Ushauri wa bure kwa vodacom Tanzania

frakitosho

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2012
Posts
802
Reaction score
256
Kadri siku zinavyokwenda tunashuhudia makampuni ya simu yakifanya ubunifu wa aina mbalimbali. Tumeshuhudia tigo wakija na kabang na extreme ambayo inatumika masaa 24 ya ukweli na sio ku-expire kila saa sita usiku kama ilivyo voda bila kujali muda uliojiunga, airtel nayo ikaja na ofa kabambe ambapo sasa wateja wake wanapata dk 175 kwenda mitandao yote, sms kibao na mb 500 kwa matumizi ya wiki nzima. Voda wao wanajivunia kuenea kwa mtandao wao lakini wanasahau kuwa wateja wengi wa simu ni wa kipato cha chini wala hawaangalii ueneaji wa mtandao bali ni unafuu wa bei. Nawashauri vodacom wabadili mbinu yao (corporate strategy) ili wawe market oriented otherwise naona kabisa wanapotea sokoni.
 
Kwako dada Harriet Lwakatare (Head of Customer Care) ulitazame hilo wazo kwa umakini, kaeni na Kelvin Twissa mje na plan nzuri ya retention kwa wateja wenu.Kuna jamaa fulani alikuwepo Tigo kamata na baadae Tigo posta jamaa mrefu mweupe, nadhani alikuwa boss fulani wa hizo branches. Alikuwa ni mfasaha sana ktk kufanya huduma kwa wateja. Voda jirekebisheni.
 
Ni kweli kabisa ndugu Rock City vodacom wanatakiwa wajipange "jiratibuni"
 
Last edited by a moderator:
Airtel yatosha ndo mpango mzima. Voda nawaweka pending until further notice!
 
Wamekuja na huduma ya 'Cheka nao' ambapo kwa Tsh 500 unapata dk 20 za kupiga mtandao wowote! Kwa huduma hii wameichalenji hata extreme ya tigo ya dk 15, tigo kwenda tigo kwa tsh 400 hivi. Angalao Voda kwa hilo wamejitahidi
 
Wamekuja na huduma ya 'Cheka nao' ambapo kwa Tsh 500 unapata dk 20 za kupiga mtandao wowote! Kwa huduma hii wameichalenji hata extreme ya tigo ya dk 15, tigo kwenda tigo kwa tsh 400 hivi. Angalao Voda kwa hilo wamejitahidi

Soki sio kweli kwamba tigo extreme ni tigo kwenda tigo. Tigo extreme ni kwenda mtandao wowote. Isitoshe inadumu kwa masaa 24 ya kweli bila kujali umejiunga muda gani tofauti na voda ambayo cheka yao ina expire kila ifikapo saa 6 usiku bila kujali muda uliojiunga. Ina maana ukijiunga na cheka saa 5 na nusu usiku itadumu kwa nusu saa tu ina expire.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu frakitoshi,
Tigo extreme ni tigo-tigo tu isipokuwa sms ndo zinaenda mitandao yote. Tigo time ndo inakwenda mitandao yote kwa rate ya Tshs. 1.32/sekunde (VAT inclusive).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…