Ushauri wa kifedha kwa vijana

Ushauri wa kifedha kwa vijana

Michael Chairman

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
922
Reaction score
586
Habari za mchana wanabodi, natumai muwazima,

Ufuatao ni ushauri kidogo wa kifedha ambao kwa kiasi kikubwa ukifuatwa unaweza kutoa tija ya kila anayeufuta.

1.Usitumie fedha kwenye vitu unavyofikiri unavihitaji kuwa navyo tumia kwa mahitaji muhimu.

2.Usinunue vitu ili kuongeza uwezo wako wa kujiamini hilo ni kaburi la kiuchumi.

3.Jifunze kufanya na kutengeneza (bidhaa) vitu vyumbani kwako kwa mfano kwa masuala ya chakula, udobi , n.k

4.Ukitaka kununua kitu ambacho si hitaji la muhimu na chenye gharama jipe muda zaidi ili uweze kuondoa hisia kwenye matumizi ya fedha, jipe hata wiki moja kisha utaona kama bado unakipenda kukinunua hicho kitu basi nunua.

5.Kumbuka kila mara kushindanisha unapokuwa kwenye manunuzi kati ya gharama na ubora.

6.Kamwe usifanye manunuzi vitu vikiwa vinaingia sokoni yaani ( new product) hivi vitu huwa na gharama ya juu sana ni tofauti na vikaa sokoni kwa miezi mitatu na mfano wa vitu hivyo ni pamoja na simu, Tv, gari, mavazi hasa ya akina mama na vijana.

Kumbuka kuishi kwenye kipato chako kamwe usiige na hakuna ubaya wowote kutunza fedha na kutumia kidogo wote wenye uhuru wa kipato ni wale waliojifunza kutumia kidogo ya kile wanachapota.

Ongeza na wewe kanuni za kifedha bora kwa usawa wa jamii yetu.
 
Tumia pesa kwenye mambo unayoyaitaji, sio unayoyataka.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Anyaway naupokea kwa wasiwasi sababu umetoka kwa kijana wa lumumba
 
Back
Top Bottom