Nchi yetu ina mabonde mengi yafaayo kulima migomba na hatimaye tunaweza vuna ndizi, kuna nyika nzuri ambazo zikilimwa kwa kumwagilia tunaweza pata zao lingine la biashara. Zipo aina nyingi sana za migomba na hata hybrid zipo. Migomba ni annual plant, sina hakika sana kama ni binual. Mkungu mzuri pale mahakama ya ndizi Mabibo unafikia Tsh 20,000/ ( hii bei ni ya mwezi wa pili 2013, sijui leo), kule Mbingu mwezi huo huo ilikuwa ni Tsh 5000/ kwa wakulima.
Eka moja huoteshwa migomba kama 500 ikiwa spacing itakuwa 3m x 3m. Kama ukiwa na eka kumi za mgomba huko Mahenge/Kilosa utakuwa na migomba 5000, na kama utavuna mikungu 300 kwa mwezi utapata 1,500,000/ ukiwa shambani na ukapata 10,000,000/ kama utafikisha Mabibo. Hapa nazungumzia mshale/mzuzu.
Gharama za matunzo si kubwa, na magonjwa si mengi, zaidi sana ni maji na thinning ili kupata mazao bora, mbolea ni muhimu.
Najua kuna watalaamu wengi sana wa kilimo, mimi nimechokoza maada ili kwa pamoja tuishambulie na kutoka na kitu kizuri kwa faida yetu sote, kukiwa na kosa nisamehewe bure. Kwa sasa Wachina wanajenga daraja la mto Kilombero, twendeni Mahenge tukalime mgomba.