Ushauri wa bure kwa Wakenya ili kupata amani: Wakataeni Uhuru na Odinga; tafuteni raisi kutoka kabila dogo

Ushauri wa bure kwa Wakenya ili kupata amani: Wakataeni Uhuru na Odinga; tafuteni raisi kutoka kabila dogo

NYANI AOINI KUNDULE............. MBONA NYINYI CCM MNASHINDWA KUWAKATAAA.............???
Wakenya toka mjue nyani haoni kundule imekuwa shida!😀😀

Kwani CCM kama Chama kina tatizo gani? Huku tunakataa watu sio chama au kabila, tatizo mlilo nalo sasa hivi. Tunajua issue sio Uhuru au Odinga, ni kabila la Uhuru na Odinga yanayopigiwa kura. Hata tunaweza kubadili jina la Wakikuyu na kuwa Wajubilee, na Wajaluo kuwa Wanasa!

Halafu nyie, haya mabo ya kuwa na koo za mabwana na watwana mnayatoa wapi? Kwani viongozi lazima wawe watoto wa Babu Kenyatta na Babu Odinga? Yaani Wakenya wengine haiko akili ya kuongoza?

Nasikia Kenya kila uchaguzi mnakuwa na vyama vipya! Hivi KANU ipo bado 😀?
 
Kenya sasa hivi kuna sintofahamu. Tume ya Uchaguzi imegawanyika, na imetoa tamko rasmi kwamba haiwezi kutoa guarantee uchaguzi ukifanyika wiki hii utakuwa huru na haki. Kamishna mmoja wa Tume hii alishatoa maelezo kwamba tume inapokea maelekezo "kutoka juu". Kwa sasa Uhuru anataka kulazimisha uchaguzi ufanyike, badala ya yeye kuachia uraisi kwa Spika wa Bunge kulingana na katiba ya Kenya, iwapo uchaguzi hautafanyika ndani ya siku 60 baada ya kubatilishwa.

Uhuru anasahau kwamba akilazimisha uchaguzi, matokeo yake yatapelekwa tena Mahakamani na kuna uwezekano mkubwa uchaguzi wa marudio kubatilishwa tena na Mahakama! Juzi hapa Uhuru alitoa mwito kwa raia wa Kenya kuiombea amani. Lakini je, suluhisho la Kenya ni kuiombea amani? Amani ili nani awe Raisi wa Kenya, Uhuru? Odinga?

Ukweli ni kwamba kwa hali iliyofikia Kenya kwa sasa, ushindi wa uraisi kwa Uhuru au Odinga hautakuwa ushindi kwa Kenya. Kenya imegawanyika mno kwa sasa, na ukiangalia kwa makini utaona kwamba ukabila ni chanzo kikubwa cha mgawanyiko wa kisiasa uliopo. Wajaluo hawatakubali kamwe ushindi wa Uhuru, na Wakikuyu hawatakubali kamwe ushindi wa Odinga.

Ushauri ninaotoa kwa Wakenya ni kwamba, wakataeni wote Uhuru na Odinga. Tafuteni raisi kutoka makabila madogo nchini Kenya ambayo hayajafungamana na Wakikuyu au Wajaluo. Hilo ndilo suluhisho pekee litakaloleta amani nchini Kenya kwa sasa.
Umenena vyema ila kilichopo kwa hii mijitu miwili ni kabila mbili kuu, upande wa Kikuyu una vikabila vidogovidogo nyuma yake na upande wa Mluo kuna vikabila vidogovidogo nyuma yake.

Hivyo ni vigumu sn kutenganisha watu hawa kwa kuwakepa kikuyu na mluo.

Na kwa kuona mbali ilionekana kuwa Odinga anaelekea kung'atuka ktk ulingo wa siasa na kuna kijana wake fulan alianza kuwa kipenzi cha waluo nae akazimwa ghafla,hapa tutegemee mambo mengi sana baada ya uchaguzi huu tata.

Ni kipi kitafuata Odinga ataweka mambo ya kisiasa kando au vipi na ni nani ataanza kuandaliwa kwa ajili ya 2020 na kuendelea?

Upande wa akina Uhuru nae ni nani ataandaliwa miaka iyo ijayo? Uchaguzi wa Kenya utaendea tu kuwa tata miaka mingi ijayo sababu kuu ya utata huo ni ukabila tu.

