Kenya sasa hivi kuna sintofahamu. Tume ya Uchaguzi imegawanyika, na imetoa tamko rasmi kwamba haiwezi kutoa guarantee uchaguzi ukifanyika wiki hii utakuwa huru na haki. Kamishna mmoja wa Tume hii alishatoa maelezo kwamba tume inapokea maelekezo "kutoka juu". Kwa sasa Uhuru anataka kulazimisha uchaguzi ufanyike, badala ya yeye kuachia uraisi kwa Spika wa Bunge kulingana na katiba ya Kenya, iwapo uchaguzi hautafanyika ndani ya siku 60 baada ya kubatilishwa.
Uhuru anasahau kwamba akilazimisha uchaguzi, matokeo yake yatapelekwa tena Mahakamani na kuna uwezekano mkubwa uchaguzi wa marudio kubatilishwa tena na Mahakama! Juzi hapa Uhuru alitoa mwito kwa raia wa Kenya kuiombea amani. Lakini je, suluhisho la Kenya ni kuiombea amani? Amani ili nani awe Raisi wa Kenya, Uhuru? Odinga?
Ukweli ni kwamba kwa hali iliyofikia Kenya kwa sasa, ushindi wa uraisi kwa Uhuru au Odinga hautakuwa ushindi kwa Kenya. Kenya imegawanyika mno kwa sasa, na ukiangalia kwa makini utaona kwamba ukabila ni chanzo kikubwa cha mgawanyiko wa kisiasa uliopo. Wajaluo hawatakubali kamwe ushindi wa Uhuru, na Wakikuyu hawatakubali kamwe ushindi wa Odinga.
Ushauri ninaotoa kwa Wakenya ni kwamba, wakataeni wote Uhuru na Odinga. Tafuteni raisi kutoka makabila madogo nchini Kenya ambayo hayajafungamana na Wakikuyu au Wajaluo. Hilo ndilo suluhisho pekee litakaloleta amani nchini Kenya kwa sasa.
Umenena vyema ila kilichopo kwa hii mijitu miwili ni kabila mbili kuu, upande wa Kikuyu una vikabila vidogovidogo nyuma yake na upande wa Mluo kuna vikabila vidogovidogo nyuma yake.
Hivyo ni vigumu sn kutenganisha watu hawa kwa kuwakepa kikuyu na mluo.
Na kwa kuona mbali ilionekana kuwa Odinga anaelekea kung'atuka ktk ulingo wa siasa na kuna kijana wake fulan alianza kuwa kipenzi cha waluo nae akazimwa ghafla,hapa tutegemee mambo mengi sana baada ya uchaguzi huu tata.
Ni kipi kitafuata Odinga ataweka mambo ya kisiasa kando au vipi na ni nani ataanza kuandaliwa kwa ajili ya 2020 na kuendelea?
Upande wa akina Uhuru nae ni nani ataandaliwa miaka iyo ijayo? Uchaguzi wa Kenya utaendea tu kuwa tata miaka mingi ijayo sababu kuu ya utata huo ni ukabila tu.
Wakenya mara nyingi mnajidai ni wasomi sn na kujiona watu wa high-high quality kumbe nyie ni bidhaa zilizofungashwa kwa makasha mazuri ya nje tu.
Wakenya ni nani aliyewaloga mpk mchaguane kwa ukabila? We mkenya unaesoma ujunbe huu unajionaje ukimchagua mtu kwa MKUMBO wa ukabila,sie Wa-Tz tuna makabila zaid ya 120 lakin tunaweza ishi mtaa moja tukaongea na kuwa marafiki hata zaidi ya miezi 3,4 bila ya kumjua mwenzio ni kabila gani.
Acheni hizo zenu za kishambashamba hapa kazi yenu kuwekana roho juu tu,watoto wenu wake zetu ikifika wakt wa uchaguz ni lazima muwaumize kisaikolojia familia zenu.
Je,ni kweli manajitambua? Jibu ni hapana hamjitambui.
Leo niishie hapa,sie wajanja tunaendelea kuwachora tu hasa kanzia kesho tunawapiga chabo tu mapovu yatakapoanza kuwatoka hiyo kesho.
Kwann msijifunze kweeeeetu Tz? Tunapiga kura bila kuangalia fulan ni kabila gani anatoka ukanda upi.
WATANZANIA HOYEEEEEEEE.
USHAURI WANGU NI KUWA BAADA YA UCHAGUZI WA KESHO SIKU ZIKIENDA SANA KUANZIA MWAKA WA KWANZA BAANDA YA UCHAGUZI,UNDENI TUME YA MARIDHIANO YA KUTOKOMEZA UKABILA.
MJE TANZANIA MTUULIZE SIE TUMEWEZAJE KUISHI BILA KUBAGUANA KIKABILA? KUANZIA KUISHI MITAAN,MASHULENI,MAKAZINI,KIDINI, MPK KTK CHAGUZI ZETU ZA SERIKAL,ZA MTAA,UDIWANI,UBUNGE MPK URAIS.
Naamin mkitoka na kurudi kwenu mkaanzisha semina hizo kutoka kwetu mtaanza kutoka ktk mfumo wa ukabila uliobobea kwenu.
Nawaombe Mungu wetu waepushe na janga hili la ukabila kuanzia kesho mjifunze kusameana.