Habari za majukumu wana Jf.
Moja kwa moja niende kwenye dhumuni.
Rafiki yangu amepatwa na hali ambayo kwangu Mimi ni ya kushangaza lakini pia inaogofya kidogo. Amekuwa akitokwa na aina fulani ya kamasi ambayo anadai inachangamana na vijidamu puani, hasa hasa pale anapojaribu kupenga zile kamasi ambazo hutokea kwa juu (nadhani sote tunaelewa ile hali ya kutaka kutoa funda LA kamasi kwa kuzivuta kwa namna flani hivi kupitia puani).
Baada ya kuona hali hiyo kwa Siku kadhaa (kwa mujibu wake), Leo aliamua kwenda pharmacy moja hivi ambayo pamoja na mengine lakini wamemwambia kuwa anaweza kuwa na jipu kichwani kwa ndani ambalo ndilo huchangia hali hiyo.
Ndugu wana Jf, naomba kuuliza; Je, kuna uwezekano wa kuwapo na jipu kichwani? Na ili kubaini inafaa akapimwe kipimo gani.? Pili, hali hii huweza kutibiwa kwa tiba ipi? (mbadala au ya kisasa).
Natanguliza Shukrani.