Ushauri wa haraka unahitajika

kindikwili

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2016
Posts
1,862
Reaction score
2,875
Wadau habari za muda huu?

Ndugu zangu kuna dada yangu alijifungua miezi miwili na wiki mbili nyuma kwa operation, wiki mbili hivi akiwa ameenda kutafuta huduma ya kupanga uzazi aliomba kwanza apimwe mkojo kubaini kama yuko salama au lah maana inaonekana alishaanza mambo ya ndoa na shemeji yangu.

Alipopimwa huyo aliyempima akamwambia nenda ukamwambie nesi una mimba ya wiki mbili. Kisha huyo dokta akamshauri kwamba njia nzuri ni kuitoa maana asingeweza kujifungua salama kwa maana bado mshono utakuwa bado, zaidi akamshauri atoe kiasi fulani kumsaidia hiyo shughuli.

Mdogo wangu huyo aliponishirikisha nikampa moyo na kumshauri akapime kwingine, alienda kupimwa mkojo hapo mtaani kwao kipimo aliniambia kinaitwa (UPT) akaambiwa ni NEGATIVE, nikambia hapana nenda kwingine wiki iliyopita kaenda tena kwingine akapima tena hicho kipimo akaambiwa ni NEGATIVE aliponitaarifu nikamwambia wakupime kipimo cha damu pia akaambiwa ni NEGATIVE.

Sasa wadau naomba nimeshindwa kujua ipi ni ipi, je nikweli huyu dokta wa zahanati hii alikosea kipimo au hawa wapimaji watatu wa mtaani kwao na huyu dada yangu ndiyo wanakosea?. Nini maoni yenu na ushauri kwa hili, nitashukuru sana kupata mawazo ya kila moja mwenye uelewa juu ya haya mambo.

Kindikwili from Ntwara tz.
 
mkuu mimba nyingi hutoka zikiwa changa au kuharibika kama aliona damu ajue ishachomoka hiyo.... muhimu kama vipimo vimeonyesha haipo basi haipo
 
Mkuu hapo inabidi uamini result tu kama mara tatu vituo tofauti majibu sawa.
Haina haja ya shingo ngumu kukubali hapo
 
haipo hiyo mkuu, mwambie aendelee na plan A,

ila huyo shemeji yako nae kiboko
 
Mimi sio dikta ila nlikuwa namshirikisha mtu hapa anasema " huyu hana mimba hapo ni kuwa bado hajarud ktk normal ndo maana vipimo vinaonyesha ni +ve but ukweli ni huo".
Hayo ni maelezo ya mzazi hapa ananieleza,wiki mbili ni muda mfupi sana
 
mkuu mimba nyingi hutoka zikiwa changa au kuharibika kama aliona damu ajue ishachomoka hiyo.... muhimu kama vipimo vimeonyesha haipo basi haipo

Aksante sana miss chagga kwa ushauri , off course hata yeye aliniambia aliona matone ya damu kidogo. Lakini miss chagga kuna mtu aliniambia mama aliyejifungua akiwa ananyonyesha ni vigumu kupata ujauzito japo inaweza kutokea, je kwa uelewa wako mama mwenye mtoto wa miezi miwili na wiki tatu anaweza kupata ujauzito? na je, kuona damu kidogo kama aliyoniambia kuna maanisha nini?
 
Mimi sio dikta ila nlikuwa namshirikisha mtu hapa anasema " huyu hana mimba hapo ni kuwa bado hajarud ktk normal ndo maana vipimo vinaonyesha ni +ve but ukweli ni huo".
Hayo ni maelezo ya mzazi hapa ananieleza,wiki mbili ni muda mfupi sana

aksante sana mkuu kwa kujali
 
haipo hiyo mkuu, mwambie aendelee na plan A,

ila huyo shemeji yako nae kiboko

Huyu shemeji bwana cjui ndiyo mwanaume machine hahahaaaa ila kama kaka mtu lazima nijali, tusije tukampoteza dogo mkuu
 
huko kuona damu kama alikuwa nayo inaweza kuwa imetoka .... kama anayonyesha vizuri hasa nyakati za usiku ndiyo njia nzuri ya kutokupata mimba ila kama anamtoto mvivukunyonya aisee atafute mbadala mapema ..........
 
Huyu shemeji si mvumilivu.anaanza kukatika katika kiuno ilihali mshono bado mbichi.maana najua bado anaharufu ya madrip ya operation.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…