Ushauri wa Haraka: Ameambiwa ana jipu Kichwani

makaghari

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2014
Posts
543
Reaction score
530
Habari za majukumu wana Jf.

Moja kwa moja niende kwenye dhumuni.
Rafiki yangu amepatwa na hali ambayo kwangu Mimi ni ya kushangaza lakini pia inaogofya kidogo. Amekuwa akitokwa na aina fulani ya kamasi ambayo anadai inachangamana na vijidamu puani, hasa hasa pale anapojaribu kupenga zile kamasi ambazo hutokea kwa juu (nadhani sote tunaelewa ile hali ya kutaka kutoa funda LA kamasi kwa kuzivuta kwa namna flani hivi kupitia puani).

Baada ya kuona hali hiyo kwa Siku kadhaa (kwa mujibu wake), Leo aliamua kwenda pharmacy moja hivi ambayo pamoja na mengine lakini wamemwambia kuwa anaweza kuwa na jipu kichwani kwa ndani ambalo ndilo huchangia hali hiyo.

Ndugu wana Jf, naomba kuuliza; Je, kuna uwezekano wa kuwapo na jipu kichwani? Na ili kubaini inafaa akapimwe kipimo gani.? Pili, hali hii huweza kutibiwa kwa tiba ipi? (mbadala au ya kisasa).

Natanguliza Shukrani.
 
Pharmacy siku hizi wana maabara?
Alikwenda pale kuchua dawa za mafua, lakini pia akaona sio mbaya aeleze kiundani hayo mafua ni ya namna gani, ndio akakutana na majibu ya namna hiyo hapo juu.
 
Jipu kichwani halina shida ni operation tu linaisha tatizo ni kwenye ubongo ,hapo ndo kuna mziki
 
Mtu unaumwa unakwenda duka la dawa? WaTz mbona tunafanya mambo yasiyo na mantiki?
 
Mwambie aende hospital kwa vipimo, ninaa ankal wangu aliwah kuumwa sana kichwa, alikua analalamika sana kichwa anameza paracetamol ikafikia hatua anaumwa had anazimia ndipo familia ikaamua kumpeleka hospital ya mkoa tanga - bombo, kule mpaka leo nashindwa kujua hospital kubwailishindwa nn kubaini tatizo mana wakamwambia hana shida ni malaria tu akaruhusiwa kurud nyumbani hali ikawa mbaya ikabidi apelekwe muhimbili akapimwa akakutwa na jipu kwenye ubongo, ikaamuliwa afanyiwe op akafanyiwa hakukaa sawa jipulikarud kwa kasi ni baada ya kumuangalia akafanyiwa ya pili hali ikawa ile ile ikabidi aangaliwe ikawa kansa akaanza mionzi kuchomewa, usikurupuke nenda hospital kubwa kwa vipimo zaidi asijekumezeshwa dawa ambazo sio zakutibu ugonjwa alionao
 
Nashukuru Sana kwa ushauri.. Nitamshauri afanye hivyo.
 
kujua kama ni jipi kichwani, kipimo murua kabisa ni CT Scan ya ubongo, hivyo hizo mambo za pharmacy aache, akapime kwanza..... na kama lipo, linatibika, kuna dawa, kuna operation, kulingana na hali ya jibu/uvimbe uliopo.
 
na pia kukutoa hofu, hakuna jipu/uvimbe kichwani bila kichwa kuuma, yani huwa kinauma haswaaa na hata utumie dawa ni nafuu tu kisha kinaendelea
 
Amefanya maamuzi yasiyo sahihi..hupaswi kujinunulua dawa UNLESS unakibali cha DAKTARI means: Ukiugua ni lazima kuanzia hospitali..na namshauri afanye hivyo.
 
Alikwenda pale kuchua dawa za mafua, lakini pia akaona sio mbaya aeleze kiundani hayo mafua ni ya namna gani, ndio akakutana na majibu ya namna hiyo hapo juu.
Unajua kaka, saa zingine naona Mkapa hakukosea kutuita watanzania wapumbavu. Sasa toka lini duka la dawa wanatoa diagnosis ya magonjwa?

Kwanza hii tabia ya kujisikia kuumwa na kwenda duka la dawa, badala kwenda kumwona daktari, ni ya kijinga sana. Na ni upuuzi wa wizara ya afya, umefanya hilo kuwa mazoea. Yaani hapa TZ unaweza kwenda duka la dawa na kupewa antibiotics bila hata ya kuwa na doctor’s prescription!

Mzee, kama umeweza hata kutumia JF, naamini una ka-elimu kidogo. Basi tumia elimu yako kumshauri huyo jamaa yako, aache kucheza na maisha yake. Next time, akijisikia kuumwa, aende hospitali na siyo duka la dawa.

[HASHTAG]#madashell[/HASHTAG]
 
Sasa makamasi yenye damu yana uhusiano gani na Brain Abscess??

Hao wanaouza Pharmacy wengi wao ni Pharmaceutical technician na ma nurse wenye certificate hawajawai kusoma magonjwa ya wanadamu kwa kina chake wanajua vitu basic sana sio watu wa kuamini sana!

Mpaka umejiridhisha na hiyo pharmacy ya watu wanao Operate hapo ndo unaweza kuwatumia na kwa issue serious bora uende hospitali na hapa nasisitiza neno "hospitali" na sio vituo vya Afya kwa issue ambazo zipo serious.

Pharmacy zipo pale kama umeishiwa na dawa zako labda au dawa zako umeandikiwa na daktari ndo uende pharmacy.

 
Mkuu na inakuaje kwa mtu ambaye anaona kichwani kumevimba na akigusa kabisa anaona uvimbe umetokeza lakini hana maumivu ya kichwa na amedumu nao huo uvimbe kwa takribani mwakamzima
uvimbe kama ni mgumu na hauna maumivu kabisa, huenda ni lipoma tu, so kuna haja ya kupiga X ray, kisha ukionekana upo kwa nje basi unaweza ukaondolewa bila shida
 
Kama anajipu kwenye ubongo (brain abscess) angekuwa na dalili kama : Kupata homa, dege dege, kupoteza fahamu, kuona ukungu, kichwa kuuma n.k. Hizo ndio dalili za Brain abscess; Hii inaonekana kwa kipimo cha CT scan ya kichwa.

Damu kutoka kwenye makamasi inasababu nyingi sana na yenyewe. Ni vizuri akaenda hospitali; kama shida yake ni kutokwa na damu puani ni vizuri akaonana na daktari wa Ear, nose and throat yaani ENT specialist ; kama yuko muhimbili unaeza ukaenda jengo la NOPD ( jengo jipya ) kuna clinic zao kule.

Ahsante
 
Na jipu shingonni ..ahingo ina niuma sana asee hosp wana sema hadi liive asee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…