Ushauri wa haraka wana JF wenzangu

Ushauri wa haraka wana JF wenzangu

zamlock

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2010
Posts
3,840
Reaction score
659
Nilikuwa na kesi na takukulu hukumu Yangu imetoka Jana nikahukumiwa kifungo Cha mwaka mmoja au kulipa faini nilicho kifanya nikalipa faini nikapewa zangu risiti nika bwaga cha kushangaza baada ya Kama masaa mawili watu wa Takukulu wananipigia Simu eti niende ofisini kwao nikashuhudie wanafunga file langukwkwa vigezo kwamba asije akatokea mtu mwingine akachukua file akanishtaki je wana Jf sheria inasemaje kuhusu hilo?
Je ningekuwa nimekwenda gerezani wangefungaje hilo file? Ushauri niende au nisiende?
 
Kawaida kwa makosa ya jinai mtu akishtakiwa na hukumu ikatoka hawezi shtakiwa tena kwa kosa hilo. Pia hukumu ikitoka na mshitakiwa akapewa altenative ya kulipa faini na akalipa basi mambo yote yanaishia hapo. Hili la kwenda kufunga faili usiwaamini wala usiende. Faili lako lishafungwa baada ya mahakama kusoma hukumu. Faili lao hata wafanyaje hawana uwezo tena wa kukushtaki kwa kosa hilo. Usiogope, Yote haya yapo kwenye sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, sura ya 20
 
Haukuwa na mwanasheria? Ungemuambia wakili wako aende. Mie sitaki kabisa kukutana na hayo majambazi yanayovaa suti. Wanataka kukutoa upepo hao, file linakaa takukuru ama linakuwa mahakamani? Na kama haujapata hukumu iliyoandikwa bado utaenda na nini? waambie wakuandikie summons:hand:
 
Wanataka kumtoa upepo tu hao hawana lolote


Haukuwa na mwanasheria? Ungemuambia wakili wako aende. Mie sitaki kabisa kukutana na hayo majambazi yanayovaa suti. Wanataka kukutoa upepo hao, file linakaa takukuru ama linakuwa mahakamani? Na kama haujapata hukumu iliyoandikwa bado utaenda na nini? waambie wakuandikie summons:hand:
 
Wanataka wakubabmbike kesi ya pili..... jamaa wana njaaa hao zaidi ya trafiki.
 
Preventing and combating corruption wanataka kimtoa upepo tena, hii sasa kazi kweli kweli!
 
Back
Top Bottom