Wakenya mara nyingi mnajidai ni wasomi sn na kujiona watu wa high-high quality kumbe nyie ni bidhaa zilizofungashwa kwa makasha mazuri ya nje tu.

Wakenya ni nani aliyewaloga mpk mchaguane kwa ukabila? We mkenya unaesoma ujunbe huu unajionaje ukimchagua mtu kwa MKUMBO wa ukabila,sie Wa-Tz tuna makabila zaid ya 120 lakin tunaweza ishi mtaa moja tukaongea na kuwa marafiki hata zaidi ya miezi 3,4 bila ya kumjua mwenzio ni kabila gani.

Acheni hizo zenu za kishambashamba hapa kazi yenu kuwekana roho juu tu,watoto wenu wake zetu ikifika wakt wa uchaguz ni lazima muwaumize kisaikolojia familia zenu.

Je,ni kweli manajitambua? Jibu ni hapana hamjitambui.

Leo niishie hapa,sie wajanja tunaendelea kuwachora tu hasa kanzia kesho tunawapiga chabo tu mapovu yatakapoanza kuwatoka hiyo kesho.

Kwann msijifunze kweeeeetu Tz? Tunapiga kura bila kuangalia fulan ni kabila gani anatoka ukanda upi.

WATANZANIA HOYEEEEEEEE.

USHAURI WANGU NI KUWA BAADA YA UCHAGUZI WA KESHO SIKU ZIKIENDA SANA KUANZIA MWAKA WA KWANZA BAANDA YA UCHAGUZI,UNDENI TUME YA MARIDHIANO YA KUTOKOMEZA UKABILA.

MJE TANZANIA MTUULIZE SIE TUMEWEZAJE KUISHI BILA KUBAGUANA KIKABILA? KUANZIA KUISHI MITAAN,MASHULENI,MAKAZINI,KIDINI, MPK KTK CHAGUZI ZETU ZA SERIKAL,ZA MTAA,UDIWANI,UBUNGE MPK URAIS.

Naamin mkitoka na kurudi kwenu mkaanzisha semina hizo kutoka kwetu mtaanza kutoka ktk mfumo wa ukabila uliobobea kwenu.

Nawaombe Mungu wetu waepushe na janga hili la ukabila kuanzia kesho mjifunze kusameana.
 
Kenya sasa hivi kuna sintofahamu. Tume ya Uchaguzi imegawanyika, na imetoa tamko rasmi kwamba haiwezi kutoa guarantee uchaguzi ukifanyika wiki hii utakuwa huru na haki. Kamishna mmoja wa Tume hii alishatoa maelezo kwamba tume inapokea maelekezo "kutoka juu". Kwa sasa Uhuru anataka kulazimisha uchaguzi ufanyike, badala ya yeye kuachia uraisi kwa Spika wa Bunge kulingana na katiba ya Kenya, iwapo uchaguzi hautafanyika ndani ya siku 60 baada ya kubatilishwa.

Uhuru anasahau kwamba akilazimisha uchaguzi, matokeo yake yatapelekwa tena Mahakamani na kuna uwezekano mkubwa uchaguzi wa marudio kubatilishwa tena na Mahakama! Juzi hapa Uhuru alitoa mwito kwa raia wa Kenya kuiombea amani. Lakini je, suluhisho la Kenya ni kuiombea amani? Amani ili nani awe Raisi wa Kenya, Uhuru? Odinga?

Ukweli ni kwamba kwa hali iliyofikia Kenya kwa sasa, ushindi wa uraisi kwa Uhuru au Odinga hautakuwa ushindi kwa Kenya. Kenya imegawanyika mno kwa sasa, na ukiangalia kwa makini utaona kwamba ukabila ni chanzo kikubwa cha mgawanyiko wa kisiasa uliopo. Wajaluo hawatakubali kamwe ushindi wa Uhuru, na Wakikuyu hawatakubali kamwe ushindi wa Odinga.

Ushauri ninaotoa kwa Wakenya ni kwamba, wakataeni wote Uhuru na Odinga. Tafuteni raisi kutoka makabila madogo nchini Kenya ambayo hayajafungamana na Wakikuyu au Wajaluo. Hilo ndilo suluhisho pekee litakaloleta amani nchini Kenya kwa sasa.
Ushaambiwa ni wakabila, hilo Kabila dogo litapitaje?
 
