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhusisha vyama vya siasa juu ya manunuzi ya vifaa vyote vya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Mnyika anakiri kwamba Tume imeitisha zabuni ya manunuzi ya vifaa vya Uchaguzi zikiwemo Karatasi za kupiga Kura. Kwa Taarifa hiyo inathibitisha NEC imefuata taratibu za manunuzi ya Umma kisheria, Na kwa maana nyingine Mzabuni aliye shinda tenda ndiye aliyepewa kazi. Lakini Mnyika ameonesha wasiwasi juu ya Mzabuni wa Manunuzi ya karatasi tu za kupigia Kura (ballot papers) kuwa "kwa vyanzo vyao CHADEMA" Kampuni inayochapisha Karatasi iko Dar es salaam.
Kwa maoni yangu naona Bw. Mnyika anasahau kwamba kabla hajaifanyia uchunguzi NEC kupitia "vyanzo vyao" , yeye kama Kiongozi na mtendaji Mkuu wa Chama alitakiwa kufika NEC na apate Taarifa kuhusu manunuzi ya Vifaa mbali mbali yalivyofanywa kama kuna haja hiyo na (kwa basis ile ile) kwamba ni Manunuzi ya UMMA na kwa namna yoyote Taarifa zake zipo NEC sio kwenye "Vyanzo vyao"
Ikiwa Kampuni imeshinda zabuni na kupewa tenda ubaya uko wapi kiasi cha kutiliwa shaka na Mtu Mkubwa kama yeye?, Karatasi za kura zina maajabu gani yanayoweza kutiliwa shaka?, Ni nini umaalum wa kuona Afrika kusini wanaweza kuwa na sifa za ziada kuliko Jamana (Kama kweli Jamana ndio wametengeneza hizo ballot papers?)
Kama Chadema ambayo ni Taasisi, haijawahi kuingiliwa katika maamuzi ya manunuzi ya Vifaa vyake vya kazi na Taasisi nyingine yoyote, Je, Ni sawa kuishurutisha NEC kufuata matakwa ya CHADEMA?
Bw. Mnyika haoni kwamba kufanya hivyo ni kuingilia Uhuru wa Tume kama ambavyo anaaminisha Umma kwamba Tume hii haipo huru?, Unasisitizaje mabadiliko kama wewe hutaki kuwa Mfano?
USHAURI
Katika kutafuta Mafanikio kisiasa na hata kushika Dola ni vyema CHADEMA kikajikita zaidi kuonesha ubora wa sera zake kwa wananchi hasa katika siku hizi zilizobaki kuliko kila wakati kutafuta Migogoro na Migongano isiyo ya lazima na kuweka kila "kinachohisiwa hakipo sawa" mitandaoni au kwenye vyombo vya habari bila ya kufuata utaratibu wa kisheria ili kujiridhisha na jambo fulani na ikibidi kama haliko sawa kulizuia.