kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,875
Wadau habari za muda huu?
Ndugu zangu kuna dada yangu alijifungua miezi miwili na wiki mbili nyuma kwa operation, wiki mbili hivi akiwa ameenda kutafuta huduma ya kupanga uzazi aliomba kwanza apimwe mkojo kubaini kama yuko salama au lah maana inaonekana alishaanza mambo ya ndoa na shemeji yangu.
Alipopimwa huyo aliyempima akamwambia nenda ukamwambie nesi una mimba ya wiki mbili. Kisha huyo dokta akamshauri kwamba njia nzuri ni kuitoa maana asingeweza kujifungua salama kwa maana bado mshono utakuwa bado, zaidi akamshauri atoe kiasi fulani kumsaidia hiyo shughuli.
Mdogo wangu huyo aliponishirikisha nikampa moyo na kumshauri akapime kwingine, alienda kupimwa mkojo hapo mtaani kwao kipimo aliniambia kinaitwa (UPT) akaambiwa ni NEGATIVE, nikambia hapana nenda kwingine wiki iliyopita kaenda tena kwingine akapima tena hicho kipimo akaambiwa ni NEGATIVE aliponitaarifu nikamwambia wakupime kipimo cha damu pia akaambiwa ni NEGATIVE.
Sasa wadau naomba nimeshindwa kujua ipi ni ipi, je nikweli huyu dokta wa zahanati hii alikosea kipimo au hawa wapimaji watatu wa mtaani kwao na huyu dada yangu ndiyo wanakosea?. Nini maoni yenu na ushauri kwa hili, nitashukuru sana kupata mawazo ya kila moja mwenye uelewa juu ya haya mambo.
Kindikwili from Ntwara tz.