frakitosho
JF-Expert Member
- Dec 13, 2012
- 802
- 256
Kadri siku zinavyokwenda tunashuhudia makampuni ya simu yakifanya ubunifu wa aina mbalimbali. Tumeshuhudia tigo wakija na kabang na extreme ambayo inatumika masaa 24 ya ukweli na sio ku-expire kila saa sita usiku kama ilivyo voda bila kujali muda uliojiunga, airtel nayo ikaja na ofa kabambe ambapo sasa wateja wake wanapata dk 175 kwenda mitandao yote, sms kibao na mb 500 kwa matumizi ya wiki nzima. Voda wao wanajivunia kuenea kwa mtandao wao lakini wanasahau kuwa wateja wengi wa simu ni wa kipato cha chini wala hawaangalii ueneaji wa mtandao bali ni unafuu wa bei. Nawashauri vodacom wabadili mbinu yao (corporate strategy) ili wawe market oriented otherwise naona kabisa wanapotea sokoni.