Waongo tunajifanya kushauri sana kwa jirani wakati nyumban yetu ina harufu ya uchafu unaokaribiana na huo,uchaguzi wa Zanzibar una mizizi ya xina gani kama sio ukabila na udini?
 
Keep off Matters concerning Kenya.
Really, no East African cooperation spirit?

Anyway,may be Kenyans need to change the lyrics in the song

Jambo, Jambo bwana,
Habari gani, mbaya sana
Wageni, tahadharishwa
Kenya yetu, kuna matata

Kenya nchi mbaya - na kuna matata
Nchi isopendeza - na kuna matata
 
Mkuu, NASA NA JUBILEE wote waepukane na candidates wa uraisi wa makabila makubwa. Simple.
MKUU, hii kitu haioti kama Mchicha...
Anatengenezewa Misingi....
Ng'ombe hanenepi siku ya Mnada....
 
Really, no East African cooperation spirit?

Anyway,may be Kenyans need to change the lyrics in the song

Jambo, Jambo bwana,
Habari gani, mbaya sana
Wageni, tahadharishwa
Kenya yetu, kuna matata

Kenya nchi mbaya - na kuna matata
Nchi isopendeza - na kuna matata
Keep off Kenyan matters.
 
Hawa dawa yao ni kuwaweka chini ya utawala Wa kikoloni kwa miaka 10! They are not yet ready for freedom! Wakitawaliwa na Trump watafurahi zaidi!
 
Au suluhisho lingine ni kuigawana Kenya kati ya Uganda na Tanzania. Nusu ya juu iende kutawaliwa na Uganda na nusu ya chini iende kutawaliwa na Tanzania!
Wana katiba nzuri lakini isiyotekelezeka kwa kikwazo cha ukabila! Wakija huku kwa hapa kazi tu watanyoka fasta!
 
La, sio ukabila haswa, bali ubabe wa kisiasa kati ya familia mbili kuu za kisiasa.

Huu mgawanyiko waweza tokea hata kama wawaniaji kutoka "jamii ndogo" wakipigiwa upatu na familia hizi mbili hasimu (the Kenyattas and the Odingas).

Hawa ndio wanaendekeza hili uhasama unaosemekana kama ni ya kikabila hapa Kenya.
Kinachowapa shida kenya ni kuwa muungano wa vyama unaangalia kabila la mtu na sio masuala mengine, hivyo kuua ukabila itachukua mda!

Mfano, tunategemea uchaguzi ujao wakikuyu waungane na wakalenjini kumpigia debe ruto.

Siku mgombea wa kikikuyu akiungana na mluo tutajua ukabila mmeupa kikumbo, tofauti na hapo ni kazi sana!
 
Mkuu, kuna wakati nilisema dawa ya migongano kama hii ni Kenya ni kwamba, Jubilee wakiweka mgombea uraisi Mkikuyu, nao Nasa waweke Mkikuyu. Jubilee wakiweka Mjaluo na Nasa waweke Mjaluo!
Mabaya zaidi ni kuwa hakuna mkikuyu aliyeko nasa au atakayekubali kujiunga nasa, wala mluo aliyeko jubilee au atakayekubali kuwa huko.
 
Another thread by foreigners advising Kenyans how to go about their problems yet the same very advisors have been unable to lift their own country from an LDC.

Isn't it odd that the same LDC has a lower rate of youth unemployment than Kenya which leads the EA block with the highest rate of youth unemployment?
 
Isn't it odd that the same LDC has a lower rate of youth unemployment than Kenya which leads the EA block with the highest rate of youth unemployment?
LDC has no statistical data to prove its claims.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Man 39.1% is too much! No Wonder vijana wengi wanaonekana kwenye maandamano coz hawana kazi.

See how your fellow Kenyans complain. UN report exposes Kenya’s big jobs crisis

It reduces your inferiority complex.
 
Another thread by foreigners advising Kenyans how to go about their problems yet the same very advisors have been unable to lift their own country from an LDC.

the big five (GEMA et al) are in the middle income economy (the minority) and the rest are in uncomparable LCD.
 
Back
Top Bottom