Ushauri wa bure kwa Wakenya ili kupata amani: Wakataeni Uhuru na Odinga; tafuteni raisi kutoka kabila dogo


Ni ngumu sana kuutenganisha Ukikuyu na Ujaluo huko nchini Kenya kama ambavyo ni ngumu mno kuumaliza Uyanga na Usimba nchini Tanzania. Hivyo ushauri wako ulioutoa hapo kwa Wakenya ni sawa sawa na kupaka rangi Upepo au kusubiri Boti ya Azam Marine II Ubungo Terminal.
 

Mkuu umeongelea ugumu halafu ukatoa mfano wa kitu kisichowezekana. Hiyo ni contradiction katika uandishi.

Huwezi kusema ni vigumu sana kutembea Dar hadi Nairobi, halafu ukasema ni sawa na kupaka upepo rangi. Hizo ni context mbili tofauti kabisa. Unapaswa kulinganisha kusubiri Boti ya Azam Ubungo na kupaka rangi upepo.

Kuutenganisha Ukikuyu na Ujaluo Kenya inawezekana, japo ni ngumu. Kabla ya kuuwawa, Karume alianza kutenganisha Uarabu na Ubantu Zanzibar (japo wengi hawakukubaliana na njia zake), kitu ambacho huenda ni kigumu zaidi ya kutenganisha Ukikuyu na Ujaluo Kenya.
 

Mmmh, El Shabab watakasirika sana, maana utakuwa umewanyang'anya adui wa kupigana nae. Wanaweza wakatangaza vita dhidi ya Tanzania! Hawana lojiki hao watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…