Mtini
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 1,492
- 2,361
Nina mifano mitatu ya kweli kabisa:
1. Nimewahi kuingia gerezani kwa usiku mmoja, huko nilikutana na mtu mmoja aliyepewa kesi ya mauaji kwa sababu hii. Alikuwa anapita njia akakuta jamaa kadhaa wanampiga mtu, akabaki hapo kama mshangaaji. Siku kadhaa zikapita aliyepigwa akafariki, polisi wakaanza msako, wakadaka baadhi, baada ya kipigo wakaanza kutaja watu waliokuwepo, jamaa naye akatajwa.
Walipofika polisi hakujisumbua kurekebisha akajiaminisha mimi sijahusika, mwisho wa siku alijikuta kapanda mahakamani baadae gerezani. Kipindi naongea nae alikukuwa kishakaa mwaka mmoja huko magereza. Baada ya miaka miwili kupita tangu nilipomuona magereza nikakutana nae uraiani sikuweza ongea nae kwa kuwa mazingira hayakuwa rafiki.
2. Siku za karibuni jamaa mmoja namfahamu alikuwa anatoka msikitini jioni, akakuta watu wanapigana, akabaki kushangaa. Siku ya siku aliyepigwa kafariki, jamaa katajwa yuko ndani anaisaidia polisi.
3. Binafsi huwa sinaga tabia ya kushangaa vitu kama hivi, marehemu baba yangu alinihusia tangu niko darasa la pili kuhusiana na jambo hili kwa kuwa naye alishawahi kupona kimiujiza kwenye tukio kama hili.